Nilikuwa sifahamu kuwa kumbe Colombia mziki wa Congo na nchi nyingine unapendwa sana na kisa hasa ni kuwa hawa jamaa na wao wana Soukous yao wanaiita Champeta. Mengi siandiki ila angalia mwenyewe/Sikiliza mwenyewe.
Bibie kama kawaida yake, huwa akifanya wimbo wa biashara kwa kuimba Kiingereza, huwa lazima awakumbuke na Amigo / Mariachi wake huko America ya Kusini. Hapa anakuja na wimbo wake huo huo ila kwa Ki-Spanish. Haya mapigo ya CHAMPETA hayo.....
Nimekuja tena. Katika pekua pekua nyimbo, nimekutana na wimbo wa Tabora Jazz wa dada Asha ukipigwa na Wa-COlumbia katika huo mtindo wa CHAMPETA. Kama huamini basi hebu sikiliza Dada ASHA ikitesa Columbia kwa Ki-SPANISH. Sijui hata wapigaji wa zamani wanafahamu kuwa huu wimbo wao umefika Columbia................