Chama kimetawala miaka 54 ,kwa nini kinategemea kubebwa ?

Chama kimetawala miaka 54 ,kwa nini kinategemea kubebwa ?

Mwiba

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
7,607
Reaction score
1,760
Inashangaza sana Chama Cha CCM kimekuwepo madarakani zaidi ya miaka 50 ,kama maendeleo wameleta wao kama ni shida wameleta wao ,ikiwa Chama hiki kinajiamini kuwa kinapendwa na wananchi walio wengi ni kwanini kinategemea kushinda kwa magube .

Kinategemea kubebwa ,kulindwa ili kisipoteze uwakilishi katika maeneo mbali mbali hapa Tanzania ,chaguzi zilizomalizika hivi karibuni zimedhihirisha hayo ,kuwa bila ya mkono wa udanganyifu CCM inakuwa vigumu kushinda ,wenyewe wanaziita mbinu ila katika kutafuta haki ya uchaguzi mbinu za udanganyifu hazikubaliki, hilo ,jamaa zangu wa ccm lazima walielewe.

Haiwezekani mpo kwenye madaraka kwa miaka yote hiyo bado mnategemea udanganyifu ili mubaki madarakani ,huko ni kupoteza dira na kuishiwa zaidi tunasema ni kufilisika katika uwanja wa siasa ,tokea ilikuwa kushindwa kwenu ni siri hadi leo hii imekuwa si siri tena ,mnashindwa mchana kweupe na kushindwa kwenu hakufichiki tena ,watoto wadogo sasa wanauelewa wa kushindwa kwenu.

Bado inaonyesha akili zenu hazijakubali kuwa mupo kwenye mfumo wa vyama vingi vya siasa ,mnajiona mpo peke yenu ,huko ni kuchanganyikiwa na kupoteza muelekeo wa uongozi ,kinachoonekana kila awamu yenu inayokuja inakuwa ni ya kujali maslahi binafsi na si ya kujali uongozi na unaowaongoza ,uwajibikaji umekuwa duni kwenu,kila awamu inayokuja inakuwa ni mbaya kuliko iliyopita ,mnatupeleka wapi ?

Kuweni makini na mkubali siasa za kiushindani katika uwanja ulio sawa bila ya kutumia udanganyifu ,kitu gani kinachowafanya msijiamini ,mnaogopa aibu ? Ya kushindwa ,ikiwa hilo ndio reason basi hamfai kuwepo katika medani za kisiasa.kama mnategemea kudaganganya ,mnategemea kubebwa ,hamtaongoza nchi bali itakuwa kama tunavyoona corruptions every angle ,ndizo mnazotuletea na kufika kuviharibu hata vyombo vya dola viwe navyo vinaishi kwa kutegemea rushwa.

Someni alama za nyakati ,nchi zinabadilika ,mnaona,mnasoma,mnasikia yanayojiri nchi zingine si hadithi za kubuniwa ni mambo ya kiuhalisia kabisa ambayo yanahitaji mtu aliepo madarakani kujifunza na kuyakubali ukweli na sababu zake ,isiwe mnazikumbatia sababu na kujiona mtaweza kuzihimili na kuziweka chini ya udhibiti ,halitakufaeni jeshi wala polisi mambo yakiteguka ,labda nyie na mali zenu na hela mlizokwapua mtakimbia ,wananchi watakaobakia ndio watakaoteseka ,japo hilo haliwashughulishi ,lakini hisia za mtu na nchi yake ni majuto hapo baadae.

CCM jipangeni katika medani za kisiasa na muwache mara moja kutegemea kubebwa na kulindwa huu si wakati wa kuyakumbatia hayo ,aachwe alieshinda kiuhalali apewe ushindi wake kwa amani kabisa na kwa moyo mkunjufu sio kulazimisha ni lazima fulani au chama fulani kishinde na kulazimisha mwengine aonekane ameshindwa ,maendeleo katu hayatapatikana kwa njia hiyo katika Nchi hii.
 
Je cha kujiuliza ni kipi ? CCM wanakimbia kivuli chao kiasi ya kuhitaji kubebwa na kulindwa ? Juzi katika hekaheka huko Zanzibar viongozi wa Serikali inayoongozwa na CCM walifungua mashule mepya wakati ndani ya shule hizo hakuna madeski wala vyoo ,ndivyo hivyo kulivyo Mtwara na sehemu zingine ,vyoo vilivyopo mashule ni hatarishi .

Jamani hata kujenga vyoo vya shule serikali inahitaji msaada ? Wanafungua mazahanati vijijini ,zahanati hizo zinafunguliwa ikiwa hazina dawa ,kweli waTz ni wadanganyika lakini mengine si ya kudanganyana tena.

Lipi wanaliogopa CCM hata wakahitajia kufanya udanganyifu ili wapate ushindi na mapingamizi yasio na kichwa wala miguu wakati ,wanajisifu wametekeleza sera na ahadi zao ??? Nawashangaa sana.

CCM wanajisifu wameleta maendeleo ingawa mwenye macho na akili haambiwi tazama wala kuhitaji kufahamishwa ,wamejenga mabarabara tena ya lami,wanajenga flyover tena za kisasa ,wakulima wamepewa kipau mbele ,maboresho makubwamakubwa ya miundo mbinu,NHS wanajenga majumba ya kisasa ,sasa ikiwa mnajilabu mnafanya yote haya hivi mtakuwa bado wananchi hawana imani na nyinyi hata ikawabidi muwe mnajipanga kubadilisha matokeo ya kura na kushirikisha vikosi vya ulinzi kulinda uharamu mnaoufanya ?

Kwanini hamjiamini kupambana kiume ? Katika masanduku ya kura na mshindi na mshindwa wapewe haki yao ya halali ? Je mnatuaminisha waTz kuwa mmezoea vya kunyonga vya kuchinja hamuviwezi ? Mnasahau wakati wa Nyerere kulikuwa na chama kimoja anaeshinda ni huyohuyo aneshindwa hakuna mwengine ila yeye ,leo mambo yamebadilika anaeshindwa yupo mwengine alieshinda lakini bado mnageuza matokeo na kubaki kulekule kwa mgombea mmoja akishinda akishindwa ni yeye.

Mnaitia nchi katika hasara kubwa sana na matatizo katika kulazimisha ushindi wenu ni hatari kwa watu baada ya generation hii au vizazi vijavyo ,mnataka kuiwachia nchi matatizo ambayo yanaweza kuepukika tena kuepukika kirahisi kabisa.

Inavyoelekea wananchi wameanza kuchoshwa na mienendo yenu ya kulazimisha ,ingawa mnajitia uziwi na upofu lakini ukweli wa wananchi umeanza kuonekana sehemu mbalimbali ,ukweli huu utakapounganika ni balaa kwenu na raia wakawaida,watu wameanza kupambana nanyi kwa kuingiana mwilini ,tumeona na kusikia ni jinsi gani CUF imetoa kipigo kwa wasio shinda ambao mmewapa ridhaa za kutangazwa washindi japo hawakushinda ,mmewatafutia balaa.

Leo wananchi wenye hasira wanapambana na vikaragosi vyenu mliowapachika kesho na keshokutwa watapambana na wale wanaokuja kuwalinda na kuwatetea ,leo wamewahi kuamuliwa kesho na keshokutwa hao walinzi mnaowaita watakuja kuokota maiti za mliowachomeka ,mtamlaumu nani ,mtadai na kusema msichukue sheria mikononi ? Mtakuwa mmechelewa kwani mambo mliyapandikiza yamemea na kuota.
 
huu mwaka ni finishing tu


_sitaki kuona kijani
 
Mwiba umesema yote na kwa ufasaha kabisa. Watakuja hapa na kukebehi ukweli huu lakini kama wameshuhudia haya yanayoendelea sehemu mbalimbali basi wameshaujua ukweli.
Hii hali ya wananchi kuamua kutembeza vipigo kwa wachakachuaji wa maamuzi yao badala ya "kumuachia MUNGU" kama walivyozoeshwa hapo awali itawadhuru bila wao kujitambua. Ona yaliyomtokea waziri Mahanga mbele ya kamera za TV na polisi, ni wazi kuwa kama hakungekuwa na polisi karibu leo tungekuwa tunazungumza mengine.
 
Last edited by a moderator:
​wordz......hawa wachumia tumbo wa Lumumba wamelala nini???au hawajalipwa buku saba saba leo???
 
Nchi hii itavurugwa na ccm na si vinginevyo. Kule wilayani mbinga watendaji wa vijiji wananyanyaswa na maafisa utumishi na mkurugenzi wao kwa maeneo yale ambayo wapinzani wameshinda. Sijui ndo hao watendaji ndo wanaopiga kura ama lah! Ccm bila kubebwa mambo hayaendi.
 
Nchi hii itavurugwa na ccm na si vinginevyo. Kule wilayani mbinga watendaji wa vijiji wananyanyaswa na maafisa utumishi na mkurugenzi wao kwa maeneo yale ambayo wapinzani wameshinda. Sijui ndo hao watendaji ndo wanaopiga kura ama lah! Ccm bila kubebwa mambo hayaendi.


Tunaposema viongozi wa serikali ya Tanzania wamepoteza sifa ya kuwa viongozi kwa umma moja ya sababu ni haya mambo yanayofanywa mbele ya macho yao na kushindwa kuyakemea na wanapojaribu kuyakemea inaonekana wazi wanatafuta njia ya kutokea na kuyanyamazisha ,mbuzi wa kafara ni mtindo wa ccm kuepuka aibu ,mmoja wawili wajiuzulu au waachishwe ili wengine waendelee kumega keki iliyoibiwa ,ujanja.

Viongozi waliopatikana na ubadhirifu ni kufukuzwa kazi na malipo sijui mafao yote yanakuwa yanasita na hayarudishwi tena,hilo halipo unaambiwa jiuzulu au kustaafu ,ili ubakie umo ila upo nje mafao yako kila mwisho wa mwezi yanaingia kama kawaida na siajabu kuna mmego utakuwa unatiliwa kwenye acc yako.

Wananchi wamelitambua hilo na sasa lugha hiyo ya kujiuzulu hawataki kuisikia ,kama utawala wenu CCM ni wa kufuata maadili na mnajulikana kwa kulifuata hilo woga wa kufanya uchaguzi ulio na haki sawa unaopambanisha washindani wengi mkiwemo nyie ambao utawala wenu ni msafi upo kwa muda wa zaidi ya miaka 50 ,kwanini msiachie uchaguzi ukafuata mkondo wake na badala yake mnatumia hila kuupindisha na kuulazimisha .mna kosa au dhambi gani zinazowafanya msiwaamini wananchi kama watawachagua kwa umahiri wenu wa kuwa maadili mazuri ya kiuongozi ? Inakuwaje mnakosa kujiamini na wakati nyinyi i waaminifu na hlio ndilo wanalolitafuta na wananchi wanapenda viongozi walio waadilifu.

Pelekeni mliowachagua kwenye kampeni ,fanyeni kampeni zenu,tangazeni sera zenu zilizofanikiwa na kama tulivyomuona Mh.Kinana na mwenzake Nape wamepita wakifufua uhai wa chama mijini na vijijini ,bila ya shaka yeyote tathmini yao waliyoiwakilisha ni kuwa bado wananchi wana imani na Chama kwa hio ushindi wa Chama hauna shaka ,So and well wananchi wamesikia na kila mmoja wetu amelisikia hilo ,ilaccm haohao unapofikia uchaguzi wanakuwa wao ndio wenye kufanya makosa ,ile imani ya ushindi usio na shaka inawapotea ,hawanayo tena wanajiweka katika kundi la kushindwa na kuanza kufanya uharamu kabla hata ya uchaguzi na kupandikiza wapiga kura ,kupandikiza kura kiasi ya kuathiri idadi ya waliojiandikisha kupiga kura .na matokeo yake hata sehemu uchaguzi haukufanywa inatangazwa CCM imeshinda kwa kikegezo kisichojulikana.

CCM kama hamuikubali hali iliyopo Tanzania kwa sasa mtapata shida sana na shida hiyo itawapelekea kufanya vitendo vya kinyama zaidi ,fahamuni kuwa Chama chenu CCM kilinenepa na kikawa kinene chenye kumvutia kila mmoja unene wenu ulikuwa na haiba ya kupendwa na kila mtu anaekifuatilia siasa zake na kuwafanya mtanuke nchi nzima ,na uongozi wenu kuwa mkubwa sasa mmekumbwa na maradhi maradhi mabaya sana ,chama kimeanza kukonda na kinaendelea kukonda hadi kitafikia kama hali iliyokuwa nayo kabla hakijaanza kunenepa ,mfano huu unaweza kuupata kwa CUF ilinenepa ghafla ikakonda lakini ipo na inafanya siasa ,na nyinyi muikubali hali hii ya kukonda bila ya kuathiri wananchi kwa kukonda kwenu ikawa mnalazimisha mambo ,kwa hali yeyote ile ikubalini hali ya kukonda kadiri mtakavyojaaliwa na iwe mnafanya siasa za kistaarabu vinginevyo mtaizulia nchi hilaki na mfadhaiko.

Muamko wa wananchi ni mkubwa sana nyie mnapendwa na wengine wanapendwa kuwazuia wengine wasipendwe hakutokubaliwa na wanaowapenda lazima wataidai haki hiyo kutoka kwenu na hawataiacha dhulma hio iendelee ,wataizuia kwa maneno kama haizuiliki watatumia vitendo na ndio palipofikiwa hawawezi kuachilia muendelee kuwadhulumu haki yao ya kupenda wanakokutaka.
 
Back
Top Bottom