Changamoto za Uchaguzi mdogo ujao kwa CDM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Changamoto za Uchaguzi mdogo ujao kwa CDM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by luvcyna, Jan 21, 2012.

 1. luvcyna

  luvcyna JF-Expert Member

  #1
  Jan 21, 2012
  Joined: Feb 24, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 1,035
  Trophy Points: 280
  Kwa wapenzi wa CDM...
  Nimeona ni vyema tukilijadili hili la changamoto zilizopo ili ikiwezekana zifanyiwe kazi mapema kabla ya kuingia ulingoni

  Katika uchaguzi mgumu wa majimbo huu utakuwa mmoja wapo kwa sababu zifuatazo;
  1. Jimbo la Arumeru Mashariki Laweza kuwa ngome kubwa kwa mtu kama Lowassa kwa sababu kuu moja tu, Hili ndilo jimbo alikozaliwa Lowassa, hii ni sawa na kufananisha JK na Bagamoyo. Kwa ufupi tu Lowassa ni mzaliwa wa kijiji cha Ambureni wilayani Arumeru na ndiko alikokulia mpaka ulipotokea ugomvi wa koo maeneo hayo na yeye akiwa na baadhi ya wazee kuamua kujitenga na kuamia umasaini monduli. Kwa mantiki hii basi ni wazi akatumia historia ku win attention ya wananchi wa pande zile dhidi yake kwa kujiweka karibu nao tena kama ndugu yao..,ikumbukwe kipindi cha cha kuelekea uchaguzi mkuu 2010 Lowassa alikuwa akijisogeza sana kwa wakazi wa kule ikiwa ni pamoja na kuhudhuria misiba mingi iliyokuwa ikijitokeza na kwa haraka unaweza kuona ndio mbinu aliyoitumia kumpigia kampeni marehemu Sumari hadi kupelekea ushindi, bila shaka ataendelea kutumia mbinu hii na hili ndilo laweza kuwa CHANGAMOTO kubwa mno kwa CDM kushinda katika uchaguzi huo.
  2. Ni wakati muhimu kwa CDM kupima uwezo wake kushinda uchaguzi mkuu 2015 endapo Lowassa ataamua kuwa mgombea wa kiti cha Uraisi sambamba na Dr. Slaa. Hlii litajidhihiisha pale ambapo Lowassa atatumika kuipigia CCM kampeni na Dr. Slaa atakapotumika kuipigia CDM kampeni.

   Huu utakuwa ni mzani tosha wa nguvu ya kisiasa kati ya Lowassa na Dr. Slaa.
  Kwa wapenzi wa CCM pia mnakaribishwa kwani kejeli zenu ni sehemu ya changamoto kwa CDM
  Kaaribuni
   
 2. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #2
  Jan 21, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Gud idea! But ungesubiri kdogo basi hata marehemu azikwe kwani chama chetu CDM tunajali thamani ya utu wa mwanadamu, so z nt gud 4 ds moment kuzungumzia mambo ya east arumeru" ni mtazamo wangu 2 kamanda. BRAVO CHADEMA.
   
 3. luvcyna

  luvcyna JF-Expert Member

  #3
  Jan 21, 2012
  Joined: Feb 24, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 1,035
  Trophy Points: 280
  Copy that kamanda
   
Loading...