Chanzo cha ndoto ya kuhamia Dodoma ni Karume

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,276
IMG-20160801-WA0065.jpg
Nawashukuru marafiki wote mliofuatilia mahojiano yangu katika runinga ya Startv kwenye kipindi cha tuongee asubuhi...

Mada ilokuwa: Kuhamia kwa serikali Dodoma,

Tumejadili kwa mapana lakini mimi nilialikwa kama mchambuzi wa masuala ya kiusalama, hivyo suala hili nimelieleza kiusalama zaidi... Pamoja na yote, nimeunga mkono kusudio la kuhamisha ikulu, lakini nimepinga njia zinazotumiwa na serikali katika kutimiza hili na pia nimeshauri hatua za kufuata,

Nimeeleza kuwa ujenzi wa ikulu ni mchakato unaotakiwa kuenenda sawa na bajeti ya nchi, ni mchakato unaotakiwa kuwa na azimio la bunge, na sio hizi propagana na papara za serikali...

Nimeeleza pia kwamba kuna wizara sio lazima ziende Dodoma au ziwepo Dar, mfano wizara ya kilimo inaweza kwenda Iringa au Mbeya, Wizara ya maliasili na utalii inaweza kwenda Arusha au Manyara huko ambako ndiko utalii ulipo... Lakini kuna wizara ambazo nilazima ziwe pamoja na Ikulu, mfano wizara ya fedha, wizara ya ulinzi nk.

Tujifunze hili ambalo lipo katika Kitabu kiitwacho Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi....

Katika kipindi kuanzia 1968-1972 uhusiano kati ya Nyerere na Karume ulikuwa mbaya sana kiasi cha kudhalilishana kwenye majukwaa na mawasiliano kuvunjika kabisa mpaka kifo cha Karume kilipotokea.

Wote walikuwa wanatumia wasaidizi wao kuwasiliana na hata hili likakatika pale Karume alipomfukuza ki-kuku Ikulu Waziri wa Fedha, Amir Jamal hata kufikia kupata mshituko wa moyo na kulazwa hospitali.

Hali ilitirubuka zaidi pale Karume alipoanzisha "ndoa za lazima" ambazo zililaaniwa duniani kote pamoja na Tangayika. Kenya walienda mbali zaidi ya kutoa tamko la kulaani zoezi hilo na kumpachika jina " lisiopendeza" Rais Karume.

Karume alijibu mapigo na kumuonya Kenyatta kuwa Zanzibar ina uwezo wa kuipiga Kenya kijeshi na ina miliki silaha zenye uwezo wa kupiga zaidi ya maili 600 kutoka Zanzibar. Ikimbukwe kuwa wakati huo Zanzibar ilikuwa ni ( closed society) na inajuulikana kwa usiri kama "Cuba of Africa" na katika toleo moja la Reader's Digest lilisema kuwa kisiwa cha Zanzibar kitazama kwa kujilimbikizia silaha nzito kutoka China na Urusi.

Siku ya pili tu, ujumbe mzito kutoka kwa Rais Kenyatta uliwasili Zanzibar kuja kuomba radhi na kufuta tamko lao. Nyerere pia altaharuki hasa baada la gazeti la serikali yake Tanzania Standard lilipopigwa marufuku lisiingie Zanzibar.Hapo ndipo hisia za usalama zilipoanza kuchomoza.

Baada ya kuuwawa Karume na Wanajeshi wa JWTZ na hali kutulia ndoto ya kuhamia Dodoma iliyeyuka kiuhalisia na mkazo ukaanza kupooza.

Je, sababu zilizopelekea kuotwa kwa ndoto hiyo zimeibuka tena hivi sasa au ni sababu nyengine mpya?
 
Mh wote mtoa mada na yeriko waongo.kwasababu navojua azimio la kuamia dodoma ni 1973. Na karume kafa 1972.sasa nyie mwatuaminisha kwamba nyerere alimuogopa karume ndio maana akataka kuamia dodoma wakat azimio lilianza baada ya kufa karume.sipend siasa ila historia umetudanganya
 
mmh hii ngumu kumeza..

ukiachana na azimio la kuhamia dodoma 1973 na miaka michache baadaye kuundwa kwa CDA.. Pia serikali ilifanya attempt kuhamia dodoma miaka ya 80, ambpo wizara saba zilihamia.
yote haya yalifanyika baada ya Mzee Karume Kutangulia mbele za haki.

Ingawa swali hapa ni kwamba kwanini serikali imefanya haraka haraka hivyo kuhamia dodoma sasa..?
kipi kilichoisukuma.?
 
Mh wote mtoa mada na yeriko waongo.kwasababu navojua azimio la kuamia dodoma ni 1973. Na karume kafa 1972.sasa nyie mwatuaminisha kwamba nyerere alimuogopa karume ndio maana akataka kuamia dodoma wakat azimio lilianza baada ya kufa karume.sipend siasa ila historia umetudanganya

Umesaidia sana kuweka kumbukumbu vizuri, naomba Yericko baadhi ya mambo unayoandika ukapata ufafanuzi sahihi kwa watu sahihi, wakati mwingine unaandika vitu ambavyo havipo/havikuwapo hivyo unapotosha ukweli, tamko la kuhamia Dodoma lilitolewa 1973, karume kauwawa 1972 tishio la usalama kwa kumuogopa Karume limetoka wapi?

Kususua kuhamia Dodoma wakati wa Nyerere kulichangiwa na mambo mengi nakupa(Yericko) chache kwa tafakari yako kuvunjika kwa jumuia ya Afrika mashariki kulilazimisha serikali kutumia sehemu kubwa ya rasilimali katika kujenga taasisi zake ili huduma zisisimame mfano kuagiza vichwa vipya vya treni toka Canada, kununua ndege mpya, kuboresha taasisi ya ukusanyaji mapato, shirika la posta na simu, bandari na mengineo,

wakati nchi ikiendelea kuimarisha hayo nilioeleza hapo juu ghafla nchi ikaingia katika vita vya Kagera hivyo kufanya matumizi makubwa ya akiba ya nchi kutumika kugharamia vita, hivo ni rahisi kusema Mwalimu alishindwa kuhamia Dodoma lakini yakupasa kutafuta sababu zilizofanya asifanikiwe, baada ya vita nchi iliingia kwenye mdororo wa uchumi sababu fedha nyingi ilitumika kwa hiyo nchi ilianza kujenga uchumi upya wakati wa mzee ruksa, tufanye kautafiti kadogo
 
Mh wote mtoa mada na yeriko waongo.kwasababu navojua azimio la kuamia dodoma ni 1973. Na karume kafa 1972.sasa nyie mwatuaminisha kwamba nyerere alimuogopa karume ndio maana akataka kuamia dodoma wakat azimio lilianza baada ya kufa karume.sipend siasa ila historia umetudanganya
Umetumia hoja dhaifu sana kujibu hoja nzito.
Tuchukulie kuwa Karume kweli alifariki Mwaka huo wa 1972. Azimio la Serikali kuhamia Dodoma likatoka mwaka 1973. Swali la kujiuliza, Je, ni sababu zipi zilipelekea wazo hili kuibuka mwaka mmoja baada ya kifo cha Karume?
Je, haiwezi kuwa Mwalimu alibaki na mashaka na Kisiwa cha Zanzibar?
Kuna wakati Mwalimu aliwahi kunukuliwa akisema angekuwa na uwezo angekisogeza mbali Kisiwa cha Zanzibar, Je, hii haiwezi kuwa moja ya sababu za kuhamia Dodoma?
Wakati mwingine huitaji kupinga kila jambo badala yake iruhusu akili yako itafakari!
Hata hivyo zipo sababu pia za kusogeza huduma za Serikali karibu zaidi na mikoa mingine ya Nchi kwa sababu Dodoma ni kama katikati ya Nchi.
Hata hivyo yapo maswali yanayohitaji majibu, Kwa nini Mwalimu hakutekeleza wazo lake hili? Kwa nini Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa na Mzee Kikwete pia walitelekeza wazo la Mwalimu?
Kama suala lilikuwa kusogeza huduma kwa wengi, wote hao wangelipa kipaumbele. Lkn hawakulipa uzito unaostahili. Je, wazo la usalama wakati ule wa 1973 ndo ilikuwa sababu halisi???
 
We mi si mwanasiasa na wala sijamjibu kisiasa wewe.nimemjibu kihistoria narudia tena wewe hujui historia
 
Na siitaji mjadala wa kisiasa maana mi nimemuelezea karume kafarik kabla ya mpango wa kuamia dodoma tofaut na maelezo yake.
 
Back
Top Bottom