Chama imara chenye Sera na Ilani Madhubuti

Chama imara chenye Sera na Ilani Madhubuti

Joined
Jan 16, 2014
Posts
23
Reaction score
11
Wana jukwaa naomba mnijuze, hivi Ilani za Vyama mbalimbali hapa nchini ni zipi? Nimebahatika kuiona Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) peke yake ila za vyama vingine sijaziona.

Mwenye nazo naomba anitumie.
Screenshot_20230604-203304_Adobe%20Acrobat.jpg
 
Nadhani hakina Sera madhubuti ndo Maana polisi imekuwa msaada wao.wakat wa Uchaguzi

Mpaka polisi wanaomba mda wa Uchaguzi wawe likizo au masomoni

Ni aibu sana
 
Ilani ya CCM sio ilani, bali ni orodha ya mahitaji ya kila binadamu humu duniani. Walichofanya ccm ni kuorodhesha kila hitaji la binadamu hata aliye nje ya Tanzania, kisha ikitokea wakafanikisha moja wapo ya kilichopo kwenye hiyo list, basi wanadai wametekeleza ilani yao! Mtu asiye na vipaombele tu ndio anaweza kuandika ilani kwa mtindo huo wa CCM.

Huu ni udhibitisho kuwa CCM imefikia mwisho wa uwezo wake, ndio maana inafanya mambo kwa uhuni wa aina hiyo. Ukitaka kujua kuwa ni uhuni, fuatilia utekelezaji wa hiyo orodha iitwayo ilani, utakuta inatekelezwa kwa kurukiarukia mambo, na mengi yanafanyika kwa kiwango duni, lengo ni kuwahi propaganda za kuwa wanatekeleza ilani yao.
 
Ni CCM pekee yenye kuwa na ilani kila uchaguzi inayokidhi matarajio nakukata kiu ya watanzania,Ni CCM pekee yenye kuwa na ilani kila uchaguzi inayoendana na mahitaji ya watanzania,Ni CCM yenye kuwa na ilani kila uchaguzi yenye kujibu maswali ya watanzania,Ni CCM pekee inayokuwa na ilani yake kila uchaguzi yenye kubeba Sera na ajenda zinazogusa maisha ya watanzania,ndio maana inaungwa mkono ,kuchaguliwa na kupita kwa kishindooo katika kila uchaguzi.

Mavyama mengine Ni ya msimu tu,Ni wasaka tonge tu,Ni vikundi vya wasaka fursa,Ni vyama vya kurithishana Kama ilivyo kwa chadema kwa mtu kumuachia Chaka mkwe wake Kama kitega uchumi chake na ndio maana huko Chadema ukigusa ukigoda tu Ni sawa na kulamba sumu kwa ulimi wako mwenyewe.

Mavyama hayo ya upinzani hayana Sera Wala ajenda Wala maono,Ni vyama visivyoweza hata kuandaa mgombea Urais na ndio maana mwaka 2015 ilibidi Chadema waazime mgombea kutoka CCM ,ambapo wakawa hawana hata ilani zaidi ya kuwaambia wafuais wao waliojikatia Tamaa kuwa wakaitafute kwenye MTANDAO.

Hinyi ningekushauri usipoteze muda wako kuzitafuta ilani zao za upinzani maana wao huenda kimzuka mzuka tu kulingana na biti la mgombea wao na kile kinachomjia kichwani na mdomoni mwake. Ilani ya upinzani Ni mgombea mwenyewe ndio ilani Yao.
 
JIwe wala hakunadi chochote. Aliubaka na kuunajisi uchaguzi.

Sitaki hata kumkumbuka.
 
Vyama vingine havina ilani, huwa vinapuyanga tu.
Sasa kama pale Ufipa st, nani mwenye uwezo wa kutengeneza ilani? Toka Dr Kitila aondoke hakuna cha ilani wala jamaa yake!
 
Back
Top Bottom