Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Maazimio hayo yalifikiwa juzi katika kikao maalumu cha baraza hilo kilichoketi wilayani hapa kwa ajili ya kupitisha bajeti yao ya mwaka wa fedha 2017 /2018
Kwa mujibu wa madiwani hao, daktari atakayekiuka utaratibu huo, hatua kali za kisheria zinachukuliwa dhidi yake. Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Said Zikatimu, alisema wagonjwa wengi katika Halmashauri yake wamekuwa wakitozwa Sh 40,000 za mafuta ili waweze kupata huduma ya gari la wagonjwa jambo ambalo si sahihi
"Kuanzia sasa, tabia hiyo imepigwa marufuku na mgonjwa yeyote anayepewa rufaa au kuhitaji gari la wagonjwa, atapelekwa bure na gharama zote zitalipwa na Halmashauri. "Wananchi wa Chalinze walikuwa wakipata kero kubwa juu ya kupata huduma ya gari la wagonjwa, walikuwa wakitozwa fedha nyingi bila sababu za msingi", alisema Zikatimu
Naye Diwani wa Kata ya Kibindu, Ramadhani Mkufya (CCM), alisema kero hiyo ilikuwa kubwa kiasi ambacho ilikuwa inawanyima haki ya kupata huduma ya afya wananchi masikini wasiokuwa na uwezo wa kutoa fedha hizo.
Chanzo: Mtanzania