Chakula kama dawa

smartdunia

Member
Jul 29, 2021
12
9
Imeandikwa Na Smartdunia.

Utasikia "biashara ya dawa inalipa kwasababu magonjwa yapo kila siku".

Mara utasikia,"ukijisikia vibaya nenda haraka kamuone daktari usije ukachelewa".

Tena utasikia,"Yupo mtumishi wa mungu ambae hakuna tatizo linaloshindikana kwake,nenda haraka ndugu yangu".

Hayo yote ,kama umewahi kuyafanya au utayafanya ni sahihi,tena kwa asilimia tisini na tisa,lakini bado Kuna haja ya kufahamishana kwamba hiyo asilimia moja iliyobaki ni kwa ajili ya nini,ina faida gani na isipozingatiwa hasara zake ni zipi?.

Kiufupi kuna haja ya kufanya kazi ndogo na rahisi ya kuziba ufa ili kuepuka kazi ngumu sana ya kujenga ukuta.

Ni Ukweli usiopingika ya kwamba,katika karne hii,binadamu wengi tumehamisha imani yetu na kuwaamini madaktari na wachungaji kuliko chochote juu ya miili na afya zetu,tumeshasahau kwamba madaktari na wachungaji namba moja ni sisi wenyewe.

Ni jambo la kusikitisha sana pale tunaposhindwa kujua kwamba,asilimia kubwa ya matatizo tulionayo leo,chanzo kikubwa ni kukosa maarifa juu umuhimu wa matumizi ya chakula kama dawa.

Wengi wetu hua tunakula ili mradi tushibe au tufurahishe ndimi zetu na kusahau kwamba chakula ni dawa namba moja kikitumika ipasavyo.

Mwandishi mmoja aliwahi kusema,"usipokula chakula kama dawa ipo siku utalazimika kumeza dawa kama chakula".

Mwandishi mwingine nae akasema,

"You are what you eat",akimaanisha mwili wa kila mwanadamu au kiumbe yeyote umeundwa kwa kile unachokula kila siku.

Utakuta mtu anahangaika kutafuta lishe Bora kwa ajili ya mifugo yake kama kuku na ng'ombe, ili ikue kwa afya apate maziwa na mayai mengi kwa ajili ya kipato, anasahau kabisa kwamba hata yeye mwenyewe anahitaji lishe Bora zaidi ya hata hiyo mifugo yake.

Leo hii matatizo ya uzazi,nguvu za kiume, Lovu,kisukari na vidonda vya tumbo ni machache kati ya mengi yanayotesa watu,na kuwafanya wapishane kwa madaktari na wachungaji tena bila mafanikio na wengi huishia kupata tulizo la muda tu,yote ni kwa sababu tumesahau kuziba ufa na kukumbuka kujenga ukuta ambao hatuwezi kuumudu.

Tunachopaswa kukijua ni kwamba,binadamu wote tumeumbwa tukiwa na ugonjwa usiotibika yaani njaa,madaktari wa ugonjwa huo ni sisi wenyewe,ugonjwa huu dawa yake ambayo ni chakula tunachokula kila siku,husaidia kuutuliza tu na sio kuutibu,dozi yake ni kutwa mara tatu,ikitumika ipasavyo inasaidia kuzuia magonjwa mengine mengi mno.

Hivyo basi,kabla hujafikia hatua ya kutumia vizuri dozi ya daktari,hakikisha unatumia ipasavyo dozi ya chakula ambayo ni dhahiri utakua umeiandaa mwenyewe.

Ili kufanikisha hili inatupasa tujitolee kujifunza Kuhusu mpangilio wa lishe Bora ili kulinda afya zetu wenyewe kwani hiyo ndio hatua ya kwanza ya ulinzi wa afya zetu.,kuenda duka la madawa kununua dawa au hospitalini ni hatua ya mwisho,haipendezi kufikia hatua ya mwisho bila kuipitia hatua ya kwanza ambayo ni nzuri na rahisi zaidi.

NB;Tusisahau kufanya mazoezi walau mara moja kila wiki,kujikinga na Corona pamoja na Ukimwi.

images%20(1).jpg
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom