Changamoto kilimo cha umwagiliaji zawaibua NIRC

Changamoto kilimo cha umwagiliaji zawaibua NIRC

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,038
Kutokana na kuwepo kwa changamoto ya kilimo cha kubahatisha kwa wakulima kutokana na mvua zisizo za uhakika, serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) imeanza kuchimba visima virefu vya maji hamsini kwa ajili ya matumizi ya kawaida na viwili kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji mkoani Tabora ambapo mradi huo utatekelezwa kwa muda wa siku ishirini na moja.

Soma pia



Akizungumza Septemba 1,2025 wakati wa uzinduzi wa mradi huo katika Kata ya Migua, Wilaya ya Nzega, Mhandisi wa Umwagiliaji Mkoa wa Tabora, Martin Mgangaluma amesema kuwa uchimbaji wa visima ni mkakati wa kitaifa wa kuwaondolea wakulima changamoto ya kutegemea mvua zisizotabirika ili kuwawezesha kujikwamua kiuchumi kupitia kilimo.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Utafiti na Uendeshaji Teknolojia kutoka NIRC, Mhandisi Naomi Mcharo amesema tume hiyo imelenga kuchimba visima elfu sitini na saba nchini kote huku akiwataka wananchi kuvilinda vifaa vya uchimbaji vilivyopo kwenye maeneo yao ili zoezi hilo lifanikiwe kwa muda muafaka.

Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Bi. Winifrida Funto akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Nzega, amewataka wakulima kuunda na kusajili vyama vya wakulima wa umwagiliaji katika NIRC ili wapate usaidizi wa mafunzo ya kilimo.

Baadhi ya wakulima wamesema uwepo wa visima vya umwagiliaji katika maeneo hayo utawawezesha kuondokana na kilimo cha kubahatisha na kwamba itakuwa fursa kwao kufanya kilimo katika majira yote ya mwaka.
 
Back
Top Bottom