Chande: Hukumu ya Lema itahamishiwa Dar es Salaam

Huu ni ushahidi mwingine wa kuonyesha mahakama zetu ni ZERO!!!! Tukio litokee Arusha lakini kesi ikafanyike Dar!!! Ni majukumu gani hayo waliyokuwa nayo Dar ambayo hayawezekani kufanyika wakiwa Arusha!? Kuna mtandao, kuna simu, kuna usafiri wa uhakika kati ya Arusha na Dar na vice versa...sasa hebu wauambie umma wa Watanzania hayo majukumu ambayo hayawezekani kufanywa wakiwa Arusha.
 
Basi itabidi kesi zote za Mahakama ya Rufaa zifanyike Dar.

Hakuna siku kazi zitapungua, sanasana zitaongezeka zaidi kila siku
 
Ahaaaaaa!!! kwa maana hiyo kuanzia sasa kesi zote zilizoko mikoani zitakuwa zinahamishiwa Dar? Tanzania anything is possible!!
 
Ukiona ivyo Lema kashindwa ndo maana wameamua kuepusha shali kwa kuipeleka DSM
Mahakama kwa zama zetu ni muhimili unaojitegemea kweli?
 
sababu zilizotolewa zinajitosheleza na wala hazihitaji ufafanuzi zaidi
 
Unakosea sana ndugu, wale jamaa ninavyowajua watakuja hata huko Dar.
 
Hapo penye red. unachukua PhD!!,,,,, hiyo PhD inauzwa bei gani nami nikanunue? ,,,, Ican buy ten of them.
 
Umati wa CDM uliokuwepo pale mahakamani Arusha ulikuwa unatisha. Inawezekana wameamua kwenda Dar ili hata rufaa ya Lema ikishindwa kusiwe na hofu juu ya usalama wao.
 
Nadhani Dsm itakuwa nzuri maana itapunguza gharama , hawa jamaa wanakaa huko Arusha wanatumia pesa yetu walipa kodi. Bora wakae dsm wakati huo wawe wanafanya na majukumu mengine.
 
hata wakienda ughaibuni hukumu hiyo itatikisa arusha.kwa nini hatukubali kuwa A-town ni ngome ya CDM?Tukumbuke kuwa chanzo cha rufaa ya kesi hii ni kuepusha hukumu mbovu isitumike kama reference na sio kuanguka kwa CDM arusha.

.
Wacha mahakama ijinyonge yenyewe na kamba itakayotumiwa baadae na wezi wa haki wakimrifaa Chande. Aibu ya huu mhimili ni aibu ya taifa vizazi hata vizazi.
.
 

Mkuu hapo unaongelea Geographical jurisdiction. Nakumbuka kuisoma hii kwenye Business Law miaka hiyooo. Hapo ni kufunguiliwa sasa kuhusu suala la appeal sijui jurisdiction hiyo inasemaje.
 

Inabidi Mahakama Ipange siku ambayo Kesi Itasomwa bila Huo Muingiliano!! Any way Majaji wa Voda Fasta Tegemea Lolote!!
 
Mkuu TUMBIRI nadhani majaji wanakimbizana na muda,unajua hizi kesi za uchaguzi lazima ziamuliwe ndani ya muda uliokubaliwa kisheria sioni kama kuhamisha kesi Dar ni tatizo sana kinachoangaliwa ni haki kutendeka.

 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…