Civilian Coin
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 2,305
- 4,379
Chama hicho kitaitwa:
ACA yaani Arena for Correcting Africa-Tanzania. Na pronunciation yake itakua AKA(ACA).
Chama hicho kipya kinatarajiwa kuwa na wadau makini tu kutoka makundi ya Wanaharakati mbalimbali hasa wale wenye nia ya dhati na Nchi yetu " Right and Responsibility".
Lengo kuu la ACA ni "Be trustful, Serve our Country" kiswahili chake ni "Kuwa mwaminifu, Tumikia Nchi yetu" kama Slogan ya chama. Hivyo kwa mawazo mapana na kuongeza nguvu, Tafadhali karibuni maana ndio tuko kwenye harakati za kuanza usajili.
Chama hakina ubaguzi, wafadhili mnakaribishwa bado mapema katika kipindi hiki cha awali.
Tunaimani Msajili wa Vyama vya Siasa hatatubania Bali atatumia haki ya Kikatiba kutupatia Usajili.
Wakati wao wanasema mtaanzishia wapi, sisi tunasema tutaanzishia hapahapa. Wakati wao wanasema pesa mtapata wapi, sisi tunasema Mungu anaishi milele.
Tupo hewani kwa ushauri: 0746 230 808
Deogratius Nalimi Kisandu.
23 Jan 2017.
.......................
SISI NI NANI ?
Wana ACA:
Sisi ni wadau na wanaharakati wa Maendeleo na Demokrasia ya kweli ya Kitanzania, tulio amua kwa dhamira ya dhati kuitumikia Nchi yetu kwa kurekebisha na kusahihisha Kasoro na Makosa ya Taifa na Afrika kwa ujumla ili kujenga Taifa Jipya lenye Fikra chanya mpya za Kimaendeleo.
Kupitia muasisi wetu Deogratius Nalimi Kisandu, tumeamua kuanzisha chama cha Siasa kwa lengo la kusahihisha makosa ya Taifa na Chama hicho kimepewa Jina la Arena for Correcting Africa-Tanzania, kwa kifupisho itasomeka kama ACA. Tafsiri rasmi ya jina hili ni Chama Cha Kusahihisha Kasoro na Makosa ya Taifa na Afrika kwa ujumla wake.
Kwa ujumla Chama hiki ni matokeo ya tafiti mbalimbali za kimaisha ya maisha halisi wanayoishi Watanzania zilizofanywa na muasisi Ndugu Deogratius Nalimi Kisandu pamoja na juhudi za wananchi wa Taifa la Tanzania na Afrika kwa ujumla katika kujisahihisha pale walipo kosea na kujikwaa kipindi cha Ukoloni(kabla ya Uhuru) na baada ya kupata Uhuru kutoka kwa mkoloni, na pia changamoto za kipindi hiki cha Ukoloni mamboleo kupitia Utandawazi.
IMANI YA Chama cha ACA.
Chama tunachokiunda tunataka kiwe chama chenye hadhi ya Kitaifa na Kimataifa katika kusimamia Utawala Bora katika shughuli zote za Umma kwa maslahi ya Taifa lote.
1. Jina la Chama litakuwa ni Arena for Correcting Africa-Tanzania, na kwa kifupi itasomwa ACA.
2. Makao Makuu ya Chama cha ACA yatakuwa Dodoma, na kutakuwa na Ofisi Kuu ya ACA Zanzibar na Ofisi ndogo ya Makao makuu Dar es Salaam.
3.Bendera ya ACA itakuwa na Rangi mbili, Nyeusi kuashiria Uafrika wetu ndani ya Utanzania wetu, na Nyeupe kuashiria Weledi, UTU, Uzalendo, Uadilifu na Amani kwa Taifa. Nembo ya chama itakuwa ni Muunganiko wa mikono miwili iliyoshikana viganja kuashiria Umoja wetu katika kulinda Haki na Wajibu wetu katika Rasilimali za Taifa.
......................
FALSAFA, ITIKADI na MADHUMUNI ya chama cha ACA.
Baada ya kupata usajili, chama cha Arena for Correcting Africa-Tanzania (ACA) kitaanza na maudhui haya:
1. ACA itakuwa chama cha Siasa kitakacho waleta Watanzania pamoja ili waweze kuitumikia Nchi yao kwa uzalendo na mshikamano.
2. ACA inatumia mfumo wa UJAMAA HURIA (Free Socialism) kama msingi wa nadharia katika maendeleo ya kisiasa.
3. ACA itakuwa ni chama kinachojali misingi ya Demokrasia ya kweli.
4. ACA itajishughulisha kufanyia kazi mambo mhimu kama kubuni ajira, viwango vya malipo, elimu, afya na Nishati.
5. ACA inapinga Ukabila, Ukanda na Udini na inapendekeza kuwepo na uvumilivu wa kiutamaduni.
6.ACA inajiandaa kushika mamlaka ya kuongoza Nchi kama serikali na pia itakuwa tayari kuwa na serikali ya umoja wa kitaifa pale itakapoona inafaa.
7. ACA itaandaa viongozi wake na wanachama wake katika kumiliki uchumi wa kujitegemea.
8. ACA inaamini Umoja na Ushirikiano ni bora zaidi kuliko migogoro, umoja ni bora zaidi kuliko mtengano na daraja ni bora zaidi kuliko Ukuta.
9. ACA imejikita zaidi katika kuinua vipato na kurekebisha Usalama wa Uchumi wa Nchi kwa wananchi wa kati na wale wa chini.
10. ACA itafanya maboresho ya mishahara kwa watumishi na haki zao, kulinda na kutetea haki za Uchumba na ndoaa na mirathi, haki za wanawake, watoto na walemavu, kutengeneza utu kwa wastaafu, kuunda na kurekebisha mfumo wa makosa ya jinai (Criminal Justice System), kupinga ushoga na usagaji, kuinua sanaa na utamaduni wa Taifa, kuheshimu makabila yote na kulinda haki ya mpiga kura.
11. ACA itajiongoza kwa mawazo ya wanachama wake na wafadhili wa chama.
12. ACA itakuwa chama cha Siasa kisicho fungamana na upande wowote wa vyama vya Siasa.
13. ACA itakuwa ni chuo cha kisiasa kwa maendeleo ya afya ya uchumi wa Taifa letu kumfanya mwanachama ajikwamue kimaisha na kile anachokipata.
14. ACA itaungana na Dunia yote kupinga mambo yote yanayoenda kinyume na haki za binadamu.
............................
MGAWANYO wa MADARAKA wa Chama cha ACA tarajiwa.
1. Ngazi kuu za Chama.
I) Mtemi Kiongozi wa Chama
ii) Katibu Mkuu Mtendaji wa Chama.
iii)Katibu Msemaji Mkuu wa Chama
iii)Mhazini wa Chama
iv)Boharia mkuu wa Chama
v)Mratibu Sera na utawala bora wa chama
v)Kampeni meneja Mkuu wa chama.
2. Ngazi za Jumuia za chama.
I) Jumuia ya Umoja wa Vijana wa chama cha ACA (UVACA)
ii)Jumuia ya Wanawake wa chama cha ACA (JUWACA).
iii) Jumuia ya Baraza la Wazee wa chama cha ACA (BAWACA).
iv)Jumuia ya Wanafunzi na Wanachuo walio masomoni: ACA Students Organisation (ACASO)
Huu ndio mfumo tarajiwa wa Uongozi ndani ya chama cha Arena for Correcting Africa-Tanzania (ACA) tarajiwa
-----
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA UANZISHWAJI WA CHAMA KIPYA CHA KISIASA KIITWACHO ARENA FOR CORRECTING AFRICA-TANZANIA (ACA).
Ndugu wanahabari na wadau wa maendeleo Tanzania, Salaam;
Kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwatakia Kheri ya mwaka mpya 2017, kwani huu mwaka ni mwaka Mtakatifu maana unaishia na namba 7, Mungu alipumzika kazi yake siku ya 7, Ombeni nanyi mtapewa, lakini sameheni mara 7 mara 70. Na mwaka huu mimi Deogratius Kisandu, nina timiza miaka 37. Mnamo tarehe 28.6.2017. Hivyo ni mwaka wa UTIMILIFU.
Ndgugu wanahabari, Tanzania ni moja ya Nchi zilizowahi kupata uhuru wake mapema sana kutoka mikononi mwa wakoloni, na pia ni Nchi ya kwanza afrika kuunda muunganiko wa nchi mbili kuwa Nchi moja, kwa kuunganisha Tanganyika na Zanzibar, yote haya yalifanyika ili kuendeleza umoja na undugu barani afrika. Tanzania ndio Nchi pekee iliyotoa ushawishi wa uanzishwaji wa jumuia ya afrika mashariki(EAC), lengo likiwa ni kuleta undugu ndani ya afrika mashariki. Lakini Pia Tanzania ndio Nchi mojawapo iliyoshiriki kumuunga mkono marehemu Gadafi aliyekuwa rais wa Libya katika wazo la kuunda Umoja wa Jumuia ya afrika(AU). Tanzania ina makabila zaidi 120 na wote tunaongea lugha moja ya Kiswahili kama kiunganishi cha undugu na umoja wetu.
Hivyo basi, sisi watanzania na mimi kwa niaba ya watanzania tumeamua kuunganisha Nchi yetu Tanzania yenye muunganiko wa nchi mbili kwa kuanzisha Chama kipya cha Kisiasa ambacho kitakidhi mahitaji ya watanzania. Chama hiki tumependekeza kuwa kitaitwa “ARENA FOR CORRECTING AFRICA-TANZANIA” na kwa kifupi kitaitwa “ACA” kwa matamshi ya Kiswahili itatamkwa hivi “AKA”.
ACA itakuwa ni chama kipya ndani ya kipindi hiki cha mwaka 2017, K-atiba iko mbioni kukamilika ila miongozo iko tayari na taratibu zingine za kiufundi zaidi. Tunatarajia kufika Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kabla ya March 2017 kwa lengo la kuanza hatua za usajili.
Hata hivyo, bado tunaendele kutafuta wadhamini wenye nia ya dhati ili kukamilisha zoezi hili la kuitumikia Tanzania yetu. Moja ya Yote Salaamu yetu na kauli mbiu yetu itakuwa “ BE TRUSTFUL, SERVE OUR COUNTRY” yaani kwa Kiswahili itatamkwa hivi “KUWA MWAMINIFU, TUMIKIA NCHI YETU”
Malengo makuu ya ACA nikuja kitofauti kabisa na vyama vingine vyote vya kisiasa ambavyo vinafanya siasa kwa lengo la kupata Ruzuku na wala si kwa lengo la kushika Dola. Lengo kuu la chama cha siasa ni kushika Dola. Na vyama vya upinzani vilivyopo havina mkakati wa kushika Dola na ndio maana wana malumbano kila kukicha, na hao wenzano CCM hata hawajui maana ya Dola na ndio maana Taifa limefika hapa kwa ukimya wa watu wema. Hivyo sisi tulio wema tumeamua kuungana na kuanzisha chama hiki ACA ili tuweze kufanya siasa za kisasa na zisizo na bughuza machoni mwa Watanzania.
Baada ya kupata usajili tutaanza kupanga safu zote kuanzia ma DC, RC na Wabunge watarajiwa kuelekea mwaka wa uchaguzi 2020. Tutafanya hivi bado mapema kama ambavyo vyama vikubwa Duniani ambavyo huwa vinafanya bado mapema ili kuweza kukabili hali ya uchaguzi kwa amani. Hatutakuwa na Ubaguzi wala rangi wala kabila wala dini wala jinsia, tutapiga kazi hasa, na hatutavumilia propaganda za kamati za ufundi, maana sisi tumezamilia kuitumikia Nchi yetu Tanzania na sio vinginevyo.
Taifa la Marekani lina vyama vingi vya kisiasa lakini vinavyoongoza kwa nguvu ni Democratic na Republican na kuonekana kama kuna vyama viwili lakini kiuhalisia vyama vipo zaidi ya viwili na hata uchaguzi wa majuzi vyama vilivyoshiriki vilikuwa vingi. Hivyo tunatarajia ACA kuwa chama kinachoongoza Tanzania(The leading Party), maana sisi tutakuwa wakitofauti.
Leo, nachukua jukumu la kuwa msemaji wa maandalizi ya chama kipya cha ACA kama Mwenyekiti wa Taifa Mteule wa ACA. Maarifa tunayo, hivyo hatuwezi kuangamia bali tutaangamiza wambeya wote wa kisiasa.
Sisi tutapokea makapi yote kutoka CCM na UKAWA mpaka WASALITI nao pia tutawapokea, maana tunajua fika hakuna aliye mkamilifu zaidi ya Mungu pekee, tutawajenga na kuwabadilisha na kuwa watu wema ndani ya ACA.
Mimi mwenyekiti na muanzilishi wa chama hiki cha ACA, nimewahi kuwa Katibu wa BAVICHA(Chadema) mkoa wa Tanga, Katibu mwenezi wa kitengo cha Vijana wa NCCR Mageuzi na Mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa wa Nccr mageuzi, na kwa mara ya mwisho nimekuwa mwanachama mtelekezwa wa CCM.
Ndugu wanahabari naomba mtufikishie Taarifa hii kwa Umma wa Tanzania.
Mawasiliano; 0746 230 808.
DEOGRATIUS NALIMI KISANDU
MWENYEKITI WA TAIFA MTEULE WA “ARENA FOR CORRECTING AFRICA-TANZANIA (ACA).”
23 JANUARI 2017