Chama cha Wapangaji Tanzania

Pastor Achachanda

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2012
Posts
3,023
Reaction score
1,317
Habari humu ndani. Huku tunakoishi kuna tabia ya wenye nyumba kuwanyanyasa wapangaji wao hadi kero. Na si rahisi kwamba kila mtu ajenge.

Nimepokea familia moja iliyofukuzwa kwenye nyumba waliyopangishwa kisa zimepita siku 4 tangu kodi yao iishe. Mwenye nyumba amekuwa mkali si kawaida hataki hata kuwaona. Bila aibu ameita vijana kuhamishia nje vitu vyao.

Kero hizi zipo nchi nzima. Je hatuoni haja sasa ya kuwa na chama cha kusimamia sheria, haki, wajibu na kanuni zitakazolinda maslahi za wamiliki wa nyumba na wapangaji?

Waheshimiwa wana JF naomba kuwasilisha hoja.
 
Yaan zimepita siku 4..! huku kwingine kama una mpango wa kuendelea kukaa basi unatakiwa u-renew miezi 3 kabla.., we vipi wewe.., sasa ulitaka wakae bure.., EBO!.., af mkiambiwa rudini Igunga mnakuwa wabishi.., pamejaa huku hamsikii..
 

Tanzania kuna vyama vya ajabu ajabu. Chama Cha Wapangaji Tanzania. Kule Temeke kuna Chama kinaitwa "CHAMA CHA WASIO NA VYAMA "
 
Sasa siku nne kodi imeisha kwanin asitoe taarifa mapema kama anatatzo?? Ndio mana kuna mikataba ebo!!
 
Napangisha nyumba. s.room. master b.room and a kitchenette. water 24/7 Mbezi analogia. 180 metres from bus stand
 
Mkuu FRANCIS DA DON, angetumia japo busara kuvumilia kwa siku kadhaa. Hela ngumu yafaa kuchukuliana.

Yaan zimepita siku 4..! huku kwingine kama una mpango wa kuendelea kukaa basi unatakiwa u-renew miezi 3 kabla.., we vipi wewe.., sasa ulitaka wakae bure.., EBO!.., af mkiambiwa rudini Igunga mnakuwa wabishi.., pamejaa huku hamsikii..
 
Mkuu FRANCIS DA DON, angetumia japo busara kuvumilia kwa siku kadhaa. Hela ngumu yafaa kuchukuliana.
Hakuna kitu kama hicho..!! unatakiwa u-renew 3 months before.., huyo hakujipanga kabisa.., rent is not an emergency my friend..., hawa ndio wake zao imefika siku ya kujifungua hana hata senti mfukoni.., upuuzi huu..!!
 
Ooyooo huyo mwenye nyumba ni mhindi au mwaarabu au mpemba na vipi picha yao
 
Sheria ipo. Inaitwa Sheria ya Ardhi Tanzania. Sema binadamu wengi (sio Watanzania tu, hili ni tatizo la dunia nzima) sio watu wa kusoma, bali ni watu wanaopenda kusomewa.

Kwa mujibu wa sheria ya ardhi (kifungu sitakupatia, vifungu huwa vinalipiwa) kodi yako ikishaisha wewe ni mvamizi sio mpangaji tena. Kwa hiyo mwenye nyumba ana haki ya kukufukuza kwenye nyumba yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…