Kama sikosei mwanzoni mwa January mwaka huu nilitoa tangazo hapa kuhusu mafunzo ya maarifa ya kazi ... sijaona mtu ametuma e-mail kwa ajili ya application.
Sasa naweka mambo wazi hapa. ...
Mafunzo hayo ni kwa ajili ya kuotesha chakula cha mifugo aina zote kwa siku nne - nane tu.
Kwa kufanya hivyo tutakuwa tumeondoa changamoto zifuatazo:
1 Ufugaji utakuwa na tija kubwa sana.
2 Migogoro kati ya wafugaji na wakulima itaisha kabisa
3. Mazao ya mifugo yatakuwa bora kwa sababu mifugo itakuwa ikitumia chakula bora .
... na mengineyo mengi.
Wewe unayesoma hii habari, nakusihi uwajulishe na wengine ili tuweze kupiga hatua kwenye sekta ya kilimo na ufugaji.
Mahitaji ili ufanye kazi hiyo ni kama ifuatavyo: -
1. Uwe na elimu ya kuanzia Std 7 na kuendelea.
2. Uwe unafundishika
3. Uwe na mtaji usiopungua 200,000/= (Hii ni kwa ajili ya kununulia vitendea kazi vya msingi)
4. Uwe tayari kununua kitini kwa ajili ya maelekezo. Tshs. 15,000/=
Maelekezo mengine utayapata pale ukishajiunga na wazalishaji wa H-Fodder
J & B Enterprises tumeumia sana kusikia mifugo inakufa kwa sababu ya kukosa chakula.
Wasiliana nasi kwa e-mail:
jnb14enterprises@gmail.com, simu 0655-533543.
Kwa walioko Mwanza karibu shamba darasa lililoko Igoma (nyuma ya St Mary's School)
TUIPENDE MIFUGO ITUPATIE CHAKULA BORA.