Ni muda mzuri kuwasikilizisha wana CCM jambo hili..kwa kifupi kabisa, siasa za Tanzania zimechukua sura mpya ya UHASAMA mara tu Stephen Wassira alivyokuwa Makamu Mwenyekiti CCM Taifa, uhasama ulikuwepo lkn si kwa kiwango hiki kilichopo sasa..
1. Maisha ya Wassira hayana fundisho lolote zuri kwa jamii ya watanzania, ukimsikiliza maneno yake ukalinganisha na umri wake unaona kuwa, Wassira hana wajibu wowote..km baba, km Mzee wa makamo, kama muumini wa imani/dhehebu fulani..yeye ana wajibu kwake mwenyewe na hivyo hana gharama yoyote kwa atakalolisema, kuagiza au kulitenda! Nadhani imeeleweka..
2. Kama litatokea jambo gumu kwa nchi kama zao la uhasama huu, Wassira ni sehemu ya matokeo hayo..waliompendekeza na hatimae kushawishi awe kwenye hiyo nafasi aliyo nayo sasa nao ni sehemu ya matokeo hayo japo wanajua sababu zilizopelekea kumuweka hapo ni kwa faida yao na si kwa CCM wala nchi kwa ujumla wake.
Hitimisho:
Itafaa sana viongozi wa dini wasio waoga wakae na Wassira kumsaidia arudi kwenye nafasi anayopaswa kuwa na hivyo kutenda sawia kwa ajili ya nchi. Si sahihi kabisa mtu wa umri wake kushabikia shari na kutokuelewana watu wa aina yoyote ile hata maadui zake..yeye alishavuka umri wa kufanya hivyo kwa mbali sana.
CCM watafakari tena na tena juu ya mwelekeo anawapeleka Wassira..hayo yakishindikana basi aliyeweka mipaka ya nchi hii na kuweka watu wake kwenye eneo hili yeye mwenyewe amsaidie Wassira ili nchi isifike kwenye magumu yatakayoifanya nchi iingie kwenye adha na mahangaiko makubwa isivyostahili km ataendelea kuwepo hapo walipomuweka..
Asante!