Chama cha ADC Chatangaza kushiriki uchaguzi Zanzibar.

pakaywatek

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
4,642
6,269
Hamad rashid mohamed amesema anamatumaini ya kushinda siyo kuwa makamu wa kwanza wa rais.
 
ccm wanavituko kweli haohao ni chama dola haohao ndio upinzani ukistaajabu ya hamad rashidi utayaona ya ccm
 
Hiyo ndio Demokrasia kamili....,sio unachotaka Wewe basi wote wafate mawazo yako!Hasa pale vyama vyenyewe vinapokosa msimamo wa kipi wanakipigania..!
 
Hamadi ata afanyaje hawezi ata kupata asilimia kumi yeye ajiongopee tu Na ccm Yake usaliti nimbaya sana
 
Hongera zao ADC kwa kukubali kuwa wasindikizaji siku ya uchaguzi......

For sure, I expect less response from voters supporting Ukawa......they already have a psychology torture...
 
Hivi ikitokea hamad akawa mshindi wa pili na akakosa wawakilishi serikali ya umoja wa kitaifa utakuaje? Hau ccm watamuazima wawakilishi ili kukidhi matakwa yao.
 
Fupisha tu,"Sema"Ccm wadhibitisha kushiri uchaguzi.
Sumaye aliwahi kusema hili kuwa miaka yote tangu vyama vingi viruhusiwe CCM imekua ikitawala huku yenyewe ndo ikijivika chama cha upinzani kwa kupandikiza watu kwenye hivyo vyama.
 
Sumaye aliwahi kusema hili kuwa miaka yote tangu vyama vingi viruhusiwe CCM imekua ikitawala huku yenyewe ndo ikijivika chama cha upinzani kwa kupandikiza watu kwenye hivyo vyama.
Hela ni shetani, unapewa hela tuu afu mambo yanaendelea kama kawaida....

Chukulia umeletewa 200milion afu uwe msindikizaji.....just take your afu uone kama utachomoa
 
Kule Somalia watu wa aina hii huwa ukijulikana tuu basi unakuwa historia
 
ITV habari imeonyesha video Hamad akihutubia. Kuficha aibu mpiga picha hajaonyesha picha ya "umati "iliyohudhuria mkutano wa Hamad. La kuvunda halina ubani.
 
Aibu kweli yule babu,halafu kuna kitu sijaelewa wamesema kampeni hakuna leo hao adc walikua wananadi nini kwa wananchi?ingekua cuf leo ingekuaje?
 
Hivi ikitokea hamad akawa mshindi wa pili na akakosa wawakilishi serikali ya umoja wa kitaifa utakuaje? Hau ccm watamuazima wawakilishi ili kukidhi matakwa yao.

Huyu si kavuliwa uwanachama au vipi? Kama ni hivyo katiba ya SUK inaeleza kwamba CHAMA kilichotokea wa pili (assuming masharti ya %ya kura yamekamilika) watapendekeza majina yasiyozidi matatu kwa Raisi ili mmoja wao achaguliwe kuwa Makamo wa kwanza wa raisi. Si lazima kuwemo jina la aliyeshiriki katika uchaguzi. Kwa maana hiyo ikiwa Hamad Rashid ameshiriki uchaguzi wakati si mwanachama tena wa ADC na ADC wamekubali kushiriki uchaguzi (Isipokuwa kutokana na masharti hawakuweza kubadili mgombea) wanaweza kupeleka majina mengine bila ya kuwemo la Hamad Rashid. Tamaa yake itamletea majuto.

Natabiri mfarakano mkubwa kwa vyama vilovyoamua kushiriki kwa sababu mbili.

1. Hakuna chama kitakachokamilisha masharti na kwa maana hiyo vyama vyote vitategemea kupindishwa sheria ili kipate uongozi, tatizo litakuja ni chama kipi kitachaguliwa wakati vyote havitatimiza masharti hapo ndipo matatizo yatakapoanza.

2. Ndani ya chama chenyewe nani awe makamo wa kwanza kukiwakilisha chama ni suala jengine. Considering kutakuwa hakuna nafasi ya uwaziri ambayo itatolewa kwa vile huo umakamo ni kwa kupindisha sheria tu.

Natabiri Serikali hiyo haramu kushirikisha vyama vyote viloshiriki ili kujaribu kuwaridhisha lakini uamuzi huo unaweza kuchukuwa miezi kadhaa kwa kujaribu ku- Jecha-rise the process. Let's wait and see
 
Hamad rashid mohamed amesema anamatumaini ya kushinda siyo kuwa makamu wa kwanza wa rais.
Pakaywatek,
Hizi ndizo starehe za Afrika.
Uchaguzi wa 2015 vyama vyote viunganishe bila CUF.

Havikuweza kupata 1% ya kura.
Mdomo haumkatai bwana wake.
 
You heard it straight from horse's mouth .A people's friend or foe? Guess you are now no longer in doubt.​
 
Back
Top Bottom