Samson Ernest
JF-Expert Member
- Aug 28, 2014
- 1,118
- 1,565
Isa 40:29 SUV
[29] Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo.
Sio ajabu siku za leo kukutana na ndugu katika BWANA amechoka sana, hana hamu tena na ibada, huduma, na ile hamu ya kuendelea mbele kwa maisha ya wokovu haipo tena. Kutokana na magumu anayopitia katika maisha yake.
Kukutana na mtu aliyekata tamaa, aliyepoteza nguvu za kiroho na kimwili, aliyepoteza kabisa matumaini kwa Mungu na yale aliyomwomba, narudia kusema sio ajabu katika siku za leo.
Pamoja na kupoteza matumaini na kukata tamaa, habari njema ni kwamba Mungu anamwangalia kwa huruma mtu aliyekutana na hali hii na kumpa nguvu mpya. Pale anapomwita juu ya hali yake, Mungu humpa tena nguvu za kusonga mbele.
Haitajalisha hali hiyo imempa udhaifu mkubwa kiasi gani, haijalishi amekaa katika hali hiyo ya kukata tamaa kwa muda gani, Mungu anaweza kumwinua tena na kumpa uwepo mpya wa kushinda changamoto ngumu.
Mungu wetu hayupo kama mlinzi tu, hata pale tunapojikuta katika hali ya kupungukiwa nguvu kutokana na changamoto ngumu tulizokutana nazo au tunazopitia katika maisha yetu, Yeye anaweza kumpa nguvu mpya yule anayemtegemea na kumtumaini.
Hatuna haja ya kukata tamaa, hata pale tunapojikuta tumepoteza vitu tulivyokuwa tunavipenda katika maisha yetu, tunaye BWANA wa marejesho, nguvu zake hazina kikomo.
Tambua ya kwamba katika hali yeyote utakayokutana nayo ya udhaifu, ipo neema ya Mungu inayoweza kukuinua tena na kukusaidia kusonga mbele katika maisha yako.
2 Kor 12:9 SUV
[9] Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.
Usichoke kiasi cha kujikataa, yupo Mungu anaweza kukutia nguvu zingine tena, neema yake ni kubwa mno kwako, huna haja ya kufikia hatua ya kujikinai na kujiona peke yako, unaye Mungu mkubwa sana katika maisha yako anayeweza kukutoa eneo gumu.
Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana