Chama cha Ushirika kuiburuza Serikali ya Mkoa wa Mbeya Mahakamani

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Siku moja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Amos Makala,kupokonya ardhi yenye ukubwa wa zaidi ya hekta 5000 ya wawekezaji na kuwapatia wananchi wilayani Mbarali,Chama cha Ushirika na Masoko cha Luhanga Amcos ambacho wanachama wake zaidi ya 320 ndio wamiliki wa ardhi hiyo kimetangaza kuiburuza Serikali ya Mkoa wa Mbeya mahakamani kutokana na uamuzi huo.

Mwenyekiti wa chama cha Ushirika na Masoko cha Luhanga Amcos,Merikiori Bagule amesema kuwa uamuzi huo wa Serikali ya Mkoa wa mbeya sio wa haki kwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Amos Makalla hakuwahi kuwasilikiza,hivyo uongozi wa chama hicho unakusudia kwenda mahakamani kupinga uamuzi huo.

Katibu wa Luhanga Amcos,Steven Mwaigwisya amesema kuwa uamuzi huo wa Mkuu wa Mkoa kama utatekelezwa una athari kubwa kwa wananchi,kwa kuwa ardhi hiyo inategemewa na watu wengi kuliko idadi ya wafugaji wanaopigiwa chapuo kupewa ardhi hiyo.

Baadhi ya wanachama wa Luhanga Amcos wamedai kuwa kuporwa kwa ardhi hiyo kutoka mikononi mwao kutawaathiri wao,familia zao na taifa kwa ujumla.
.
 
Ndio faida ya mihemuko
 
Back
Top Bottom