kama vp nendeni habari maelezo, tangazeni nia na tarehe ya kuchoma moto vyeti vyenu kwa kua havijawasaidia chochote. Naamini watapay attention na wanaweza kuwakumbuka.
Ni mtazamo tu msikasirike washkaji haya mawazo tu
wanajamii wa TZ, tatizo la ajira linazidi kuwa kubwa na tabaka la wenye nacho na wasionacho linazidi kuwa kubwa, hii inatokana na ukweli usiojificha kwamba waliotokea kwenye familia za viongozi au matajiri ndio wanaopata ajira hata kama hawana sifa.
Pia nasikia kuwa serikali haina hela ndio maana hawatoi ajira.
PENDEKEZO
- Naamini vijana tusiokuwa na ajira tupo wengi sana, na viongozi wetu hawajali maana wakwao wanapata ajira mdebwedo, kwa hiyo tuungane tuwe na chama ambacho kitaweza kutoa PICHA HALISI ya tatizo la ajira. Labda wanaweza kuona ni serious issue.
- chama hicho kiwe na viongozi kutoka kila Profession
- Chama hicho kichunguze taratibu zote na vigezo vinavyo tumika ktk kutoa ajira
- Chama hicho kishawishi serikali kupunguza matumizi makubwa ya fedha yasiyokuwa na ulazima ili hicho kidogo kinacho patikana tugawane wote. mfano; magari ya kifahari kwa viongozi, semina na tume ambazo huwa ni uwizi mtupu kwani nyingine hazifanyiwi kazi zinabaki kwenye makaratasi tu, na......... na........
- Pia vijana wataelimishana juu ya kujiajiri na kukabiliana na changamoto za maisha.
NAAMINI KWA PAMOJA TUKIAMUA CHAMA HIKI kitakuwa na wanachama wengi na kitakuwa na nguvu kuliko vya kisiasa maana wanachama wake ni VIJANA na wana NGUVU kimwili na kiakili.
Wàzo zuri muanzisha uzi, ila icje ikawa unataka ujiajiri kwa ada zetu za uanachama maana tusio na ajira kimsingi ni wengi sasa kweli wote tukijiunga kwenye huu umoja wako hata tukilipa fee 500 kwa mwezi aaah si haba milioni hukosi kwa mwezi halaf unapotelea Mgeta huko Milimani!
Na suggest jina TANZANIA GRADUATES UNEMPLOYMENT ASSOCIATION TGUA