Chama unachoshabikia kinasema wewe nani

Chama unachoshabikia kinasema wewe nani

The only

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2011
Posts
11,088
Reaction score
14,576
Huu ni mtizamo wangu binafsi juu ya mtizamo unaopelekea vijana kujigawa vyama mbalimbali Tanzania, Kimsingi mimi naheshimu machaguo yote ila kwa utafiti wangu usio rasmi wa kuzungumza na vijana mbalimbali jambo moja in common niligundua vijana wanauzalendo na nchi yao na ambao siasa ni career yao wamejipanga kufikia makubwa kwenye tasnia hiyo ,Hivyo nitafupisha machaguo yao na sababu hasi na chanya zipelekeazo kuwa waliposimamia.

1.Walio vyama vidogo (CHAUSTA ,ACT,UDP, e.tc)
Chanya : Ni vijana wenye msimamo usio wa kuiga na wanaoteswa na siasa za umaarufu za ''wengi wakweli'' mara nyingi huwa wenye mafanikio hata maisha yao binafsi au wanatokea familia zenye asili hiyo

Hasi : ni vijana wenye low profile wasio na ushawishi wa kupenya kwenye vyama vikubwa hivyo kutafuta ''kiki'' huku ndo nia yao ,huwa wanamitizamo isiyotekelezeka na wengi wakosoaji wasio na mikakati ya utendaji .

2.CUF
Chanya : Ni vijana makini wengi walianza kuifuatilia siasa ya nchi zamani na huwa wanamsimamo wa maisha yenye maadili ya Kitanzania na kurudi kwenye nguzo zetu za ujamaa na kujitegemea zikijikita kwenye utu na kazi.

Hasi : Wengi ni waislamu wenye hulka na misimamo ya udini wakiificha kinafiki na kutoa vijisababu vya kuwa hiyo ni hujuma ,aidha wale wadini nyingine hupenyea japo wakijua kwenye unafki wa kubalansi udini watanufaika .Aidha kuna wale pia waliofata misimamo na mivuto thabiti ya lipumba na maalimu hawa ni bendera wataeamua yuko sahihi hufa naye.

3.CCM
Chanya : Ni vijana unaweza sema makini sana tena wazalendo kwa nchi yao ,Hutambua kama chama kimefanya makosa mengi mazito ya aibu ila hupambana wakijua njia pekee ya dhati kuokoa nchi ni kutumia CCM kwani kilishawahi ,hawa walishabikia sana sera za kujivua gamba wakimaanisha wachafu watoke wakiache chama salama lakini kutokana na kujikuta hata viongozi wa kuwatoa hao wasio wasafi nao wachafu ngoma ikadunda na kuwaacha vijana hawa wakisubiri embe chini ya mnazi kwa kuamini '' Utatuzi wa tatizo huanzia ndani'' ,nasisitiza kuna vijana makini sana CCM.

Hasi : Wengi wao kimtizamo hasi huwa ni vijana wachumia tumbo ,wanaamini katika kujipendekeza kwa wakubwa na sio kusimamia wanachokiamini,wameziba masikio yote kwani kufanikiwa kwao ni kuteuliwa kuwa wakuu wa wilaya ,wakurugenzi n.k ,sababu inayopelekea kukomalia msimamo huu ni mfumo wa chama kuwazawadia vijana wa hivi staki kutaja vijana waliofanikiwa kujipendekeza itaharibu u -neutral wa hoja ,eneo zuri waliloaibikia ni ushabiki kwa lowasa ,sisemi kumshabikia ilikuwa kosa laa huo ni msimamo wao ninaouheshimu ,tatizo ni jinsi walipogundua chama kimemgaya na wao walimgeuka kama hawamjui wakati niritarajia wakae kimya (wachutame) pamoja na makamilifu mengi ya mamvi ni wazi alitumia sana rushwa kushawishi hawa malaya wa kisiasa .Kwa minajili ya kubakiza hoja kuwa neutral Mamvi namheshimu na sio focus ya hili ,focus ni vijana

4.CHADEMA :

Chanya : Hawa na ni vijana makini na wazalendo tena niwaongezee na kaujiko ni vijana wasomi halisi,hawa na wale makini wa CCM ni wa aina moja tofauti ya hawa wengi wana shughuli zao hivyo hawana haja ya kujipendekeza kwa system wameamua kuchukua hatua ya wazi kuleta mabadiliko ,na hawana muda kusubili chama kibadilike ndo yaje mabadiliko wameweka mbele haja ya mabadiliko juu ya kustawi kwa chama ,na hawa hata CHADEMA ikimess up au wakapewa option mbadala ya kuitoa CCM watachagua hiyo dhidi ya ustawi wa chama .

Hasi :Ni vijana wanaoichukia CCM bila kupata muda wa kutafakali mazuri machache iliyonayo kiasi wanawaza kuruka toka meli mbovu ya CCM inayotembea kuangukia kwenye mgomba unaoelea (CHADEMA) Hawakubali kuhoji demokrasia ndani ya CHADEMA ukijalibu wanasema una akili ndogo au wanakuita kilaza ,Kuhoji je ni halali kumchukua mgombea fisadi (kwa mujibu wa viongozi wao ) kuwa raisi ili tu kuishinda CCM kumkabidhi waliyemwita fisadi namba moja ,hapa pia ukitamka kibaya chochote juu ya lowasa, wanaharibu mjadala kwa kutaja mapungufu ya Magu kama kutosimamia vyema demokrasia, kubana uhuru halali wa mikutano ya kisiasa na maandamano kwenye katiba aliyoiapia mbele ya mungu wake wa kikristo,mungu asiyedhihakiwa(kwa mujibu wa biblia).Hawa vijana akisema kesho Mbowe magu ni kiongozi safi kesho wataanza kumsifia

SOURCE: Walifanya hivyo kwa Dr slaa

5.Wasio na chama chochote

Chanya : Hawa ni wazalendo wanaopenda kesho iliyobora bila kukaguana sana tulikosea wapi wanataka kuona shule zikiongezeka vijijini sio umaarufu wa aliezileta au chama ,wengi niliokaa nao huwa wamesoma sayansi za vitu sio watu (engineering,physics ,chemistry e.tc) wanafaa sana kwa utendaji na huwa wanamipango inayotekelezeka mdomoni wanasahau basi halijai kwa kuwa na dereva mzuri bali mpiga debe mwenye mbwembe japo wote muhimu

Hasi :Hiki huwa ni kichaka cha wale wasio wazalendo wanaotaka msimamo au chama chochote utakao fanikiwa wawe kwenye upande wa kupatia daima hujificha kwenye kuwa wafanyabiashara wasio na msimamo wowote kisiri wakipiga hela kwa kuaminiwa na pande zote ,wanaharakati au uanasheria wakisingizia sheria kuwa wo wanahaki ya kumtetea yoyote ,Mchungaji Tutu alisema ukiona mnyonge na mwenye nguvu wanapigana halafu mtu anasema hayuko upande wowote ,huyo yuko upande wa mwenye nguvu.

Uchambuzi huu umejikita kwenye kweli chungu hizi :

1.CCM imetuangusha na imeshindwa sana kwa awamu nne si kwamba wamefanya makusudi nia yao ilikuwa njema ila walikosea kiufundi na Kimsimamo.

2.Mh Magu Ameanza vyema sana, nampongeza tena sana sikuwahi kutegemea ubora huu wa kazi toka kwake mungu ambariki kabisa, UKWELI MCHUNGU : Msingi wa kufanikiwa kwake ni kufanya kazi bila kufurahisha pande ,ila anaanza kukosea kama JK anatengeneza tabaka la marafiki zake, na pili anapoteza msingi mkuu wa utanzania UPENDO ,KUCHUKULIANA NA KUVUMILIANA namna anadeal na upinzani inafuta yote haya aelewe hawa wapinzani wamepata nguvu kwa makosa ya CCM ya nyuma sio kwa kuwa na ugomvi na yeye zipo picha nyingi akiwa waziri akicheka na kina mbowe, akisifiwa na luwasa atambue njia pekee ya kujua maovu ya mkeo huwa ni kutembea na adui yake wa kike.

Ila kwa kumuuliza mke wangu umewahi kuchepuka hutojua maisha .Japo nadhani hashauriki kwa muonekano lakini anyway natampigia 2020.

3.CHADEMA&UKAWA Havinauwezo wa kupokea dola viendelee kujiimalisha ndani hususani penye demokrasia pale ,na vione namna ya pamoja kuepukana na upepo wa Lipumba.

4.Namna pekee ya kupeleka nchi yetu mbele ni uzalendo na utawala wa sheria hakuna na haikuwahi kutokea nchi ikaendelea bila kuwepo mawazo kinzani yanayoheshimiwa. Kuna watu walipambana CCM irudi madarakani (na ndo wengi) ili waweze kupata manufaa waliyokuwanayo hapo nyuma (JK big time) leo wao wenyewe ndo wanamlaani magu maana walimsapoti kwa sababu ovu yap amewageuka na ukweli waliomuweka mkuu pale (Nasisitiza aliwekwa hakuwa na ubavu hata ya kuingia top 10) Sisi wengine tulimchagua si kwa kumuamini nooo again big noo ila hatukuwa tukimuamini kabisa luwasa.

TANZANIA NI MOJA NA WATU WAKE NI WAMOJA, KUTOFAUTIANA NDO KUPENDANA.
 

Attachments

  • Y.jpg
    Y.jpg
    4 KB · Views: 17
  • Y2.jpg
    Y2.jpg
    3.8 KB · Views: 21
  • Y3.jpg
    Y3.jpg
    8.7 KB · Views: 19
Back
Top Bottom