Matanga
JF-Expert Member
- Nov 13, 2019
- 2,281
- 3,988
Bwana mmoja hodari wa kushiriki katika shughuli za ukoo wake, ghafla paaaaaaaap akajitoa.
Baada ya wiki chache, usiku mmoja wa baridi kali sana, kiongozi wa kikundi hicho cha ukoo, alikwenda nyumbani kwa bwana huyo, kumtembelea.
Akamkuta yu mpweke anaota moto. Mwenyeji alimkaribisha mgeni wake, kisha kukapita kimya kirefu baina yao huku wakiiangalia miali ya moto ikipepea.
Baada ya dakika nyingine zaidi za ukimya, yule kiongozi alisogelea moto na kuchagua kipande kimoja cha gogo lililokuwa likiwaka sana na kulitoa kwa kutumia jaro na kuliweka kando na baadaye alirudi kuketi kwenye kiti chake, huku mwenyeji wake akiangalia kwa umakini mkubwa kila kitu kilichokuwa kikiendelea!
Haukupita muda mrefu, moto uliokuwa ukiwaka kwenye lile gogo lililowekwa pembeni, ukaanza kusinzia na hatimaye kuzimika.
Tangu kuingia kwa kiongozi yule nyumbani kwa mwenyeji wake, wawili hao walizungumza maneno machache sana. Kabla mgeni hajaondoka, alichukua jaro na kulirudisha lile gogo katikati ya moto na mara moja likashika moto kutokana na kuwa pamoja na magogo mengine yaliyokuwa yakiwaka.
Baadaye, ilifika muda wa mgeni kuondoka na alipoufikia mlango na kumuaga mwenyeji wake, yule bwana aliyejitenga na kikundi cha ukoo, akamshukuru sana mgeni wake kwa kumtembelea na pia kwa somo kubwa alilompa na akatoa kauli kwamba atarudi kundini haraka sana!
SWALI: NINI UMUHIMU WA KUNDI?
JIBU: KILA MWANAKIKUNDI ATAKAYEJITOA, HUONDOKA NA MOTO NA JOTO LAKE
Ni muhimu kuwakumbusha wanakikundi kwamba kila mmoja wao ni sehemu ya moto unaowaka, kwa hiyo tuna wajibu wa kuufanya moto wa kila mmoja wetu uwake. Ni lazima pia kuendeleza mshikamano wetu ili moto wetu uwe mkali na udumu muda mrefu zaidi.
KUNDI LETU HUGEUKA NA KUWA FAMILIA MOJA KUBWA AMBAMO KILA MWANAKIKUNDI HUPATA AMANI NA FURAHA, BILA KUJALI KWAMBA MUDA MWINGINE TUNAPATA KERO, KARAHA NA MISUKOSUKO MINGI.
*Muhimu zaidi ni kwamba tuwe pamoja. Sababu ya kuwa na kikundi ni kwamba tunakutana, tunajifunza, tunajiburudisha, tunataniana, tunabadilishana mawazo ama kule kutambua kwamba hatupo wapweke!*
*Hivyo basi kuna haja ya kuupepea moto wetu ili uendelee kuwaka kwa ukali zaidi, kwani MAISHA HUPENDEZA ZAIDI TUKIWA PAMOJA NA NDUGU NA MARAFIKI.*
Mchana mwema!!!