Magical power
JF-Expert Member
- Sep 27, 2022
- 2,455
- 6,465
ZAWADI: Kaka Magical Power, naomba ushauri tafadhali, usinipuuze 🙏
MAGICAL POWER: Sawa, sema dada. Upo salama?
ZAWADI: Sina amani kabisa. Mume wangu wa ndoa miezi mitatu, amebadilika ghafla. Hana mapenzi tena, hanigusi, halali nyumbani. Kila nikimuuliza anasema niko busy, mara kazini, mara kanisani.
MAGICAL POWER: Ulianza kuona mabadiliko lini?
ZAWADI: Ni kama wiki tatu sasa. Jana nimefuatilia kwa siri, nikagundua anaishi na mwanamke mwingine nyumba ya kupanga maeneo ya Kimara. Wamepanga kama wachumba, hadi wanashea vyombo vya ndani.
MAGICAL POWER: Subiri kidogo... Mume wako wa ndoa miezi mitatu?? 😳
ZAWADI: Ndio kaka, yaani tulivyofunga ndoa aliniahidi kila kitu. Nikauza biashara yangu nikahamia kwake. Sasa hata pesa ya matumizi hanipi. Napoishi nimebakia mtumishi asiye na mshahara wala heshima.
MAGICAL POWER: Sasa dada, unahitaji msaada wa nini? Maana hapo kuna mambo matatu: kiburi, uongo na usaliti wa kiwango cha juu.
ZAWADI: Nataka kujua, niendelee kuvumilia nikiamini ni mapito ya ndoa au nichukue hatua? Maana wazazi wangu hawajui kinachoendelea, bado wanamwona kama malaika.
MAGICAL POWER: Hapana dada, unateswa kimya kimya huku watu wakikushangilia. Hii si ndoa, ni mtego wa mateso. Uvumilivu usikufanye uendelee kuliwa maisha yako yote. Wape wazazi ukweli. Kama mwanaume hana heshima ya ndoa, basi si wa ndoa.
ZAWADI: Aisee… umenifungua akili. Nilihitaji kusikia haya. Ahsante kaka Magical Power.
MAGICAL POWER: Karibu sana. Kumbuka, usijifiche kwenye kivuli cha ndoa hadi ubaki kivuli cha mwanamke.