NGolo Kante
Member
- Feb 28, 2017
- 80
- 131
Tokyo, Japan. Muungano wa vyama tawala nchini umefanikiwa kushinda idadi ya kutosha ya viti na kufikisha theluthi mbili ya wingi wa viti kwenye Bunge Dogo katika uchaguzi mkuu uliofanyika jana Jumapili.
Baada ya karibu kura zote zilizopigwa kuhesabiwa hadi ilipofika asubuhi ya leo, viti 461 kati ya viti 465 vilivyokuwa vinagombewa vimenyakuliwa.
Kama ilivyokuwa inatarajiwa, chama tawala cha Liberal Democratic (LDP) kinachoongozwa na Waziri Mkuu Shinzo Abe kimepata viti 283 ambavyo ni vingi zaidi ya wingi unaotakiwa wa viti 233. Chama cha Komeito ambacho ni mshirika wa LDP chenyewe kilishinda viti 29 na kuufanya muungano wa vyama tawala ufikishe viti 312.
Kutokana na idadi hiyo ya viti, muungano huo sasa una nguvu zaidi na unaweza kupitisha sheria katika mchakato wa kurekebisha katiba ya nchi hiyo.
Waziri Mkuu Abe amesema hatua ya chama tawala kupewa idadi kubwa ya viti inaakisi mtazamo wa watu kwamba aendelee kutekeleza sera kwa kutumia mazingira ya uthabiti wa kisiasa.
Alisema atafanya kila awezalo kuyafikia matarajio hayo ya watu na atajaribu kutoa matokeo katika utaratibu thabiti.
Hata hivyo, chama cha upinzani cha Constitutional Democratic (CDP) kilifanikiwa kuongeza mara tatu ya idadi ya viti ilivyokuwa navyo kwenye baraza hilo kabla ya uchaguzi na kufikisha viti 54. Kwa viti hivyo, chama hicho kina uhakika kuwa chama kikuu cha upinzani kwenye bunge hilo.
Chama cha Hope cha Gavana wa Jiji la Tokyo, Yuriko Koike kimepata viti 49 ikiwa ni idadi ndogo kuliko ile iliyotarajiwa. Koike amekubali kushindwa kwenye uchaguzi huo na kusema kuwa ana mengi ya kujutia kutokana na kushindwa huko kwa chama chake.
Vyama vyote vya CDP na Hope vilianzishwa muda mfupi kabla kampeni za uchaguzi kuanza.