Chanzo cha El Clasico

Nihzrath

Member
Jan 15, 2013
51
116
KUELEKEA "EL CLASICO" WEEKENDI HII.

UPINZANI WAO ULIANZIA HAPA

Ni katika ardhi iliyopo Manispaa ya San Lorenzo. Mahali ilipo hifadhi ya 'Siera de Guadarrama' ni hifadhi iliyozungukwa na vilima vingi, na miamba yenye kuvutia, ndipo mahali lilipo Kanisa la 'Valle de los Caidos'. Ni kilomita chache na ulipo mji mkuu wa Madrid. Mahali hapo ndipo ulipolala mwili wa mwanaume mmoja maarufu sana aliyeitwa Francisco Paulino Hermenegildo Teodulo Franco Bahamonde, na jina lake maarufu sana aliitwa Generali Franco, ama "El Caudilo" kama wahispania walivyopenda kumuita yaani 'Kiongozi'.

General huyu aliyezaliwa mwaka 1892 na kufariki mwaka 1975 mjini Madrid. Aliongoza nchi ya Hispania kutoka mwaka 1939 baada ya kumalizika vita vya wenyewe kwa wenyewe hadi mwaka 1975 alipofariki.

Ni mwanaume huyu ndie aliyekuja kuwa chanzo cha kuzaliwa "El Clasico" na kuongeza upinzani wa mechi kati ya Real madrid na Barcelona, kabla yake hakukuwapo na upinzani baina ya timu hizo kama ulivyo sasa. Pamoja na kuwa kiongozi wa nchi ya Hispania Generali Franco hakuficha mapenzi yake kwa Real Madrid, na aliipa kipaumbele Real Madrid kuliko timu nyingine.

Ni upendeleo huo wa watawala kwa Real madrid ulianza kuchukiwa na baadhi ya vilabu vingi ikiwemo Barcelona. Kuimarishwa kwa huduma za kijamii katika mji wa Madrid mahali ilipo timu ya Real Madrid na kutopewa kipaumbele kwa wananchi wa jimbo la Catalunya katika huduma za kijamii, kulipelekea kuhamsha chuki za wakazi wa jimbo la Catalunya dhidi ya timu ya Real Madrid na utawala mzima wa Franco.

Mechi hiyo ikaanza kuchukuliwa kwa mtazamo wa kisiasa. Real Madrid ikatazamwa kama inawakilisha utaifa wa Hispania na Barcelona ikatazamwa kama anayewakilisha utaifa wa Catalani, ndipo chuki zikaanzia hapo. Ni tarehe 13,juni 1943 ndipo hasa uhasama ukazaliwa baada ya Barcelona kupigwa goli 11-1, kipigo kilichobakia kuwa rekodi mpaka hivi leo. Ilikuwa katika nusu fainal ya Kombe la 'Copa de Generalismo" sasa inajulikana kwa jina la Copa de ley.

Kuna maelezo kuwa kabla ya mechi hiyo wachezaji wa Barcelona walitishwa na polisi wa nchi hiyo, na ilifikia Mwenyekiti wa Barcelona kipindi hicho Enric Pineyro kushambuliwa na mashabiki wa Madrid. Viongozi wa Barcelona walilalamikia hatua hiyo lakini hakuna aliyejali, wakiamini kuwa kuna msukumo kutoka kwa Generali Franco, hata hivyo matokeo hayo yalitambuliwa na FIFA pamoja na UEFA.

USAJILI WA ALFREDO DI STEFANO WAONGEZA UHASAMA

Ni kilomita arobaini tu mahali alipolala Generali Franco. Ni kwenye viunga vya makaburi maarufu ya jumuiya ya 'Nuestra Senora de la Almudena yaliyopo Madrid. Ndipo mwili wa mwanaume mwingine ulipolala. Mwanaume huyu aliyeitwa Alfredo Di Stefano katu hawezi kukwepa kuwepo kwa uhasama huu.

Ilikuwa mwaka 1950, klabu hizi mbili zilipomgombea kumsajili Di stefano kutoka klabu ya Deportivo los millonarios ya colombia. Inaelezwa kuwa klabu ya Barcelona ilikuwa ya kwanza kumsajili Di Stefano lakini Real madrid nao wakaingilia kati usajili huo na wakamsajili mchezaji huyo hali ambayo ikapelekea kujitokeza mgogoro ambao uliwalazimu FIFA kuingilia kati na iliamuliwa kwamba wote Barca na Madrid wammiliki kwa pamoja mchezaji huyo acheze misimu kadhaaa Real Madrid kisha acheze Barcelona.

Uamuzi huo ulimtia unyonge sana Rais wa Barcelona ambaye alilazimika kujiuzulu baada ya kutambua kulikuwa na nguvu fulani kutoka kwa watawala kuhusu shauri hilo akiamini hawakuitendea haki Barca. Kujiuzulu kwake kukapeleka kuundwa kwa bodi mpya ya Barcelona ambayo iliamua kufuta mkataba wa Di Stefano na Barcelona.

Di Stefano akabakia Madrid mahali ambako aliipa mataji matano ya Ulaya, na kilicho wauzi zaidi Barcelona katika mechi yake ya kwanza ya El Clasico, Di stefano alifunga magoli mawili katika ushindi wa goli tatu. Akabakia adui zaidi miongoni mwa mashabiki wa Barcelona.Uhasama zaidi ukashamiri!!

ntaniy97@gmail.com
 
mech ya jmos naisubir kwa hamu sana yaan
 
Siongezi wala sipunguzi ni kweli tulifungwa kwa hujuma ila hata wao walishakula kichapo cha haja

#1926 (spanish cup)
Real Madrid 1-15 BARCELONA
#1955 (friendly match)
BARCELONA 16-0 Real Madrid
 
Lingine la ziada Mourinho ukaribisho wake alikula 5 akaja Ancelot akala 4 akafatia Benitez akapatiwa dozi ya 4 :0
Maoni yangu kwa heshima ya Zizu naomba yy apewe dozi ya paracetamol yani kutwa mara 3 huku MSN WAKIWAJIBIKA
 
Kwa sasa Real Madrid watasubiri sana. Barcelona ni timu ya dunia. Namwonea sana huruma zizzou kwa kipigo atakachopata pale nou camp.
 
Siku hizi hakuna El clasico ya maana, Madrid siku hiz imekuwa kama simba ya tz, kwa Madrid hii sitegemei hata sare japokuwa Naichukia sana Barcelona.
Ila hii Madrid siwezi kuiwekea dhamana
 
#salute kwako Nihzrath for good & attractive history# ila elclassico ya siku hizi haija balance upande mmoja mzito(barca).
 
bahati mbaya huwa sibet... ila Jmosi Barca lazima wachezee kichapo cha mbwa mwizi,
Pole, hicho kipigo mtakachopata kesho cha Ulimboka kina afadhali. Mashabiki wa madrid siwaonei huruma ila kocha wao ndio namsikitikia kwa fedheha anayokwenda kupata. Mnapigwa c chini ya ngozi 3.
 
Hii Madrid ya siku hizi hata kutoa sare na Barca wala hawawezi, Mimi naipenda Madrid lakin kwa Madrid ile hata kwenda kucheck game yenyewe napatwa na mchecheto.
Kuna wachezaji ambao hawana hadhi ya kuchezea Madrid.
 
Hata chadema mlisema itatoa rais kwa kuangalia mafuriko kwenye kampeni zao.sio kila siku ni ijumaa.leister city nani alitegemea ingekuwa hapo msimu huu
 
Pole, hicho kipigo mtakachopata kesho cha Ulimboka kina afadhali. Mashabiki wa madrid siwaonei huruma ila kocha wao ndio namsikitikia kwa fedheha anayokwenda kupata. Mnapigwa c chini ya ngozi 3.
kesho sio mbali mkuu.... mechi ikiisha tu nitakuja kwenye huu uzi usikimbie
 
Bahati mbaya huwa sibet... ila Jmosi Barca lazima wachezee kichapo cha mbwa mwizi.

Ni vzr kuota inakupa matumain
 
KUELEKEA "EL CLASICO" WEEKENDI HII.

UPINZANI WAO ULIANZIA HAPA

Ni katika ardhi iliyopo Manispaa ya San Lorenzo. Mahali ilipo hifadhi ya 'Siera de Guadarrama' ni hifadhi iliyozungukwa na vilima vingi, na miamba yenye kuvutia, ndipo mahali lilipo Kanisa la 'Valle de los Caidos'. Ni kilomita chache na ulipo mji mkuu wa Madrid. Mahali hapo ndipo ulipolala mwili wa mwanaume mmoja maarufu sana aliyeitwa Francisco Paulino Hermenegildo Teodulo Franco Bahamonde, na jina lake maarufu sana aliitwa Generali Franco, ama "El Caudilo" kama wahispania walivyopenda kumuita yaani 'Kiongozi'.

General huyu aliyezaliwa mwaka 1892 na kufariki mwaka 1975 mjini Madrid. Aliongoza nchi ya Hispania kutoka mwaka 1939 baada ya kumalizika vita vya wenyewe kwa wenyewe hadi mwaka 1975 alipofariki.

Ni mwanaume huyu ndie aliyekuja kuwa chanzo cha kuzaliwa "El Clasico" na kuongeza upinzani wa mechi kati ya Real madrid na Barcelona, kabla yake hakukuwapo na upinzani baina ya timu hizo kama ulivyo sasa. Pamoja na kuwa kiongozi wa nchi ya Hispania Generali Franco hakuficha mapenzi yake kwa Real Madrid, na aliipa kipaumbele Real Madrid kuliko timu nyingine.

Ni upendeleo huo wa watawala kwa Real madrid ulianza kuchukiwa na baadhi ya vilabu vingi ikiwemo Barcelona. Kuimarishwa kwa huduma za kijamii katika mji wa Madrid mahali ilipo timu ya Real Madrid na kutopewa kipaumbele kwa wananchi wa jimbo la Catalunya katika huduma za kijamii, kulipelekea kuhamsha chuki za wakazi wa jimbo la Catalunya dhidi ya timu ya Real Madrid na utawala mzima wa Franco.

Mechi hiyo ikaanza kuchukuliwa kwa mtazamo wa kisiasa. Real Madrid ikatazamwa kama inawakilisha utaifa wa Hispania na Barcelona ikatazamwa kama anayewakilisha utaifa wa Catalani, ndipo chuki zikaanzia hapo. Ni tarehe 13,juni 1943 ndipo hasa uhasama ukazaliwa baada ya Barcelona kupigwa goli 11-1, kipigo kilichobakia kuwa rekodi mpaka hivi leo. Ilikuwa katika nusu fainal ya Kombe la 'Copa de Generalismo" sasa inajulikana kwa jina la Copa de ley.

Kuna maelezo kuwa kabla ya mechi hiyo wachezaji wa Barcelona walitishwa na polisi wa nchi hiyo, na ilifikia Mwenyekiti wa Barcelona kipindi hicho Enric Pineyro kushambuliwa na mashabiki wa Madrid. Viongozi wa Barcelona walilalamikia hatua hiyo lakini hakuna aliyejali, wakiamini kuwa kuna msukumo kutoka kwa Generali Franco, hata hivyo matokeo hayo yalitambuliwa na FIFA pamoja na UEFA.

USAJILI WA ALFREDO DI STEFANO WAONGEZA UHASAMA

Ni kilomita arobaini tu mahali alipolala Generali Franco. Ni kwenye viunga vya makaburi maarufu ya jumuiya ya 'Nuestra Senora de la Almudena yaliyopo Madrid. Ndipo mwili wa mwanaume mwingine ulipolala. Mwanaume huyu aliyeitwa Alfredo Di Stefano katu hawezi kukwepa kuwepo kwa uhasama huu.

Ilikuwa mwaka 1950, klabu hizi mbili zilipomgombea kumsajili Di stefano kutoka klabu ya Deportivo los millonarios ya colombia. Inaelezwa kuwa klabu ya Barcelona ilikuwa ya kwanza kumsajili Di Stefano lakini Real madrid nao wakaingilia kati usajili huo na wakamsajili mchezaji huyo hali ambayo ikapelekea kujitokeza mgogoro ambao uliwalazimu FIFA kuingilia kati na iliamuliwa kwamba wote Barca na Madrid wammiliki kwa pamoja mchezaji huyo acheze misimu kadhaaa Real Madrid kisha acheze Barcelona.

Uamuzi huo ulimtia unyonge sana Rais wa Barcelona ambaye alilazimika kujiuzulu baada ya kutambua kulikuwa na nguvu fulani kutoka kwa watawala kuhusu shauri hilo akiamini hawakuitendea haki Barca. Kujiuzulu kwake kukapeleka kuundwa kwa bodi mpya ya Barcelona ambayo iliamua kufuta mkataba wa Di Stefano na Barcelona.

Di Stefano akabakia Madrid mahali ambako aliipa mataji matano ya Ulaya, na kilicho wauzi zaidi Barcelona katika mechi yake ya kwanza ya El Clasico, Di stefano alifunga magoli mawili katika ushindi wa goli tatu. Akabakia adui zaidi miongoni mwa mashabiki wa Barcelona.Uhasama zaidi ukashamiri!!

ntaniy97@gmail.com
@Nihzrat natakiwa nifanyaje ili na mimi niweze kuanza kutoa mada humu JF? Please assist.
 
Back
Top Bottom