Changamoto za Kunywa Vilevi Mitandaoni: Hatari ya Tonie Professor

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,132
Reaction score
10,514
Mitandao ya kijamii imekuwa sehemu ya maisha ya kila siku kwa vijana wengi, lakini pia imegeuka kuwa uwanja wa changamoto zisizo na maana wala faida yoyote kwa jamii.
images (56).jpeg

Hivi karibuni, kijana anayejulikana kwa jina la Tonie Professor ameibua mjadala baada ya kuanza kurekodi na kusambaza video akinywa vilevi vikali kama Konyagi na vinywaji vingine kwa wingi, huku akifanya hivyo kama sehemu ya “challenge” kwa mashabiki wake katika mitandao ya TikTok na Instagram.
images (55).jpeg

Mashabiki wake, kwa kutaka kuona zaidi, humtupia maoni yenye kumshawishi kunywa pombe zaidi na zaidi. Hali hii imeanza kuigwa na vijana wengine ambao wanataka kuonekana mashujaa wa ulevi, jambo linaloongeza hofu kubwa katika jamii.
1756749152770.jpg

Wataalamu wa afya wamekuwa wakionya mara kwa mara juu ya athari za kunywa vilevi kwa kiwango kikubwa, zikihusisha uharibifu wa ini, figo, moyo na hata kuathiri mfumo wa fahamu. Lakini hatari kubwa zaidi sasa ni kitendo cha vijana kushindana kwa kigezo cha nani anaweza kunywa zaidi bila kupoteza fahamu.

Je, mamlaka na wizara husika hazioni? Je, ni mpaka pale ambapo tutaamka na taarifa za vifo vya vijana kutokana na changamoto hizi ndipo hatua zichukuliwe?
1756749160417.jpg

Mitandao inaweza kutumika kuelimisha na kujenga, lakini kwa sasa imekuwa jukwaa la hatari linalowachochea vijana kushindana katika ulevi. Ni wakati wa mamlaka, wazazi na jamii kwa ujumla kuchukua hatua madhubuti ili kunusuru mustakabali wa vijana wetu.

NIKIUMWA SINA HELA MPAKA NYUMBANI
 
Huyo ni mtu mzima , maamuzi ni yake na pesa ya kununua vilevi ni yake ,hivyo sioni sababu ya kuingilia maamuzi yake , kama ni kufa wafe tu , wauza majeneza na urembo wa misibani nao wapeleke watoto shule.
 
Kuna watu wengi wanakunywa kumzidi huyo dogo.

Isipokuwa alichofanya huyo Dogo amefanya monetization (Ulevi) wake au kunywa kwakwe sasa amekuwa MTU wa tungi na content creators.

So atakuwa Ana earn kwa content huku anafurahia maisha.

Kuhusu watu kunywa pombe Kali , ni Serikali yenyewe kujua ni kiwango gan cha Alcohol power kinafaa kuuzwa.
 
Huyu azuiwe. Ni kama mtu anayejinyonga au anayekunywa sumu kisha akajirusha mtandaoni
 
Nakubaliana kabsa kuwa sikupaswa kulileta hili jambo.
 
Iga ufe...

Sidhani kama Kuna uhalisia kwa anachokifanya. Tayari tungeshapata majibu.
 
Mitandao ya kijamii imekuwa sehemu ya maisha ya kila siku kwa vijana wengi, lakini pia imegeuka kuwa uwanja wa changamoto zisizo na maana wala faida yoyote kwa jamii.
View attachment 3461694
Hivi karibuni, kijana anayejulikana kwa jina la Tonie Professor ameibua mjadala baada ya kuanza kurekodi na kusambaza video akinywa vilevi vikali kama Konyagi na vinywaji vingine kwa wingi, huku akifanya hivyo kama sehemu ya “challenge” kwa mashabiki wake katika mitandao ya TikTok na Instagram.
View attachment 3461695
Mashabiki wake, kwa kutaka kuona zaidi, humtupia maoni yenye kumshawishi kunywa pombe zaidi na zaidi. Hali hii imeanza kuigwa na vijana wengine ambao wanataka kuonekana mashujaa wa ulevi, jambo linaloongeza hofu kubwa katika jamii.
View attachment 3461696
Wataalamu wa afya wamekuwa wakionya mara kwa mara juu ya athari za kunywa vilevi kwa kiwango kikubwa, zikihusisha uharibifu wa ini, figo, moyo na hata kuathiri mfumo wa fahamu. Lakini hatari kubwa zaidi sasa ni kitendo cha vijana kushindana kwa kigezo cha nani anaweza kunywa zaidi bila kupoteza fahamu.
View attachment 3461699
Je, mamlaka na wizara husika hazioni? Je, ni mpaka pale ambapo tutaamka na taarifa za vifo vya vijana kutokana na changamoto hizi ndipo hatua zichukuliwe?
View attachment 3461697
Mitandao inaweza kutumika kuelimisha na kujenga, lakini kwa sasa imekuwa jukwaa la hatari linalowachochea vijana kushindana katika ulevi. Ni wakati wa mamlaka, wazazi na jamii kwa ujumla kuchukua hatua madhubuti ili kunusuru mustakabali wa vijana wetu.

NIKIUMWA SINA HELA MPAKA NYUMBANI
Mamlaka za Tanzania huwa wanasubiri majanga ndio waamke.

Unakumbuka ile ajali ya wanafunzi Arusha? Magari ya shule yalikaguliwa hadi funguo
 
Ni jambo la Muda.

Baada ya miaka 2 kuanzia sasa tutakuja na story yake na itakuwa ni fundisho kwa watu.

Pombe ni mbaya na kama unakunywa basi unywe kistaarabu.
 
Huyu janja anakunywa kwa challenge na request za watu
 
Back
Top Bottom