Chaneli ya TVN kutokea Korea yaingia rasmi Afrika

Krikichino

JF-Expert Member
Oct 5, 2019
651
1,098
Habari zenu wakuu, kwa wale wapenzi wa korean dranas hii ni ya kwenu.

Channel ya TVN kutokea Korea Yaingia Rasmi Africa.

Wakorea ambao kwa muda mrefu sasa tumekuwa tukiangalia series zao na wao wameamua kuleta version ya Africa ya Channeli ya TVN.

Kama umeangalia series kama MR SUNSHINE, CRUSH LANDING ON YOU pamoja na GOBLIN ya mwaka 2016, TVN ndio channel iliyohusika kutengeneza au kuonesha series hizo.

Kampuni ya CJENM ambayo ndio inamiliki kituo cha TVN huko Korea kama ambavyo IPP inavyomiliki ITV imeingia makubaliano na DSTV kuruhusu channel hiyo iitwayo TVN AFRICA kuanza kurusha matangazo yake.

Channel hii ni namba 134 hapo DSTV itakuwa inapatikana kupitia package ya DSTV Compact, Compact + na DSTV Premium huku kwa South Africa imepata upendeleo maana itakuwa inapatikana pia kupitia DSTV Family.

UTOFAUTI NI NINI?

Well, TVN AFRICA haitakuwa sawa na ile original TVN ya Korea kwa maana ya kwamba hii ya Africa itakuwa na Subtitles za kiingereza lakini pia dramas zitakazokuwa zinaoneshwa huku Africa zitakuwa tofauti na Korea "meaning TVN Africa will have a customized feed special for Africa"

TVN ndio channel ya kwanza ya kikorea kuingia rasmi kwenye soko la Africa.

Ombi la waafrika wengi kwenye social media baada ya kusikia taarifa hizo ni kwamba TVN Africa isiwe inarudia rudia series za zamani kama ambavyo channel nyingine za kimataifa zinafanya.

Mfano Nickeledeon Africa mpaka leo bado inaonesha shows kama ICARLY ya 2007, GAME SHAKERS pamoja YA THE THUNDERMANS ya 2013 hizi ni shows ambazo hazipo on demand tena hivyo watu wanataka series mpya kwenye channel hiyo.

Pia suala la dubbing ni kitu ambacho watu walikuwa wanakiongelea kwenye social media hasa Facebook, huku wapenzi wa Korean Dramas wakisema kuwa hawataki waingiza sauti kwenye series ambazo zitaoneshwa kwenye chanel hiyo ya TVN Africa kwani inaondoa uhalisia wa series nzima.

KWANI TVN ILIANZIA WAPI?

Yes channel ya TVN ilianza mwaka 2006 huko Korea ikiwa chini ya kampuni ya CJENM kampuni inayoongoza kwa Kutengeneza filamu huko nchini Korea kusini.

Wajuzi wa mambo wanasema wakati TVN inaanza haikudhaniwa kuwa itakuja kuwa tishio kwani TV stations kama SBS, KBS pamoja MBC ndio zilizokuwa zinapata watazamaji na wadhamini wengi.

Lakini utofauti wa TVN na chaneli hizo tatu ni kuwa kama jina lake linavyojieleza Total Variety Network, TVN ilikuja kivingine kwani vipindi vyake havikuwa vinachagua rika. Ndani ya TVN kulikuwa na vipindi vya michezo, muziki, filamu, tamthiliya, habari na vinginevyo.

Ni kama tu ITV ambavyo ina THE BASE kwa ajili ya vijana, KIPIMA JOTO kwa ajili ya watu wazima na WATOTO WETU kwa ajili ya watoto. Hivyo TVN ilileta mapinduzi haswa kwenye kiwanda cha maudhui.

Kwa sasa kituo hiki kinachoongozwa na Rhee Myeong Han kina shows tofauti tofauti kama ON& OFF, HOME TOWN FLEX lakini vile vile kuanzia mwaka 2009 mpaka 2012 walipata nafasi ya kuonesha michuano ya UEFA na EUROPA pia inaendelea kuoneshwa.

Pia TVN inamiliki studio yake kwa ajili ya kutengeneza Korean dramas ijulikanayo kama Studio Dragon ambayo ukiangalia kwa umakini ni kama kampuni inayojitegemea.

Studio Dragon inahusika kutengeneza Series zote za TVN na hata nje ya TVN huku Netflix ikiwa ina 4% share katika kampuni hiyo na ndio maana hata series ya KINGDOM starring Ju Ji Hoon inayooneshwa na Netflix ilitengenezwa na Studio Dragon.

Swali kubwa watu wanalojiuliza ni je TVN Africa itaweza kuwa na influence kama ambayo MTV Base au Fox Africa iko nayo kwenye bara hili?

Chochote kinaweza kutokea kwa sasa tuendelea kurahani series na vipindi vizuri kutoka TVN Africa.

Uzi Tayari

tvn_centred.jpg
MrSunshine_Flag-Horizontal_PRE_EN-US-660x400.jpg
tvn_center.jpg
48b8f99dc0f04a7d912a25d21c5cc446.jpg
 
tunazipata vizuri tu.

kissiassian.sh

dramacool

dramanice.movie

toxicwap.com

bila masharti ya for or not for africa
Mkuu nadhani hii itawasaidia sana wale ambao hawawezi mambo ya kudownload kama watoto na wadada kazi
 
Mmmmmmhmn kuna vitu vya ajabu siku hizi. Sasa unakuta mtu kakaza macho anatazama drama za kikorea, si ni bora nitazame bongo movie?!
 
Back
Top Bottom