Uchaguzi 2020 Changanua kwa kina yaliyotokea kabla ya kupiga kura

DaudiAiko

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
302
274
Wana bodi,

Kwanza kabisa ninapenda kuwatakia wagombea wote wa Udiwani, Ubunge na Urais kila la heri kwenye uchaguzi utakao fanyika tarehe 28 mwezi wa 10 mwaka huu.

Ila katika kampeni ni vyema kama kwa Watanzania tujaribu kuchanganua kwa undani yaliyotekelezwa na serikali kabla ya kuwa "critical" sana. Nina imani sana kwamba wengi wana mengi ya kuchangia na mengi sana ya kukosoa na ndio maana serikali inaweka sehemu kama hizi ili Watanzania wote wahusike kwa njia moja au nyingine kwenye uendeshaji wa nchi yao. Sana sana kabla ya ku kosoa, jiulize kama una mawazo mazuri zaidi kuliko yale yanayo tekelezwa na serikali kabla ya ku kosoa sana

Ninapo ona kinacho elezwa kuhusu mafanikio ya serikali ya awamu ya tano: ufufuaji wa shirika la ndege la taifa, fly over Dar Es Salaam, ujenzi wa barabara nyingi, ujenzi wa vituo vya afya na mengineyo. Ina eleweka kwamba kuna malalamiko mengi kuhusu yalio fanyika kushindwa kuwa kugusa Watanzania walio wengi. Ila kitu ambacho kitawa shangaza wengi ni jinsi gani serikali inaweza kufanya mengi yalio enje ya uwezo wake.

Tutatalamika sana kuhusu fedha za walipa kodi ila tukijaribu kufanya tathmini ya mambo yote ambayo serikali imefanya, utagundua kwamba fedha za walipa kodi hazi fikii idadi ya fedha ambayo serikali inatumia katika shughuli za maendeleo zinazo fanyika au zilizo fanyika katika kipindi cha serikali ya awamu ya tano.

Tafakari,

Jumanne njema kwa wote
 
Back
Top Bottom