Hili linaweza kuwa somo gumu hata kwangu mtoa mada,lakini nitajitahidi kueleza kadiri ya uwezo wangu
'
Wakati Mungu anatukataza tusile matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya,huenda Mungu alikua na maana kubwa sana kwetu wanadamu
'
Ni muda mrefu sasa nimekua nikitafakari ni nini lengo la Mungu kutaka tusijitambue,nilichokigundua kutoka kwenye tafakari yangu ndo leo nimeona nije hapa ili niongeze majibu lakini pia niwajuze kile nilicho kigundua lakini zaidi sana mnikosoe,hii naamini ndio njia nzuri ya kujifunza
'
Nimegundua kuwa KUJUA ndio chanzo cha ubaya na uovu wote
'
KUJUA ninakokuzungumzia ni kupata ufaham wa yale uliyokua huyajui,mfano;
'
NIKIJUA ulipoweka fedha zako nitakuibi kirahisi sana
'
Wanadamu tulipopata KUJUA namna mwili wa binadamu unavyofanya kazi ndipo watu wametengeneza sumu na silaha mbalimbali ili kumuangamiza binadamu mwenzao
'
Nchi jirani ITAKAPOJUA siri ya nchi nyingine,chi hiyo usalama wake unakua mashakani
'
Hata jirani yako ANAPOJUA siri zako,unakuwa na mashaka
'
Mifano ni mingi sana lakini ukitafakari ujagundua kuwa,KUJUA kuna faida na hasara,lakini inaonekana hasara ni nyingi ukilinganisha na faida
'
Sijui kama nimeeleweka kile ambacho nasema hapa lakini mpaka sasa naamini binadamu amekua mhanga mkubwa sana wa KUJUA au UFAHAMU
'
Hapa ndipo ninapoiona sababu ya Mungu kutuzuia KUJUA au kupata UFAHAMU,inaonekana hatuna uwezo wa kuwa na UFAHAMU kwa kuwa umetuletea maumivu badala ya nafuu,hatukutakiwa tuwe na UFAHAMU kabisa
'
Hapa ndipo napata ujasiri wa kusema,KUJUA au UFAHAMU ndio chanzo cha uovu wote duniani
'
Wewe unasemaje?
Umekoment hivi baada ya kujifahamu au..?Umetoa wapi haya?Nani amesema haya?JF ina vilaza sana siku hizi!
Umejenga hoja yako vizuri lakini sikubaliani na hitimisho lako kuwa chanzo cha uovu ni kujua. Kwa mimi nahitimisha kwa kusema chanzo cha uovu wote ni UKAIDI. kama mwanadamu asingekaidi agizo la Mungu la kutokula tunda la kati basi asingepata matatizo wala uovu wowote. Mfano unaweza USIJUE kama nina hela lakini ukanisachi ili iniibie ikiwa utazikuta, hapo kama USINGEKAIDI amri ya kuiba usingefikia kunisachi.
Kujua kumetufanya tuwe wajinga badala ya kuwa werevu na ndio maana wajuaji wengi mwishowe hupata hasara na hasara hiyo wamejitakia wenyewe
ndio maana hata Mungu alisema mwanadamu anaangamia kwa kukosa maarifa kwani hakutaka tuwe wajuaji bali tuwe na maarifa.
Kama mwanadamu angetumia maarifa ni dhahiri asingekula lile tunda, lakini kwa kujifanya mjuaji ndipo akala tunda na sasa anavuna maumivu
Tetra tumejua kuwa aliyetaka tuju alitaka nini......
'
Kwanza alitaka tuasi
'
Pili atimize ahadi yake aliyomwambia Mungu kuwa anahakikisha mwanadamu anakua upande wake(Lucifer)
'
Wakati fulani nilipata kupanda basi na jamaa mmoja ambae baadae nikaja kujua ni mwanachama wa Freemason
'
Aliniambia kuwa,nyie mnaomwabudu Mungu mnachekesha sana,iweje mumwabudu ambae ni dikteta?
'
Akasema,sisi tunamkubali sana Lucifer kwa kuwa ndie alitupa mwanga na ujuzi,mnae mwabudu alitaka muwe gizani!
::
Eiyer
Siku zote anaekufuata fuata ujue umemzidi jambo.
Lucifer na wafuasi wake wanalijua hilo ndo maana hawaishi kuweka viitikio visivyoimbika.
TUFUATE UFAHAMU WA KWELI upo TUPONE.
Hao wanadhani wapo ktk Mwanga kumbe ktk jua kali la mchana bado wanawasha tochi ili waone.
Mpe huruma
=
Huyu tayari ANAJUA kuwa unaweza kuwa na hela ndo maana anaingiza mikono yake mfukoni mwako!