Changia mawazo tuisaidiye serikali ya Tanzania.

Juaangavu

JF-Expert Member
Nov 3, 2009
935
132
Ndugu wana JF tuisaidiye serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mawazo ili iweze kuboresha huduma kwa raia. Kwa kuanzia mi ninayo yafuatayo, hivyo ninaomba kuwakirisha:

  1. Barabara ya Morogoro (Morogoro road) – Barabara hili ni kiungo muhimu sana cha uchumi wa taifa hili, ikitiliwa maanani kuwa reli ya mizigo haifanyi kazi. Ili hali shughuli za mradi wa mabasi yaendayo kasi ukiendelea, ninapendekeza waziri husika (Mwakyembe/Magufuli) aongee na mkandarasi wa huo mradi ili aweze kufanya kazi usiku na mchana. Ili mradi uweze kukamilika mapema na kupunguza kero ya foleni ikiwemo kuchelewa kwa mizigo inayoingia ndani ya jiji (uenda toka nchi nyingine tunazopakana nazo au mikoani) au toka ndani ya jiji. Waziri pia aamuru TANROAD kuondoa matuta yaliyo kwenye ‘service road’ kuanzia Ubungo TANESCO mpaka Kimara kwa kuwa hizo service road ndo hivi sasa zinatumika kwa ajili ya magari kupita.
  2. Reli ya mizigo – serikali tafadhali punguza matumizi, kopa na uweze kuboresha miundo mbinu ya reli ya TRC, mtupunguziye wingi wa maroli barabarani. Ni imani yangu kuwa wing wa maroli kwa kiasi ni chanzo cha uharibikaji wa barabara, chanzo cha ajali barabani na pia foleni kwa kiasi chake. Najuwa wenye malori hawatafurahi kuona, lakini chonde –turejeshe reli ya mizigo isaidiye kuboresha usafirishaji wa mizigo itokayo na kuingia ktk jiji na nchi yetu kwa ujumla;
  3. Uharibikaji wa magari barabarani – ninakumbuka Magufuli aliwahi kudai kuwa magari yote yaliyoegeshwa/kutelekezwa kwenye ifadhi za barabara yanavunja sheria ya nchi, na faini yake ni Sh 1,000,000. Mi ninapendekeza magari yote yanayoharibikia barabarani yaondolewe mara moja, ili lwaweza tekelezwa kwa kuwa na sheria au sheria ndogo ndogo ambapo askari wa barabarani kwa kushirikiana na halmashauri za sehemu husika watahita ‘breakdown’ mara moja kuondoa gari husika, na mmiliki wa gari atatakiwa kulipa gharama za kuondoa gari kwa mwenye breakdown na kiasi kupelekwa halmashauri kwa ajili ya shughuli za kimaendeleo-sema kutengeneza madawati ya shule nk. Faini ya Shs 200,000 yaweza wekwa kwa ajili ya shughuli hiyo. Kuliko hali ilivyo hivi sasa unapoweza kukuta lori limeharibikia katikati ya barabara, linaachwa hapo kwa wiki nzima au linatengenezewa hapo mpaka ikamilike
  4. Maamuzi ndani ya bunge letu –katika wakati huu wa teknohama, bunge letu limeendelea kupitisha maamuzi kwa mfumo wa kizamani kabisa – waliosema Ndiyo wameshinda! Ingelipendeza kama maamuzi ya bunge yatapitishwa tu pale wabunge wapatao 75% ya wabunge wote wapo bungeni (hii itaboresha maamuzi na uwakilishi wa wananchi bungeni); na maamuzi yapitishwe tu pale zaidi ya theluthi mbili ya wabunge watakapokuwa wameunga au kuikataa hoja husika. Kwa kuwa kila kiti cha mbunge kina kinasauti, viboreshwe kuwekea ‘voting burton – No, Yes or Neutral’. Kumbukeni – bajeti ya Wizara ya Ushirikiano wa Afrika mashariki ya mwaka wa 2012/13 ilisomwa mbele ya wabunge wasiozidi 36; na upitishaji wa bajeti ya Wizara ya Mambo ya ndani ilikuwa na wabunge wasiyozidi 100; kati ya wabunge 352. Jikumbushe kwa kusoma hapa: Wabunge watelekeza bajeti ya Afrika Mashariki
  5. Askari barabarani- niwapongezi kwa kazi wanayoifanya kwa kuwa barabarani kwa muda mrefu sana. Maeneo yafuatayo yanahitaji kufanyiwa marekebisho; pale inapotokea dereva wa gari la umma amevunja sheria – askari wa barabarani amchukuliye/amwadhibi kama wanavyofanya kwa madereva wa magari mengine. Imekuwa kana kwamba hawa madereva wa haya magari ya umma wanasheria ya kwao au ni ma-boss kwa hawa askari. Pili, kuna askari wanasimama eneo la Kona – majira ya asubuhi ambapo wanakuwa wanazuia au kukamata magari yanayoingia ndani ya jiji kutokea Kimara pindi wanapopita kwenye service road. Kwa kuwa magari mengi asubuhi yanatoka nje ya mji na kuingia ndani ya jiji, wale askari kazi yao iwe ni kusaidia ili watu wawahi kufika maofisini na kuanza uzalishaji kuliko kuanza kuzuia. Mi ninapendekeza waongoze magari kutimia service road na main road ili watu wawahi kwenye uzalishaji, na wale wanaotoka ndani ya jiji kwenda mikoani, kwa kuwa magari yanakuwa siyo mengi majira ya asubuhi waendelee kutumia barabara ya kushoto yaani wasitanue kwenda upande wa kulia wafikapo pale kona.

Nimeaanza na hayo, karibuni wadau mchangiye tuisadiye hii serikali yetu kwa mawazo. Mjenga nchi ni mwananchi.
 
Back
Top Bottom