Chama chajiandaa na chaguzi ndogo

Kakulwa P

JF-Expert Member
Feb 8, 2012
200
72
Mojawapo ya vyama vikubwa hapa nchini juzi kilifanya kikao chake nyeti na kutoa tamko la kuchangisha pesa kutoka kwa wale wanaokiunga mkono kwa ajili maandalizi ya chaguzi ndogo mkoani Kagera.

Baada ya kikao hicho baadhi ya waalikwa walisikika wakisema chama hiki kinajuaje kama kutakuwepo uchaguzi mdogo kuanzia ngazi ya Kata au ubunge? Na kwanini washirikishwe kutoa michango kwa ajili ya chama hicho?

Najua kuna wanaJF watakaotoa majibu kama ya Lusinde Mb. lakini kwa vyama makini hii ni changamoto kubwa ya kufanya ufuatiliaji na kujiandaa.
 
Mojawapo ya vyama vikubwa hapa nchini juzi kilifanya kikao chake nyeti na kutoa tamko la kuchangisha pesa kutoka kwa wale wanaokiunga mkono kwa ajili maandalizi ya chaguzi ndogo mkoani Kagera.
Baada ya kikao hicho baadhi ya waalikwa walisikika wakisema chama hiki kinajuaje kama kutakuwepo uchaguzi mdogo kuanzia ngazi ya Kata au ubunge? Na kwanini washirikishwe kutoa michango kwa ajili ya chama hicho?
Najua kuna wanaJF watakaotoa majibu
kama ya Lusinde Mb. lakini kwa vyama makini hii ni changamoto kubwa ya kufanya ufuatiliaji na kujiandaa.

Sasa wewe ukiandika kama Lusinde unatarajia majibu gani?

kwa nini unaandika kwa kufichaficha? huna uhakika? ni bora ungekaa kimya tu wala usingepoteza kitu
 
Taarifa yako haipo wazi. Hata vyama vya kufa na kuzikana vyaweza kuwa vyama vikubwa, na ndivyo wanavyochangishana kabla ya misiba. Sasa chama hicho ni kipi?
 
Uzuri wa chama cha Mapinduzi CCM kinapenda kuwa na majimbo mengi saana na Wabunge wengi sana wa kupiga makofi na kuunga mkono hoja hata kama haina Mashiko lakini sio kutekeleza ahadi zake kwa wananchi kama wanavyohahidi wakati wakiomba kura.

Tunawakaribisha tena katika uwanja wa Mapambano kama ilivyokuwa kule Arumeru natumai jibu wamelipata kupitia kwa kiongozi wao mkubwa waliyemtuma Mh,Ben W. Mkapa na bwana mwenye sanduku la Matusi Livingstone Lusinde lakini tunawasihi watoe mchango wa fedha ili tukutane kwenye hilo jimbo wanalolitarajia kupitia mahakama.
 
kagera jimbo gani mkuu.

Ni vizuri sasa tukawaza kwa mapana kuwatafuta viongozi wa vyama vya siasa na kuuliza vyenye usajili wa kudumu au kutumia intelijensia ya vyama kujua undani wa kikao hiki kilichofanyika, huenda kuna kesi za chaguzi ndani ya Kata au jimbo ambazo upepo unaelekea kutengua matokeo yaliyopo sasa.

Vyama vya siasa na wanachama wake wanao wajibu kwa hili, lakini mimi huwa sina wakati mzuri kuchangia majibu ambayo siyo maana na jambo ambalo nimeliweka hapa ili tuliangalie kwa mapana tusije kujifunika kunakucha.

Hawa ndugu zangu wanaojibu kama muonavyo mie si mnywaji wa gongo wala halinifanani ila ni wao kuulizia kwenye vyama vyao kuwa vikao hivyo nyeti vimejulikana siyo siri tena.

Jaslaws umeonyesha njia ya namna ya kuleta mjadala mpana ambao mwisho wa siku tutapata kile kilichojiri kikaoni, wale wasio na hoja za kisiasa nao wanazo hisia zao kwa mujibu wa katiba yetu hivyo mawazo yao nayaheshimu, mimi nasema tena kwa vyama makini vifanye juu chini kufuatilia hili jambo lina maana kubwa.

Wakati wameanza kwa vyovyote wanajua kinachokuja.
 
Back
Top Bottom