Chama cha Walimu (CWT) sitisheni likizo yenu, walimu hawana mtetezi

KAPURO

JF-Expert Member
Feb 12, 2016
235
152
Wakati mwingine huwa najiuliza ni chombo kipi hasa kinaweza kupigania maslahi na haki za watumishi Tanzania nakosa majibu , kuna vyama vingi vya wafanyakazi lakini leo nitasema kidogo kuhusu CHAMA CHA WALIMU ( CWT), hivi malengo hasa ya chama hiki ni yapi ? , na mteja wake ni yupi ? , hivi majukumu ya chama cha walimu yanatimizwa ? binafsi pamoja na kazi kadhaa nzuri zinazofanywa na chama cha walimu bado napata hofu juu ya weledi wao katika kuwapigania walimu (clients wao) , pamoja na kusimamia kesi za walimu kadhaa waliopata matatizo kazini bado CWT wamejisahau mno kutimiza wajibu wao ,

Hivi CWT hata haya mmeshindwa kuyasema kwa faida ya wateja wenu ( clients wenu) , mmeshindwa kabisa kuibana serikali katika mambo haya yanayopoteza matumaini ya walimu , hivi mnasubiri mpaka nini kitokee ndiyo mtimize wajibu wenu dhidi ya wateja wenu , hivi mnamaliza likizo yenu lini, tafadhari sitisheni likizo yenu mje kupigania haya

Mosi, punguzo la kodi kutoka 11% mpaka 9% walimu na watumishi wengine wamelalamikia sana kodi kandamizi na imewahi kuwa agenda ya CWT, mara kadhaa CWT walisikika wakiitaka serikali ipunguze kiwango cha kodi kwa watumishi bahati nzuri sherehe za may 1 za 2016 Mh Rais akatoa ahadi kufikia mwezi July 2016 kodi iwe 9% kutoka 11% bahati mbaya sana mpaka sasa bado kodi ni 11% CWT nao wapo likizo wanasubiri serikali iendelee na uhakiki wa watumishi hewa usio na kikomo, walimu hawana mtetezi katika hili zaidi ya kusubiri serikali yenyewe , CWT inapaswa watoke likizo walisemee hili , lazima watambue hakuna chama cha wafanyakazi chenye undugu na serikali duniani inatakiwa wapiganie maslahi ya watumishi siyo kusubiri maslahi ya watumishi yaboreshwe kwa matakwa ya serikali.

Pili, nyongeza halali ya mshahara (salary increments) ya kila mwaka kuanzia mwezi July 2016 serikali inatoa sababu zile zile za kufanya uhakika wa watumishi hewa na CWT wameingia kwenye tamthilia wamejipa likizo wapo kimya wanasubiri serikali kwa mapenzi yake ndiyo iboreshe mishahara ya walimu , tangu lini chama cha wafanyakazi kikafanya harakati kwa kusubiri serikali haiwezekani na duniani haiwezi kutokea lazima CWT wasitishe likizo waje kuibana serikali ifanye nyongeza ya mishahara ilivyopaswa kufanywa July 2016, siyo sahihi CWT kusubiri serikali ifanye uhakiki wa watumishi hewa usio na kikomo huku watumishi waadilifu wakipunjwa haki zao halali kisheria.

Tatu, kunyanyaswa kwa walimu awamu hii kila kiongozi anatafutia umaarufu na sifa kupitia kwa walimu , maRC, maDC, Wakurugenzi, wabunge, madiwani, tumesikia ya Mtwara RC asafishia nyota kwa walimu, tulisikia kanda ya ziwa mwalimu alipigishwa deki na mkurugenzi walimu wananyanyaswa kwa mwamvuli wa kurejesha nidhamu kwa watumishi, walimu ndiyo imekuwa sehemu ya kupigia mazoezi wanasiasa huku CWT wakiwa likizo hawana habari hata wakijitokeza wanaishia kupiga mikwala na kurudi likizo ya kukaa kimya , CWT lazima msitishe likizo mkiweza fanyeni ziara kwa wateja wenu hali siyo shwari wateja wenu wanakula vitisho kutoka kwa wanasiasa na watendaji wenye mabavu yao tena wanatumia kinga ya HAPA KAZI TU.

Nne, malipo halali ya likizo siku hizi malipo ya likizo imekuwa historia sijui kanda nyingine lakini walimu wanadai na kudai bila mafanikio tena wanapewa majibu mepesi, hakuna fedha ! , tutawalipa tukipata fedha ya ziada !, tunatawalipa kwa awamu ! yaani walimu wanapewa majibu utadhani siyo haki yao mbaya serikali /halmashauri ilipe kwa matakwa siyo kwa wakati kuna walimu wanadai malipo yao ya likizo mwaka, miaka mpaka wanasahau halafu chama cha walimu CWT wapo likizo wameipisha serikali ifanye inavyotaka kwa watumishi/walimu CWT tokeni likizo walimu hawana mtetezi rudini kazini mpiganie malipo halali ya likizo za walimu .

Tano, ajira mpya za walimu serikali kwasababu zake imeamua kutoa majibu rahisi eti walimu wapo wa kutosha wakati hali halisi walimu hawatoshi kabisa iwe wa sanaa , biashara na sayansi bado kuna uhaba mkubwa wa walimu na mzigo kwa walimu ni mkubwa mno ukingatia elimu bure imekuja na hamasa kubwa kwa wazazi, kidato cha kwanza sasa wanaripoti wanafunzi wa kutosha, darasa la kwanza ndiyo usiseme lakini serikali imeamua kurahisisha mambo kwa jibu jepesi tu " WALIMU WANATOSHA TATIZO WAMERUNDIKANA" chama cha walimu siyo wajibu wenu kuajiri lakini mnapaswa kulisemea hili haraka, serikali lazima ifungulie ajira za ualimu kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari bado walimu ni tatizo , tokeni likizo mapema huku wateja wenu hawana mtetezi wakiomba kuongezewa walimu waambiwa waache uvivu.

Sita, posho za kusimamia na kusahihisha mitihani ya mock ,Kulikuwepo utaratibu mzuri walimu kulipwa kwa kazi ya kutunga, kusimamia na kusahihisha mitihani ya mock kidato cha pili , tatu na nne kimsingi ni malipo halali kisheria lakini ghafla serikali kwa makusudi imeondoa malipo hayo na kuwataka walimu wafanye majukumu hayo bure asiyetaka aache kazi mara moja , sijui ndiyo kubana matumizi au hayo pia yalikuwa madili, mwalimu mwenye malipo kiduchu anaminywa huku Wakurugenzi, maDAS, maDC, maRC, wabunge na wanasiasa wengine wakiendelea kulipana posho kwa ziara za kwenda kutumbua majibu CWT wapo likizo hawana habari waipisha serikali ibane matumizi mpaka kwa malipo halali ya walimu , tafadhari CWT sitisheni likizo yenu wateja wenu (clients wenu) hawana mtetezi rudini mdai haki hii ya walimu iliyominwa bila sababu.

Saba , kupandishwa madaraja walimu hapa ndiyo balaa tupu walimu wamepoteza matumaini hata waliopata bahati walirejeshwa kusubiri uhakiki wa watumishi hewa usio na kikomo, walimu walipandishwa madaraja miezi kadhaa ghafla wakaambiwa zoezi limefutwa kupisha uhakiki sijui na maslahi yao yamekumbwa na uhakiki au watapewa malimbikizo baada ya uhakiki , kwa utaratibu mwalimu inatakiwa apande daraja baada ya miaka minne mmoja wa probation na mitatu baada ya kuthibitishwa kazini lakini ajabu kuna walimu wana miaka sita(6) mpaka saba kazini hawajui habari za kupanda daraja na ni marufuku mwalimu kudai apandishwe daraja mpaka serikali iguswe , CWT hata hili hamlioni kweli hiyo likizo yenu inawagharimu walimu tafadhari msikubali kucheza ngoma ya uhakiki wa watumishi hewa ilisiyoisha utamu kwa serikali, anzisheni vuguvugu kudai madaraja ya wateja wenu (clients wenu) waofanya chama kiwepo.

Nane, uhamisho halali wa walimu suala ya uhamisho imekuwa hadithi ya kusadikika kwa walimu hata akiwa na sifa zote za kuhama ataambulia majibu ya kuumiza moyo , hata akipewa utaratibu akiufuata bado vitaibuka vikwazo kipindi ndiyo kabisa hakuna kuhama vituo vya kazi maana HAPA KAZI TU, lazima kufanya kazi utadhani mwalimu anaomba uhamisho ahame nchi moja kwa moja, mtu anakwenda kuwatumikia watanzania wale wale , wenye mahitaji yaleyale bado anazuiliwa kuhama wengine wanaambiwa wachague moja kutohama au kuacha kazi waende watakapo, CWT jitokezeni mpiganie walimu wenu uhakiki wa watumishi hewa hauishi utamu kwa serikali, jitokezeni muitake serikali iruhusu uhamisho halali kwa walimu wenye vigezo vya kuhama, walimu hawana mtu wa kupigania uhamisho wao halali uliokumbwa na uhakiki wa watumishi hewa, CWT sitisheni likizo yenu rejeeni kazini walimu hawana mtetezi unyonge wao unatia huzuni.

Tisa, madeni ya muda mrefu ambayo bado yapo kwenye mchakato yanachakatwa miaka na miaka bila kuchakatika walimu wana miaka nenda rudi wanaidai serikali kila mara serikali inawataka wajaze fomu , waandike barua za madai tena na tena maana kwenye michakato mafaili yanapotea kweli kweli , kuna walimu wanakaribia kustaafu madeni yakiwa kwenye mchakato awamu hii ndiyo kabisa uhakiki wa watumishi hewa umepitia kwenye mchakato, madeni yapo kwenye uhakiki ili serikali isilipe hewa na CWT imetoa baraka kwa serikali ichakate madeni ya walimu bila kumaliza , serikali ina mipango mingi lazima CWT ilete vuguvugu vingine madeni ya walimu yote yatakuwa hewa .

Kumi, mikopo halali kwa walimu kuzuiliwa kwa mwamvuli wa uhakiki wa watumishi hewa, wakati serikali ikitafuta mikopo kutekeleza majukumu yake watumishi wake hawana ruhusa kuomba mikopo kwenye Taasisi za kifedha maana wanaweza kuomba watumishi hewa na CWT imekubali walimu wakose fursa halali ya kuomba mikopo yenye tija , CWT ipo likizo huku walimu wakilalamika kuhusu mikopo bila mtetezi , serikali haiwezi kuruhusu kirahisi bila msukumo kutoka nje na chama cha walimu kina nafasi ya kuisukuma serikali iache kuminya haki ya walimu kuomba mikopo kwenye Taasisi za kifedha. CWT sitisheni likizo wateja wenu hawana mtetezi njooni upesi likizo yenu inawagharimu walimu.

Mwisho, CWT ukimya wenu unatia shaka sana wateja wenu hawaelewi dhamira yenu wanashindwa kutambua mpo upande upi wengine wanaenda mbali sasa wanadhani ninyi ni mawakala wa serikali, ukimya wenu unaongeza maumivu ya fedha 2% mnazokata kwenye mishahara yao kiduchu, wateja wenu (clients) hawana mtetezi sasa hawajui salama yao ipo wapi , bila nguvu yenu mwalimu mmoja mmoja hawezi kusimama kudai maslahi na haki zake zinazominywa kwa mwamvuli wa HAPA KAZI TU,

CWT likizo yenu ya ukimya isitisheni walimu wanahitaji juhudi na weledi wenu kipindi hiki kuliko vipindi vyote, walimu wanahitaji ujasiri wenu dhidi ya serikali, ikumbusheni serikali ipitishe jicho la huruma kwa walimu , hakuna elimu bora pasipo maslahi na haki za walimu , walimu wapewa kipaumbele elimu haiwezi kuwa bora kwa kuwatazana wanafunzi na mahitaji yao huku matatizo na changamoto za walimu zikupuuzwa, CWT rudini kazini mlete vuguvugu walimu wapo tayari kuwaunga mkono,

Nawatakia tafakari njema Rais wa CWT, makamu wake, katibu wake mkuu na watendaji wote wa CWT sambamba na wadau wa elimu wote.

Mkiwa upande wa walimu kupigania haki , maslahi na kutatua matatizo yao kila mwalimu hatajuta kukatwa 2% kwenye mshahara wake na CWT .

MWALIMU NI CHACHU YA MABADILIKO.
 
Hivi hicho chama kipo kweli? If so Kazi yao huwa ni nini eti?
Ningewashauri walimu kujitoa kwenye hiki chama na Kujiunga vyama vingine kwa mujibu wa Sheria..
This is a useless thing.
 
Tena Mkuu hata kwenda kudai hayo madeni halmashauri unaambiwa uende na kibali cha kukuruhusu ww kwenda kwa afsa Utumishi vinginevyo husikilizwi,kweli walimu wana kila sababu ya kufelisha watoto wetu asee
 
Back
Top Bottom