Chakachua ya ardhi yakolea wilaya ya Kisarawe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chakachua ya ardhi yakolea wilaya ya Kisarawe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kabwela, Aug 23, 2010.

 1. Kabwela

  Kabwela Member

  #1
  Aug 23, 2010
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Salam ndugu Watanzania wenzangu

  Ningependa kuwaajuvya kuwa chakachua kwenye masuala ya ardhi imeanza kuoamba moto katika wilaya ya kisarawe hasa baada ya thamani ya ardhi kuanza kuongezeka.

  Hilo lathibitika baada ya muwekezaji mwenye asili ya Israel aitwaye Shallom kupewa eneo la ardhi ya mtaa wa relini, kitongoji cha makurunge, kijiji kiluvya A mwaka 1999 wakati baadhi ya wanavijiji waliokuwa wamiliki wa maeneo hayo kutofidiwa. Muwekezaji huyo hakufanya shughuli zozote za maendeleo kwa muda wote huo mpaka mwaka huu (2010) kuanza kuwatumia afisa maendeleo wa wilaya ya kisarawe na mtendaji mmoja wa halmashauri ya kijiji kuwanza kuweka mabango mpaka maeneo mengine ambayo hayakuwa yakimilikiwa na muwekezaji huyo.

  Baada ya mwekezaji huyo kupewa eneo hilo, wanavijiji wakawa wanauza maeneo mengine ambayo hayakuwa yakimilikiwa na muwekezaji huyo na yakawa yanasajiliwa kupitia serikali ya kijiji cha kiluvya A ambacho kinashiriki kubandika mabango ya kuonesha hata maeneo ambayo si ya muwekezaji huyo kwani hata mipaka yake haifahamu vizuri.


  [​IMG]
  Bango lililowekwa hivi karibuni na mtendaji wa halmashauri ya kijiji cha kiluvya A kuhalalisha ukamataji wa wanavijiji


  Wakati hayo yakiendelea afisa maendeleo ya wilaya na muhusika wa halmashauri ya kijiji hicho imeshakamata mwanakijiji mmoja na kumfungulia kesi ya kuvamia eneo la muwekezaji huyo wakati yupo nje ya eneo la muwekezaji huyo na alikuwepo akiishi hapo kabla muwekezaji huyo hajapewa eneo hilo. Wakati kesi ya huyo mwanakiji inatajwa kwenye mahaka ya wilaya ya kisarawe leo jumatatu, kuna mwanakijiji mwingine amepigiwa simu na askari polisi aripoti kwenye kituo cha polisi siku ya jana (jumapili) saa tano asubuhi.

  Wanavijiji hao wameamua kuungana na kumuomba mwenyekiti wa mtaa kuandika barua kushinikiza ofisi ya kata kuingili kati suala hilo wakati nakala za barua hizo zikiopelekwa kituo cha polisi kisarawe, mkuu wa wilaya, mkurugenzi wa wilaya na ofisi ya kijiji.

  Nitaendelea kuwajuvya yanyoendelea kadri mambo yanavyoendelea kufunguka.
   
 2. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Duh! Asante kwa taarifa! Hivi lile sakata la Wasanii na Waandishi wa habari la VISEGESE na Mkuranga limeishia wapi? Hii tia maji tia maji tutashtukia hatuna chetu... Hao hao wanakijiji wakienda kupiga kura wanawachagua hao hao wanaowapora ardhi yao...
   
Loading...