Changamoto za hisa mwenye kuzijua tafadhali

eden kimario

JF-Expert Member
Jun 13, 2015
10,235
16,205
Wana jf nimeamua kwa mara ya kwanza katika maisha yangu kua nataka kununua hisa za sehemu fulan sasa ninachoomba msaada kwenu ni kuhusu changamoto zake au hasara zake kuhusu faida nimezisikia nyingi ila nataka kujua hasara inakuja wakati gani maana najua hakuna biashara isio na hasara

Kiukweli nimeamua kununua hisa kwa mara ya kwanza na wapi pa kuanzia nimepewa kila kitu na nimeambiwa nakaribishwa ofisini muda wowote

Wana jf hasa wenye uelewa na hisa naomba msaada wenu

Nawasilisha asanteni nitashukuru kama mkinisaidia hili
 
Nadhani ungepata msaada mzuri kama ungesema umepanga kununua hisa toka kampuni ipi, inaonekana ushafanya chaguzi
 
Wanajf nataka kununua hisa DSE so nahitaji kujua changamoto zake ukiacha sifa na faida ninazozisikia nitafurahi mkinipa msaada kwa hili
 
Kwa tafsiri lahisi HISA ni kumiliki. Mtu akisema anamiliki Hisa basi huwa anamiliki kampuni ambayo amenunua hisa. Ile hela unayonunua hisa ni hela inayoenda kuchangia mtaji.

Katika kununua Hisa ni vizuri ukaangalia yafuatayo :
1. Menejimenti ya kampuni :- Kufanikiwa kwa kampuni yoyote sokoni ni matokeo ya menejimenti nzuri. Kampuni ambayo haina menejimenti nzuri ima itadumaa au thamani ya hisa zake itakuwa ya kusuasua sokoni. Mfano CRDB.
2.Taswira ya kampuni katika jamii (Goodwill). Kuna kampuni ambazo taswira yake katika jamii si nzuri hili husababisha ufanisi wake usiwe mzuri sokoni.
3.Mipango ya maendeleo ya Taifa. Ni vizuri ukitambua kampuni inaakisi vipi au inaingia vipi kwenye mipango ya Taifa. Serikali ni mmoja wa wateja wakubwa na kama kampuni unayoenda kununua hisa zake inajishughulisha na mambo ambayo ni kipaumbele cha serikali ni lahisi HISA za kampuni hiyo kupanda thamani.
4. Je, shughuli zinazofanywa na kampuni hiyo ni kwa kiasi gani zimelifikia soko? Katika kila watanzania 100 wenye uhitaji wa huduma za benki ni 20 tu waliofikiwa, kwa tafsiri hiyo soko la benki lina nakisi kubwa ya huduma. Mtu anunua hisa kwenye taasisi ya fedha ambayo ni makini uhakika wa kupata faida ni mkubwa.
5. Fuatilia vizuri umiliki wa soko wa kampuni husika na mikakati yake ya baadae. Mfano shirika la Bima la Taifa linamiliki soko kwa chini ya 10% kutoka kumiliki 100%. Kununua hisa kwenye kampuni ya aina hii kunahitaji kujua mipango na mikakati yao ya Muda wa kati na mrefu ili kujiridhisha.

Mengine nitaelezea baadae kwa kadri ya maswali yako.
 
kwa mbaali naanza kuelewa kuhusu HISA lakin sasa unafaidika je sasa wewe unaenunua kwa mfano mimi na HISA 10% CRDB hyo asilimia nazinunua kwa shiling ngap na nakuwa napata kiac gan per certain time
 
Ingia mtandaoni jielimishe mwenyewe kwanza ili hata mtu akileta uzoefu wake upate cha kulinganisha. Pia kuna hati fungani (treasury bills?) ambazo nadhani ni salama zaidi kuliko hisa. Ingia website ya BoT ujielimishe. NMB pia nimeona wanauza. Nenda huko DSE au kwa wakala yeyote ukiwa na mwanga kidogo. Hongera kwa kufikiria kuwekeza.
 
Nadhani ungepata msaada mzuri kama ungesema umepanga kununua hisa toka kampuni ipi, inaonekana ushafanya chaguzi
mkuu mimi nataka za nmb hizi walizotangaza juzi........faida na hasara zake pliz
maana sielewi chochote zaid ya kujua kuwa unakuwa mmiliki
 
Ingia mtandaoni jielimishe mwenyewe kwanza ili hata mtu akileta uzoefu wake upate cha kulinganisha. Pia kuna hati fungani (treasury bills?) ambazo nadhani ni salama zaidi kuliko hisa. Ingia website ya BoT ujielimishe. NMB pia nimeona wanauza. Nenda huko DSE au kwa wakala yeyote ukiwa na mwanga kidogo. Hongera kwa kufikiria kuwekeza.
mkuu nmb wanauza hati fungani laki5.........utofauti wa hisa na hati fungasni ni nini????????
 
wadau kuna tofauti gani kati ya hati fungani na hisa??????????
na je mfano wanauza hati fungani kwa 500000 huko nmb,.wanasema faida yake ni 13% hii ndo inakuAje????????????
tunaomba elimu wadau mupo kimya kweliiii
 
kwa mbaali naanza kuelewa kuhusu HISA lakin sasa unafaidika je sasa wewe unaenunua kwa mfano mimi na HISA 10% CRDB hyo asilimia nazinunua kwa shiling ngap na nakuwa napata kiac gan per certain time

Naomba nijibu kwa mfano. Benki ya CRDB inaweza kuwa na hisa milioni 2 ambazo zimeuzwa na kila hisa ina thamani ya Tsh 300. Ili umilikiki 10% ya hisa zake utachukua 10% ya 2 milioni ambayo ni hisa 200000. Utachukua Tsh 300 kwa kila hisa mara hisa 200000 na utapata Tsh 60 mil. Kwa maana hiyo unahitaji Tsh 60 mil kumiliki 10% ya hisa za CRDB.

Faida utakayopata
1. Gawio.
Hesabu za kufunga mwaka zikifanyika na CRDB ikapata faida. Mfano milioni 2,000/=. Kikao cha wanahisa hukaa kuamua faida itakayogawiwa kwa wana hisa iwe kiasi gani. Wakiamua milioni 1,000 zigawiwe, unachukua hiyo 1 bilioni unagawa kwa milioni 2 ambayo ni Tsh 500 kwa kila hisa. Kwa kuwa wewe una hisa 200,000 basi unachukua 200,000 mara 500 ambayo ni Tsh mil 100.

2. Thamani ya hisa kupanda.
Unaweza kununua hisa kwa Tsh 300 kampuni ikafanya vizuri sokoni baada ya Miaka 3 thamani ikawa Tsh 800. Kwa hiyo ukiziweka hisa zako sokoni unapata faida.

Dhamana.
Hisa hutumika kama dhamana ya mkopo katika baadhi ya taasisi za kifedha. Kwa maana hiyo badala ya kuweka nyumba au gari unaweka hisa zako
Tutaendelea kwa kadri ya maswali.
 
mkuu sasa nmb wanauza hati fungani kwa laki5.......na faida ni 13% inakuaje hii????????????
na je hati fungani na hisa zinautofauti gani???????????
naomba maarifa mkuu nataka kununua hati fungani kama zinalipa.........
 
Kwa tafsiri lahisi HISA ni kumiliki. Mtu akisema anamiliki Hisa basi huwa anamiliki kampuni ambayo amenunua hisa. Ile hela unayonunua hisa ni hela inayoenda kuchangia mtaji.

Katika kununua Hisa ni vizuri ukaangalia yafuatayo :
1. Menejimenti ya kampuni :- Kufanikiwa kwa kampuni yoyote sokoni ni matokeo ya menejimenti nzuri. Kampuni ambayo haina menejimenti nzuri ima itadumaa au thamani ya hisa zake itakuwa ya kusuasua sokoni. Mfano CRDB.
2.Taswira ya kampuni katika jamii (Goodwill). Kuna kampuni ambazo taswira yake katika jamii si nzuri hili husababisha ufanisi wake usiwe mzuri sokoni.
3.Mipango ya maendeleo ya Taifa. Ni vizuri ukitambua kampuni inaakisi vipi au inaingia vipi kwenye mipango ya Taifa. Serikali ni mmoja wa wateja wakubwa na kama kampuni unayoenda kununua hisa zake inajishughulisha na mambo ambayo ni kipaumbele cha serikali ni lahisi HISA za kampuni hiyo kupanda thamani.
4. Je, shughuli zinazofanywa na kampuni hiyo ni kwa kiasi gani zimelifikia soko? Katika kila watanzania 100 wenye uhitaji wa huduma za benki ni 20 tu waliofikiwa, kwa tafsiri hiyo soko la benki lina nakisi kubwa ya huduma. Mtu anunua hisa kwenye taasisi ya fedha ambayo ni makini uhakika wa kupata faida ni mkubwa.
5. Fuatilia vizuri umiliki wa soko wa kampuni husika na mikakati yake ya baadae. Mfano shirika la Bima la Taifa linamiliki soko kwa chini ya 10% kutoka kumiliki 100%. Kununua hisa kwenye kampuni ya aina hii kunahitaji kujua mipango na mikakati yao ya Muda wa kati na mrefu ili kujiridhisha.

Mengine nitaelezea baadae kwa kadri ya maswali yako.
Nimekuelewa vizuri mkuu nashukuru sana kwa msaada wako sasa sina budi kuifatilia hii ninayotaka kwenda kununua hisa
 
wadau kuna tofauti gani kati ya hati fungani na hisa??????????
na je mfano wanauza hati fungani kwa 500000 huko nmb,.wanasema faida yake ni 13% hii ndo inakuAje????????????
tunaomba elimu wadau mupo kimya kweliiii
Na mimi ndicho ninachosubiri kwenye gawiwo ni kila mwaka au inakuaje na hiyo faida ni sawa na shilingi ngapi
 
Naomba nijibu kwa mfano. Benki ya CRDB inaweza kuwa na hisa milioni 2 ambazo zimeuzwa na kila hisa ina thamani ya Tsh 300. Ili umilikiki 10% ya hisa zake utachukua 10% ya 2 milioni ambayo ni hisa 200000. Utachukua Tsh 300 kwa kila hisa mara hisa 200000 na utapata Tsh 60 mil. Kwa maana hiyo unahitaji Tsh 60 mil kumiliki 10% ya hisa za CRDB.

Faida utakayopata
1. Gawio.
Hesabu za kufunga mwaka zikifanyika na CRDB ikapata faida. Mfano milioni 2,000/=. Kikao cha wanahisa hukaa kuamua faida itakayogawiwa kwa wana hisa iwe kiasi gani. Wakiamua milioni 1,000 zigawiwe, unachukua hiyo 1 bilioni unagawa kwa milioni 2 ambayo ni Tsh 500 kwa kila hisa. Kwa kuwa wewe una hisa 200,000 basi unachukua 200,000 mara 500 ambayo ni Tsh mil 100.

2. Thamani ya hisa kupanda.
Unaweza kununua hisa kwa Tsh 300 kampuni ikafanya vizuri sokoni baada ya Miaka 3 thamani ikawa Tsh 800. Kwa hiyo ukiziweka hisa zako sokoni unapata faida.

Dhamana.
Hisa hutumika kama dhamana ya mkopo katika baadhi ya taasisi za kifedha. Kwa maana hiyo badala ya kuweka nyumba au gari unaweka hisa zako
Tutaendelea kwa kadri ya maswali.
Asante sana mkuu nazidi kufunguka kichwa kuhusu hisa
 
Back
Top Bottom