Changamoto za ndoa .

Wewe ndo unasababisha anywe hivyo vitoko..... Unaongea sana wewe mwanamke. Inaonekana una mdomo mrefu sana bwege wewe!!!
 
nadhani kama mlishawekeana hayo makubaliano basi hakuna ndoa tena hapo we sepa. ungekuwa hamjafanya hivyo ningekushauri utafute namna myamalize ila ndo hivyo.

pole sana bi dada...
 
MBITIYAZA ila si wakorofi
eti mapaja kama yako nimechekaaa nikaona nije kuchekeea huku tu
 
Ukitamka nimekuacha kwa talaka 3 hizo ni talaka tosha kiislam kwa Mimi nijuavyo
 
H
hapana nashukuru sana nimekueleWa
Wewe ndo unasababisha anywe hivyo vitoko..... Unaongea sana wewe mwanamke. Inaonekana una mdomo mrefu sana bwege wewe!!!
Ahsante
 
Hapo hamna ndoa.. Talaka ameshatoa tayari. Kama ni tatu au ni moja, soma hapa chini...

Wanazuoni wa Kiislamu wametofautiana kama talaka tatu mara moja zinahesabiwa kuwa ni tatu au ni moja. Hii ni kwa sababu kila kundi limetoa ushahidi kwa rai zao. Lakini kauli yenye nguvu zaidi ni kuwa mume anayetoa talaka tatu kwa mara moja inahesabiwa kuwa ni talaka moja lakini atakuwa amefanya makosa na madhambi katika tendo lake hilo na inabidi aombe msamaha.

Wakati mmoja Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alipashwa habari ya kuwa kuna mtu aliyetowa talaka tatu kwa mara moja. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alikasirika sana na kishaa akasema: “Mnachezea Kitabu cha Allah, nami bado nipo baina yenu”(An-Nasai, na akasema Ibn Kathiir kuwa Isnadi yake ni Nzuri).

Na alikuwa ‘Umar (Radhiya Allaahu 'anhu) akiletewa mtu ambaye ametoa talaka tatu kwa mara moja akimpiga viboko (Ibn Abi Shaybah).

Na katika mas-ala haya Allah ametuambia: “T'alaka ni mara mbili” (2: 229).

Hii inamaanisha moja baada ya nyingine na wala siyo kuzitoa kwa wakati mmoja. Sayyid Sabiq katika Fiqhis Sunnah anasema kuwa hii ndiyo iliyokuwa njia iliyofuatwa wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), Abubakr, ‘Umar na Makhalifa wengine (Radhiya Allaahu 'anhum) kabla kubadilishwa.
 
Ahsante sana ujumbe muhimu sana huu ahsante mkuu
 
Jaribu kumuelewa huyo dada.... Stroke ni ugonjwa tu unaweza kuvumilia sana.... Lakini ulevi wa kupitiliza unaokupelekea kujitapikia, kufanya fujo yan ni ulevi uliobeba kudhalilishana na sio kwamba hajaongea nae ameshaongea nae mpk vikao lkn anahaidi ataacha bila kutekeleza ahadi ya kuacha hivyo ni shida.. ... Nilichotaka kusema kwa ugonjwa unaweza mvumilia lkn sio kwa starehe ya karaha ambayo akihamua anaweza acha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…