Umenikumbusha kuna kampuni ilinipigia simu niende singida interview nikakataa kwamba mbali, baada ya siku mbili wakapiga simu tena niende shinyanga nikafanye interview nimeenda eti wamekodi hotel yaani nianze kazi moja kwa moja nitalala hotelini baadaae nitatafuta nyumba....nikaulizia malipo, walipotaja tu nikawauliza mara ya pili wakataja na maneno mengi kweli.....hasira zikanipanda nikawaambia hata kazi ninayoifanya kwasasa hawalipi hivyo kwahiyo siwezi kupoteza muda....nikawaomba nauli nilizotumia kwenda then nikawaambia nitarudi baada ya wiki mbili nikachukue mizigo.....ikawa jumla. NIKAFIKIRIA INGEKUWA WANAANDIKA SALARY mtu wala huwezi kuhangaika kufanya applications kama unaona malipo hayafai, Kampuni za kijinga sana hapa Nchini, usione zipo nyingi hivi yaani nyingi ni za kishenzi sana!!!....Kusumbua watu tu, mm siku hizi naandikaga salary expectation kwenye CV na barua ili wakiona sio size yao wasinisumbue kuniita interview....USHENZI TUPU!