Chama cha walimu(cwt) na ndoto za kibepari.

bangra

Member
Joined
Nov 16, 2013
Posts
16
Reaction score
0
Siku za usoni chama cha walimu(CWT) Kitaanzisha Benki wanayoinadi kuwa ni ya walimu kitu ambacho ninakipinga kwa sababu katika mfumo wa kibepari kuna matabaka makubwa mawili; tabaka la wamilikaji njia kuu za kiuchumi(hapa ni viongozi wa CWT) na wafanyakazi (na hapa ni walimu).kwa maana hii tabaka la wamilikaji mali katika mfumo huu wanamiliki kila kitu ikiwemo wafanyakazi na kwa njia hii wanafanya kila liwezekanalo kupata faida na kuendelea kupata faida.

Hoja hapa ni kwamba walimu ndio wanaokatwa pesa zao na hata mtaji wa beki hiyo ni majasho ya walimu, swali mwalimu atafaidikaje na faida itakayopatikana? Hapa hakuna namna ya mwalimu kunufaika kwa faida itayopatikana. Mikopo? Hii ni kitaalamu ipo katika kundi la distribution na kwa kuwa kila mkopo huwa una riba basi panatakiwa kuwe na kitu kinachoitwa redistribution. Lakini kitu hiki (redistribution) ktk ubepari hakipo na kwa maana hii benki hiyo itakuwa ni chombo cha unyonyaji dhidi ya mnyonge. Itakumbukwa wakati cwt inaanza walimu walikaririshwa kuwa mbiu ya mnyonge ni umoja lakini kwa hali itakavyokuwa ni kinyume chake.

Binafsi siuungi mkono benki hiyo na napendekeza uanzishwaji wa viccoba na saccos za walimu kama mbinu ya kuwakomboa walimu.

Lakini pili michango ya walimu kuanzia mwaka ambao benki itaanza ihesabiwe kama hisa ambazo watakuwa ni kama wamezinunua kulingana na makato ya kila mwezi na hili litawapatia walimu faida kwa kadiri ya hisa zao na hii si tu itawanufaisha walimu pia itawavutia watu wengine ama kuwa walimu au kupata fursa ya kuwa wanachama wa CWT.

Ahsanteni Nawasilisha.
 
Subiri waanzishe halafu tuone utendaj wake ukoje halfu hapa tutapata jambo la kujadili
 
Nimetokea kuichukia sana CWT kwanza kimeacha kabisa kutetea maslahi ya walimu na kujikita katika biashara , walimu wanaidai serikali na serikali haitaki kulipa haya madeni CWT imekaa kimya alimradi inakusanya mabilioni ya fedha kutokana na makato ya mishahara ya walimu.
 
Hakuna chama pale. Viongozi wamekiwa mabepari wamemwacha mwalimu na chaki yake.
 
Siku za usoni chama cha walimu(CWT) Kitaanzisha Benki wanayoinadi kuwa ni ya walimu kitu ambacho ninakipinga kwa sababu katika mfumo wa kibepari kuna matabaka makubwa mawili; tabaka la wamilikaji njia kuu za kiuchumi(hapa ni viongozi wa CWT) na wafanyakazi (na hapa ni walimu).kwa maana hii tabaka la wamilikaji mali katika mfumo huu wanamiliki kila kitu ikiwemo wafanyakazi na kwa njia hii wanafanya kila liwezekanalo kupata faida na kuendelea kupata faida.

Hoja hapa ni kwamba walimu ndio wanaokatwa pesa zao na hata mtaji wa beki hiyo ni majasho ya walimu, swali mwalimu atafaidikaje na faida itakayopatikana? Hapa hakuna namna ya mwalimu kunufaika kwa faida itayopatikana. Mikopo? Hii ni kitaalamu ipo katika kundi la distribution na kwa kuwa kila mkopo huwa una riba basi panatakiwa kuwe na kitu kinachoitwa redistribution. Lakini kitu hiki (redistribution) ktk ubepari hakipo na kwa maana hii benki hiyo itakuwa ni chombo cha unyonyaji dhidi ya mnyonge. Itakumbukwa wakati cwt inaanza walimu walikaririshwa kuwa mbiu ya mnyonge ni umoja lakini kwa hali itakavyokuwa ni kinyume chake.

Binafsi siuungi mkono benki hiyo na napendekeza uanzishwaji wa viccoba na saccos za walimu kama mbinu ya kuwakomboa walimu.

Lakini pili michango ya walimu kuanzia mwaka ambao benki itaanza ihesabiwe kama hisa ambazo watakuwa ni kama wamezinunua kulingana na makato ya kila mwezi na hili litawapatia walimu faida kwa kadiri ya hisa zao na hii si tu itawanufaisha walimu pia itawavutia watu wengine ama kuwa walimu au kupata fursa ya kuwa wanachama wa CWT.

Ahsanteni Nawasilisha.
Hapo kwenye red, wewe unasema unapinga benki halafu unapendekeza namna ya walimu kupata hisa kwenye benki hiyo hiyo unayoipinga. Tukueleweje?
 
Back
Top Bottom