Chama cha Wanasheria Tanzania Chatoa kauli Kuhusu Zanzibar

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Chama Cha Wanasheria wa Tanganyika [TLS] kimepokea kwa mshtuko; kimehuzunishwa na kimesikitishwa sana na kauli, tahadhari, onyo vilivyotolewa na Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar, Naibu Kamishna wa Polisi Salum Msangi aliyoitoa tarehe 28 Juni, 2016 wakati akiongea na waandishi wa habari kisiwani Pemba.

Kauli, tahadhari, na onyo aliyoitoa Kamanda Msangi viliripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari na mkanda wa video kusambazwa katika mitandao ya kijamii. Katika mkanda huo Kamanda Msangi anasikika na kuonekana akitoa matamshi ambayo kwa tafsiri ya kawaida yanaonesha kuwa na taathira ya kuwatisha mawakili na wanasheria watakaojitokeza kuwatetea watuhumiwa wa makosa mbalimbali ya jinai kwa kusema kuwa wakiendelea na utaratibu huo na wao watashitakiwa pamoja na wateja wao.

Kwa ufafanuzi tunarejea tena kauli hiyo kama alivyonukuliwa kutoka kwenye mkanda wa video akisema yafuatayo:-

“baadhi ya wanasheria, kwa sababu tumepata taarifa kuna wanasheria wanafikiri kuwa wameshapata fursa ya kujipatia pesa kwa ku, kwa kujifanya wanatetea wahalifu. Kwa hiyo akikamatwa mhalifu, wao wanakimbilia hapo na kuna makoti yao. Wana, wana, wanataka sijui dhamana sijui wanataka kitu gani sijui. Tunatoa tahadhari, ee, kwamba, tunawashauri waache tabia hiyo mara moja kwani wakibainika wataunganishwa na wahalifu katika makosa waliyoyatenda ili waka, wakateteane wenyewe huko ndani watakapokwenda..”

Baada ya kutafakari kwa kina kauli hii ya Kamanda Msangi na baada ya kushauriana na Chama cha Wanasheria wa Zanzibar [ZLS] ambao walishatoa tamko lao; Baraza la Uongozi la TLS linapenda kutoa tamko rasmi kama ifuatavyo:-

1. Chama cha Wanasheria wa Tanganyika kinalaani na kupinga kwa nguvu kauli, tahadhari pamoja na onyo vilivyotolewa na Kamanda Msangi kwa kuwa vinakiuka Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977; Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, pamoja na sheria za nchi na za kimataifa.

2. Chama cha Wanasheria wa Tanganyika kinapenda kuwakumbusha Watanzania wote ikiwa ni pamoja na Jeshi la Polisi kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ya Mwaka 1977 inataka vyombo vyote vya Serikali, ikiwa ni pamoja na Jeshi la Polisi, kuhakikisha kwamba utu na haki nyinginezo za binadamu zinaheshimiwa na kuthaminiwa kwa mujibu wa ibara ya 9 (a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Haki hizo ni pamoja na haki ya kusikilizwa kwa ukamilifu ambayo inajumuisha haki ya kuwa na wakili, kwa mujibu wa ibara ya 13 (6) (a):

“(6) Kwa madhumuni ya kuhakikisha usawa mbele ya sheria, Mamlaka ya Nchi itaweka taratibu zinazofaa au zinazozingatia misingi kwamba–
(a) wakati haki na wajibu wa mtu yeyote vinahitaji kufanyiwa uamuzi na Mahakama au chombo kinginecho kinachohusika, basi mtu huyo atakuwa na haki ya kupewa fursa ya kusikilizwa kwa ukamilifu, na pia haki ya kukata rufaa au kupata nafuu nyingine ya kisheria kutokana na maamuzi ya Mahakama au chombo hicho kinginecho kinachohusika.”

3. Chama cha Wanasheria wa Tanganyika kinasikitishwa na kuongezeka kwa tabia ya viongozi wa Serikali kutoa matamko ambayo ama yanaingilia mihimili mingine ya dola, au yanaashiria hali ya viongozi kutoheshimu Utawala wa Sheria au dhamira ya kutotaka kubanwa na kanuni za Utawala wa Sheria kwa kutoa matamko au makatazo yanayokiuka katiba pamoja na misingi ya Utawala Bora.

4. Kwamba mtu yeyote anayezuia au kutisha mawakili au wanasheria wasifanye kazi ya kuwatetea watuhumiwa wa Makosa ya Jinai, si tu kwamba anakiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na ile ya Zanzibar, bali mtu huyo pia anakuwa amekiuka sheria za nchi kwa sababu uwakili ni kazi ambayo imeanzishwa kwa mujibu wa sheria za nchi na Mawakili wamesajiliwa kwa mujibu wa sheria na kupewa leseni na Jaji Mkuu ama wa Tanzania au wa Zanzibar ili wafanye kazi ya Uwakili.

5. Chama cha Wanasheria wa Tanganyika kimesikitishwa na kauli ya Kamanda Msangi hasa ikitiliwa maana kuwa ni kiongozi aliyepewa dhamana ya kusimamia utekekezaji wa mfumo wa haki jinai. Tunadhani alipotoka na tunatarajia ataomba radhi kwa uungwana wa kiTanzania ili kurudisha imani ya Mawakili na Watanzania kwa Ujumla wao juu ya utendaji kazi wake.

6. Chama cha Mawakili wa Tanzania kinaamini ya kwamba kauli ya Kamishna Msangi ya kutokutambua uwepo wa mawakili na kazi zao ni ishara tosha kuwa Kamanda Msangi amejivisha Kazi ya Mahakama na ameshawahukumu kabisa watuhumiwa wa makosa ya Jinai na kuona hawana haki ya kuwa na utetezi.

7. Chama cha Wanasheria wa Tanganyika kinapenda kumkumbusha Kamishna Msangi ya kwamba Mawakili ni Maafisa wa Mahakama Kuu na wanao wajibu wa kuwatetea Watanzania wote bila kujali imani zao; hali zao za kifedha au mitazamo yao ya kisiasa.

8. Tunapenda kuchukua fursa hii kulikumbusha jeshi la polisi kuwa hakuna mtu ambaye yuko juu ya sheria na kila mtu ana mipaka yake, ambayo tunatarajia Kamishna Msangi na watendaji wengine wote wanaifahamu na wataiheshimu na endapo hawaifahamu basi wajitahidi kuifahamu; kuijua na kuitekeleza.

9. Tunapenda kuwakumbusha Watanzana wote hasa, vyombo vya dola kuwa kwa mujibu wa Kanuni za Msingi za Umoja wa Mataifa za Mwaka 1990 zilizopitishwa mjini Havana, Cuba Tarehe 27 Agosti mpaka tarehe 7 Septemba 1990 ambapo Tanzania ni sehemu ya Umoja wa Mataifa zinatakamka yafuatayo:-

i. Kanuni ya kwanza inaeleza kuwa kila mtu ana haki ya kutetewa na Wakili wa chaguo lake kila hatua ya maamuzi juu ya shitaka lake.

ii. Kanuni ya 7 inazitaka Serikali kuhakikisha kuwa watu wanaokamatwa kwa tuhuma za makosa ya Jinai, ikiwa wamefikishwa Mahakamani au hawajafikishwa, wapate nafasi ya kuwakilishwa na Wakili katika muda usiozidi masaa 24 toka kukamatwa kwao.

iii. Kanuni ya 16 inazitaka serikali zote ikiwa, pamoja na serikali ya Tanzania, kuhakikisha Mawakili wanafanya shughuli zao bila vitisho, Manyanyaso au kuingiliwa kwa aina yoyote na chombo chochote.

10. Chama kinatoa tahadhari kwa baadhi ya watendaji wa jeshi la polisi kuangalia kauli wanazozitoa kwani kauli hizo zinaharibu sifa nzuri za kiutendaji za jeshi hili ambalo tunaamini linafanya kazi kwa nia njema ya kulinda usalama wa raia na mali zao. Tunatambua kuwa Jeshi la Polisi liko katika mchakato wa mageuzi makubwa ya kiutendaji na linapenda kufanya kazi kwa ukaribu na wadau wote hasa katika utekelezaji wa falsafa yake ya Polisi Jamii.

11. Chama kinapenda kuamini kuwa Kamishna Msangi ana mapungufu yake yeye binafsi katika ujuzi wa mambo ya msingi yanayohusiana na kazi anayoifanya na tunaamini anahitaji kupata msasa wa ujuzi wa sheria kwa kupatiwa kozi maalumu ya utawala wa sheria na nafasi ya Jeshi la polisi katika kufanikisha na kukuza demokrasia na utawala wa sharia.

12. Chama cha Wanasheria Tanganyika kinatarajia kufanya mawasiliano rasmi na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, ili kupata kauli rasmi ya Jeshi la Polisi kuhusu matamshi ya Kamanda Msangi na kujua msimamo na mtazamo rasmi wa Jeshi la Polisi kuhusu utendaji kazi wa mawakili katika Tanzania Bara na Tanzania Visiwani kabla ya kutoa tamko la ziada.

13. Chama cha Wanasheria wa Tanganyika kinawaasa wanachama wake na wale wa Chama cha Wanasheria wa Zanzibar [ZLS] walioko bara na visiwani kutotishika kwa namna yoyote na vitisho vilivyotolewa na Kamanda Msangi wala wasirudi nyuma katika kutimiza wajibu wao kwa wananchi kwani Mawakili wanao wajibu wa kisheria na Haki ya kuwatetea watuhumiwa wa Makosa ya Jinai.

14. Chama kinalaani kauli hii ya Kamanda Msangi na kauli zingine zote zinazotishia utendaji kazi wa mawakili au kuingilia utendaji kazi wa vyombo vya utoaji haki, ikiwemo Mahakama.

15. Tunatoa rai kwa mawakili wote wa bara kuwa wasiogope kuchukua vibali ili kuwatetea watuhumiwa walioko Zanzibar, na hali kadhalika Mawakili wa Zanzibar wasirudi nyuma wala kutishika.

Imetolewa kwa idhini ya Baraza la Uongozi la TLS

John Seka
Rais
Chama Cha Wanasheria wa Tanganyika
06.07.2016
 
Chama cha Wanasheria wa Tanganyika kinapenda kumkumbusha Kamishna Msangi ya kwamba Mawakili ni Maafisa wa Mahakama Kuu na wanao wajibu wa kuwatetea Watanzania wote bila kujali imani zao; hali zao za kifedha au mitazamo yao ya kisiasa.

8. Tunapenda kuchukua fursa hii kulikumbusha jeshi la polisi kuwa hakuna mtu ambaye yuko juu ya sheria na kila mtu ana mipaka yake, ambayo tunatarajia Kamishna Msangi na watendaji wengine wote wanaifahamu na wataiheshimu na endapo hawaifahamu basi wajitahidi kuifahamu; kuijua na kuitekeleza.

Hakika!
 
Hawa polisi hivi wanadhani wao hawatataka wanasheria? Wangemuuliza Zombe...Kova na kesi ya kugombea nyumba...sijui hii kasumba kwanini inaota kwa kasi kiasi hii...kweli nimeamini tunaingia katika kiza kinene...!!!
 
hahaha! mtuhumiwa yoyote inabidi awe na wakili. kama hana uwezo apewe na serikali!
 
Aloo...mbona mambo yanakoelekea siko day by day??
What is wrong ??
 
Wanajulikana hiyo familia kwa kujipendekeza! Ona sasa wanavunja katiba! Hafai kuwepo pale! Anataka asogee kwenye CP! Jeshi zima la polisi wanawachukia sababu wanatumika kisiasa kweli kweli ndio wanarushwa vyeo haraka haraka! Hao ndio walimteka Ulimboka!

Who cares!
 
Hili tamko kama kweli limetolewa na chama cha wanasheria Tanganyika,Nikiri wazi kuwa Tanzania hatuna wanasheria.Tuanze kwenda kuwatafuta Rwanda.Bure kabisa.

Kwa sababu zifuatazo:

Ukiangalia hapo namba 6 pameandikwa CHAMA CHA MAWAKILI TANZANIA!!!!!! kilianza lini kiko wapi? Hakuna kitu kama hicho.Tanganyika kuna chama cha wanasheria Tanganyika na Zanzibar kuna chama cha wanasheria Zanzibar.Hicho chama cha mawakili Tanzania ni cha kutunga,kimetungwa na kwa watu wasomi wanaojiita LEARNED BROTHERS AND SISTERS kuweka vitu vya kutunga ni aibu kwa tasnia ya sheria.Kwa sababu hili tamko lina vitu vya kutunga ni NULL AND VOID la kulitupilia mbali na lichukuliwe kuwa ni tamko koko ambalo halijatoka kwenye chama chenye hadhi kama Chama cha wanasheria wa Tanganyika.
 
Hawa wanasheria wa Tz ni zaidi ya uchwara,,,
hawa jamaa linapotokea la kuwahusu ndio utakuta wanaanza kutoa matamko ila kwa kuvunjwa katiba na kukandamizwa raia huwa hawaoni,,,,
Wajifunze kwa wenzao Kenya juzi walivoandamana
 
Back
Top Bottom