Changamoto za biashara nchini upande wa kodi / ushuru

Changamoto za biashara nchini upande wa kodi / ushuru

LumumbaCaptain

New Member
Joined
Oct 18, 2023
Posts
1
Reaction score
0
Vijana tukiwa takribani 40% ya idadi ya watu hapa nchini hivi sasa ...

Tumeambiwa tupo wengi tuliyohitimu level mbali mbali za elimu diploma, degree na Masters....(still jobless & moodless)

Tumeambiwa tujiajiri na tuwe wabunifu , tumejitajidi na tunaendelea kujitahidi ktk hilo ili kukimbizana na MUDA coz ndiyo umebeba NDOTO zetu , ili na sisi tuweze kufurahia MAISHA na RASILIMALI ZA NCHI YETU TANZANIA...

Sasa shida inaanzia hapa au iko hapa ?!🇹🇿😢

Kwa wanaofanya biashara watanielewa zaidi

  • Kodi ya TRA ni kubwa sana na Maafisa TRA sijui hawaridhiki n mishahara yao coz ukinunua hata kagari ,piki piki au kujenga nyumba badala ya wao wafurahie mteja wetu anastawi , wivu unaanza unakandamizwa vilivyo (kuna kuwa na kama ushindani flani) , wabadilike ktk hili coz tunafanya kazi kwa bidii ili tukue kiuchumi na kulinda future zetu ktk nyanja mbali mbali..
  • Halmashauri / Manispaa - Hawa nayo wanagandamiza sana mfano wilaya niliyopo haijafikia vigezo vya kutozwa 50k kwa mwezi ila sasa ni full kulazimishwa kama huwezi pisha jengo mwingine aingie ili nikawe mwizi au chokora na future ife (waache ubinafsi sisi ndiyo mabosi wao they have to listen us) ....
  • Bado kuna leseni hii siyo mbaya sana coz inatambulisha una idhini ya kufanya hiyo biashara yako husika ila isiwe kubwa sana coz 70% tunafanya biashara za kufanana so waratibu wa sheria twendeni taratibu ktk kukusanya kodi ili mtoaji awe n furaha n uzalendo n asonge mbele , watu wa uchumi wanasema "tafsiri ya unachokifanya inatakiwa iendane n muda" isije ikapita miaka 5 au 10 hakuna matokeo chanya hapo unapoteza muda ktk unachokifanya..
  • Service / Hotel /Gesti Levy / ada ya huduma - hii logic yake ni nini kama si wizi, kwani kodi ya halmashauri / manispaa si wangegawa % fulani iende huko mambo ya kuambia sijui unatakiwa uchangie % flani ndiyo upewe LESENI ni kuoneana tu na kupeana stress na vidonda tumbo ktk Motherland..😢🇹🇿
  • Ushuru wa Mazao - kuvusha gunia ktk mipaka waliyoweka ndani ya wilaya yako ni 1500 kwanini isiwe 500 coz wakulima ni wengi na wapo ktk mipaka ya Wilaya yao ktk kuinyanyua kimaendeleo, watu wanarisk kuingia ktk kujenga magodauni mashambani kuliko kwenye gunia zake 100 akatwe 1500 kila gunia ambapo ni sawa na 150k ilihali huyo mkulima wakusanya huo ushuru hawajui hizi mbilinge za baridi kali huko shambani, nyoka, tembo, wadudu waharibifu, kuibiwa na watu, gharama za kuendeshea...kwanini kwenye gunia 100 asitozwe sh 500 kila gunia na cost yake ikawa 50k
Wakati huo huo tunaambiwa taifa sijui lina uchumi wa kati na muda huo huo tena unasikia report ya waziri wa fedha deni la serikali ni T 107..

Na tunaambiwa hela inakopwa kwa ajili ya miundo mbinu ya nchi kama barabara, mawasiliano , afya , elimu n.k ila bado haina ufanisi huo ni almost 40% tu..

• Taifa letu kwa sasa linawasomi kede kede kila idara ila viongozi wa juu hawatusikilizi kwa uzuri wananchi wao sisi ndiyo watendaji wakuu tunajua real pinch waswahili wanasema utamu wa ngoma ingia ucheze..

• Nirudi kwenye suala la Afya nchi yetu kwa sasa ina madaktari lukuki na serikali imejitahidi kujenga / kuzikarabati hospitali za kiwilaya almost 80% , sasa swali ni je hayo majengo nani anaya operate kwanini daktari asomeshwe na kodi zetu mpk ana graduate then achague kufanya kazi kwenye majiji, miji mikubwa au makao makuu ya mkoa ili hali kodi ni mkusanyo wa nchi nzima ikiwa ndiyo tafsiri ya neno TRA (Mamlaka ya Mapato Tz) , watu wanateseka maradhi mbalimbali kama ya ngozi, macho, meno, sikio, uzazi, uvimbe, kisukari,presha n.k

Jambo lingine hapo hapo ktk ishu ya Afya ambapo ndiyo msingi wa utafutaji wetu coz wanasema MTAJI MKUU WA MWANADAMU YEYOTE NI AFYA BORA, turudi hapo hapo TRA & SERIKALI inakuaje Majengo ya vituo vya afya nchini, vifaa & madaktari, wauguzi na Manesi wanakuwa supported na kodi yetu then matibabu yanakuwa makubwa namna hiyo na ni hospitali za serikali (ambapo tafsiri yake ni wananchi) mfuko wa serikali ni mkubwa ukitumika vyema n ipasavyo matibabu yeyote yatakuwa chini sana (uzalendo n uwajibikaji uwe juu)

• Jambo lingine ktk safari ya maisha mchakamchaka ni endelevu na mrefu hadi kila mtu ahadi yake ya kupumzika itakavyofika , nikiwa na maana hapa duniani tunategemeana hakuna mjanja ktk hili 100% , kuna kadhia kama maradhi, misiba, majanga ya asili hapa tunawezaje kusaidiana ktk jamii n kodi utitiri hizo n usisahau taswira ya umaskini ya nchi yetu bado ndiyo kwanza tunasonga kuelekea kwenye mwanga twendeni taratibu n mikakati chanya ya uwajibikaji, uwazi n uzalendo , ripoti za CAG ziwe za kufurahisha si kuchefua nafsi zetu...hasara zinatokeaje kiurahisi hivyo na zimehusishwa document (tuzuie upigaji wa kodi zetu ktk tenda na mifumo ya serikali kama NEST)


Bado mambo ya harusi, kupongezana kupata mtoto ni sehemu ya matukio makubwa ya kijamii tutatoboa sisi vijana kuyaoperate coz tunawork harder ila vipato bado vinashindwa kukua ..

•Kuoa/ kuolewa imekuwa kikwazo kuanzia 2015 hadi sasa kutokana n ugumu wa maisha , uchumba sugu umekithiri katika jamii hata viongozi wa dini wanapigia kelele sana vijana wauage (USURIA) ila vijana mioyo yao inataka mwili unakataa aibu ya jamii kwa kushindwa kurun mahitaji muhimu ktk familia...

•Kingine ni watumishi waongeze mishahara n viongozi wa juu wapunguziwe mishahara tuache double standard na ubinafsi n viburi..

•Waliounda mfumo wa nchi iwe n Mahakama, Bunge n Serikali walikuwa magenius sana ila shida tunaoendeleza mfumo ndiyo tumekuwa na tabia ngumu (hatuwasikilizi tunaowaongoza hii ni mbaya)


• mifumo ya kiutawala inahitaji mabadiliko Bunge litoe amri wabunge wakae ktk majimbo yao na si ktk majiji au miji mikubwa n pia halmashauri zipewe nguvu ya kiutendaji ktk Wilaya zao kusubiri hazina kuu iliyoko dar n hii nchi ni kubwa na imegawanywa kimuundo wa kiuongozi ni kujichelewesha wenyewe , wafanye kazi report itumwe huko juu coz wao ndiyo wanaelewa wananchi wanadai nini na si watu walio dar tu

• Tunahitaji lami nchi nzima ktk wilaya zilizobakia na mawasiliano imara ya 5G kila Wilaya na gharama nafuu za mitandao ya simu..

• Jambo la kumalizia ni kwamba viongozi tunaomba mtusikilize hii nchi inataka reforms (mabadiliko) maeneo mengi tu na miaka 5 kiutendaji n mingi sana tukiacha wizi n ubinafsi tukafocus kiuzalendo Tz itakuwa better nation, na pia acheni kuzuia uhuru wa kujieleza na wa mitandao ya kijamii kama X na Telegram..

• Cha mwisho kabisa niwaombe Watz wenzangu kuzidi kusali na kuiombea nchi yetu hasa viongozi waache viburi, ubinafsi na pia kuziombea jamii zetu kuacha kuendekeza tabia za asili kama Wivu, Majivuno, chuki, Kiburi, Uchoyo, Hasira , Tamaa ...kwani zinaua sana ushirikiano ,mshikamano na Upendo ktk jamii au taifa....

Cha niongeza wazungu wanasema "Learning is a continous process" (Kujifunza ni mchakato endelevu).. Watz tupende kujifunza mambo ya Afya,siasa, tamaduni, teknolojia n.k kama tunavyopenda mpira na kuufwatilia ili kuongeza maarifa ili tuweze kujenga hoja na kukabiliana na kila changamoto kwenye jamii...HALAFU NA WEWE KARIA NA TEAM YAKO BLUNDER YAKO YA DERBY TUMEIONA UNAHITAJI REFORM UTATUULIA SOKA LETU..

Asanteni ni mtazamo tu wa maumivu ya kizalendo tunayoyapitia Raisi wetu S.S.H....🇹🇿❤️🙏
 
Back
Top Bottom