Heshima Kwenu Wadau.
Nasumbuliwa na tatizo linalosumbua akili yangu sana. Mke wangu anawashwa sana mwili wote na hasa maeneo ya Paja la upande wa kulia kwa juu karibu na maeneo yake Mahsusi hali imekuwa mbaya kiasi muwasho unapocharuka anaacha kila kitu na kuanza kujikuna.
Kwa upande wangu huwa napatwa na muwasho mkali maeneo yangu nyeti hasa kuzunguka shingo ya "Babu" na vipele hutokea japo hali hii hutokea kwangu mara chache hasa siku ya pili baada ya kukutana kimwili na Mke wangu.
Mbaya zaidi ( na kwa uwazi zaidi) ninapokutana na Mwanamke wa nje (mchepuko) baada ya siku 2-3 ananipa taarifa ya kwamba anawashwa sana maeneo nyeti. Na taarifa hizi nimezipata kwa michepuko mitatu kwa nyakati tofauti ndani ya miaka miwili.
Tatizo la muwasho kwa mke wangu limeanza miaka mitatu iliyopita na tumeshapata mtoto pamoja na yote haya.
Kwa kipindi chote tumekuwa tukijitahidi kutafuta tiba hospitalini sana, bila mafanikio. Mwanzo tuliambiwa ni Fangazi na kuandikiwa madawa ya kupakaa na kumeza na hata sindano kwetu sote bila mafanikio pia. Tumepima Kaswende hadi VVU tangu mwaka jana kwa mara ya kwanza na hivi majuzi tar. 29-Mei Kaswende na VVU kwa mara ya tatu kila baada miezi mitatu na matokeo ni hatuna maambukizi ya VVU kwetu sote pamoja na mwanetu.
Nimekuja hapa JF baada ya kupitapita huku na huko nikafanikiwa kupata jukwaa hili. Natumaini nitasaidiwa japo kwa ushauri.
Natanguliza shukrani..