Changa la macho Magufuli kagoma kulipa mifuko ya jamii Tril 4, mafao shakani na mifuko kufa japo wameunganisha

Huu sasa ni utani..!! Trillion 4..! anajenga Reli ya SGR toka makotopora mpaka Tabora hiyo hela jamani..! Mifuko itakufa kama watendaji wataruhusu wawaingize wanasiasa ili wapige hela maana wanasiasa wana sura mbili kila sehemu wao wanataka kula
Pesa za mifuko ya pensheni zililiwa na viongozi na kuanzisha miradi isiyo na thamani halisi awamu zilizopita.Mweshimiwa Maghufuli kwa sasa kweli ana msalaba mzito maana ,pesa zimeliwa,miradi iliyoanzishwa karibuni yote ni hasara...Sio kama ataki,ni kuwa anatafuta mbadala ili pesa zipatikane wastaafu wasife njaa.Mweshimiwa rais anajitaidi sana ila ana watu wa kumsemea na kueleza hali halisi.Hii nchi imetafunwa sana.Na kuna madudu mengi kwa yeye anayeyajua kweli acha akose usingizi....manaana ajamaliza hili lingine lina jitokeza..Mungu amtie nguvu na hekima katika kuiongoza nchi hii
 
Kina Mtulia na waitara wanaunga mkono juhudi za mutukuf kuiba "hera" za "wararahoi"
Iko siku tutawakalisha kwenye ncha ya mshale
 
Na wewe umeelewa swali? Kumbuka nilitaka kujua imejadiliwa au bado

Kwani kwenye bunge mijadala inaanzia wapi? Mijadala inaanzia kwenye Kamati kabla haijapelekwa kwenye Bunge zima. Sasa hivi kamati za bunge ndio zinazokutana kabla ya kikao kamili cha Bunge. Sasa usiulize tena source ya taarifa husika!!
 
Huyu mzee wakati alipokutana na wadau kuzungumzia kikokotowo si alisema kuwa alipoingia madarakani alikuta madeni ya matrilioni kwenye mifuko ya Jamii na akazilipa na sasa zimebaki bilioni chache tu?

Sasa hii taarifa ya kuwa kuna deni la Trilion 4 imekaajekaaje? AU huyu mzee siku ile alitupiga kamba?
 
Msema kweli ni mpenzi wa Mungu..... Yaani serikali ilipe hela walizokula akina Dau na mwenzie Manji?!
kuna document iliwai kaa bungeni masaa tu,ikafutiliwa mbali...imejaa madudu ambayo ukiyasoma Dau anastaili kufungwa maisha yeye na washirika wake na kutaifishwa mpaka makobaz yake...sema tu aiwezekani kuiweka hapa ila kwakeli kwenye hili Baba Maghufuli tuna mlaumu bure
 
Pesa za mifuko ya pensheni zililiwa na viongozi na kuanzisha miradi isiyo na thamani halisi awamu zilizopita.Mweshimiwa Maghufuli kwa sasa kweli ana msalaba mzito maana ,pesa zimeliwa,miradi iliyoanzishwa karibuni yote ni hasara...Sio kama ataki,ni kuwa anatafuta mbadala ili pesa zipatikane wastaafu wasife njaa.Mweshimiwa rais anajitaidi sana ila ana watu wa kumsemea na kueleza hali halisi.Hii nchi imetafunwa sana.Na kuna madudu mengi kwa yeye anayeyajua kweli acha akose usingizi....manaana ajamaliza hili lingine lina jitokeza..Mungu amtie nguvu na hekima katika kuiongoza nchi hii

Haikosi hawa wapinzani ndio waliwekeza fedha za hii mifuko kwenye miradi mibovu!!

Sasa hivi chama tawala kinarekebisha mambo ili hii mifuko isichezewe tena na hawa wapinzani!!

Sijui naota!!

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Haikosi hawa wapinzani ndio waliwekeza fedha za hii mifuko kwenye miradi mibovu!!

Sasa hivi chama tawala kinarekebisha mambo ili hii mifuko isichezewe tena na hawa wapinzani!!

Sijui naota!!
Ukimaliza kuota kajiharishie na kakojoe kisha ukalale tena,ili uendelee kuota.angalia usikojoe kitandani

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ni hivi majuzi tu Jiwe alituaminisha kwamba kalipa deni la serikali kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii na imebaki only 200 bil ili kukamilisha malipo ya deni. Leo tunaambiwa kuna deni la 4 tril. Hivi huu uongo ni kwa manufaa ya nani na una muhimu gani katika uendeshaji wa nchi?
 
Kwani kwenye bunge mijadala inaanzia wapi? Mijadala inaanzia kwenye Kamati kabla haijapelekwa kwenye Bunge zima. Sasa hivi kamati za bunge ndio zinazokutana kabla ya kikao kamili cha Bunge. Sasa usiulize tena source ya taarifa husika!!
Kwaiyo mleta habari ni mwana kamati wa hizo kamati za bunge?

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
 
Msema kweli ni mpenzi wa Mungu..... Yaani serikali ilipe hela walizokula akina Dau na mwenzie Manji?!
Acha utani ndugu, hizo tr 4 hao unaowatuhumu wamezifanyia nini? Huwezi kutuhumu Manji na Dau bila kuihusisha CCM na Serikali yake. Dau ni balozi , Manji yuko humu nchini anakula maisha. Kwa nini usituambie zilitumika kuijenga UDom na nyinjgine CCM?

Vv

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali inadaiwa Trilioni 8 na si 4....Serikali iweke mkakati wa kulilipa hilo deni....wawe na target ya kulipa trilioni 1 kila mwaka!!
 
Huyu mzee wakati alipokutana na wadau kuzungumzia kikokotowo si alisema kuwa alipoingia madarakani alikuta madeni ya matrilioni kwenye mifuko ya Jamii na akazilipa na sasa zimebaki bilioni chache tu?

Sasa hii taarifa ya kuwa kuna deni la Trilion 4 imekaajekaaje? AU huyu mzee siku ile alitupiga kamba?
Ukitumia neno 'huyu Mzee' tayari unamkosea adabu Mtu yeyote wa rika lake.

Alicholipa Rais ni malimbikizo ya michango ya Wafanyakazi wa Serikali kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.

Kilicholetwa hapo ni madeni ambayo Serikali ilikopa kutoka mifuko ya hifadhi, na kwa hakika ameirithi!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwaiyo mleta habari ni mwana kamati wa hizo kamati za bunge?

Hili jibu langu ni kwa swali kama ripoti ya CAG ilikuwa tayari imejadiliwa bungeni; ukisoma vizuri hilo jibu utapata jibu lako wewe pia!
 
mifuko ikishindwa kulipa wastaafu nadhani wastaafuu tutagawana mafao ya Nduga..i.....jobu
 
Back
Top Bottom