Chaguzi ndogo zinaimarisha Chadema

Chaguzi ndogo zinaimarisha Chadema

rosemarie

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2011
Posts
6,887
Reaction score
3,439
Wakuu tupo Kalenga na tumeshangazwa jinsi watu wa jimbo hili walivyoamka na kuelewa mambo,nimemsikia kijana mdogo sana akimtania mwenzake,hivi huyu mume wa mzungu akichaguliwa atamleta mzungu huku kijijini?hilo ni swali la msingi na gumu sana kulijibu,tumeona jinsi makamanda wa Chadema wanavyofanya kazi kwa nguvu zote na kuungwa mkono na wananchi wa Kalenga
tumeshuhudia Ktibu Mkuu akifungua matawi na kuhakikisha viongozi wa matawi wanapatikana,kwa kweli ni kazi ngumu lakini inasaidia sana kuimarisha chama
cha kufanya ni kusubiri fisadi lingine life tupate nafasi nzuri ya kwenda kuimarisha chama kitongoji baada ya kitongoji!!!
 
Eti fisadi lingine life,nimecheka,ebu ngoja kwanza tusubiri matokeo ya kura za kumchagua mwenyekiti wa bunge maalumu la katiba....kila la kheri kwa samwel sita maana ndiyo mtu pekee anaweza kwenda sawa na bunge hili japo sio wa kumuani sana huyu ila bora yeye kuliko wengine walau anajua maana ya utu.

Kila la kheri kwa chadema na timu yote hapo kalenga
 
Kalenga, Mungu saidia tu CDM ishinde, hii ni kete kali. Najua Chalinze ni mteremko.
 
Kweli Mwenyezi Mungu akipenda atupunguzie idadi ya mafisadi,achukue mafisadi papa kama matano tuu kabla ya uchaguzi mkuu mwakani
 
Kweli Mwenyezi Mungu akipenda atupunguzie idadi ya mafisadi,achukue mafisadi papa kama matano tuu kabla ya uchaguzi mkuu mwakani

Hata mimi nitafurahi sana. Leo kidogo nifunge kituo cha afya nikiwa kwenye supervision, kwa huruma nimekiacha. Naichukia CCM sana na siipendi kabisa, na kwakuwa ni soldier natamani waasi watokee ili niwaunge mkono haraka ili tuwatoe wadhalimu madarakani.
 
Wanakalenga tuondoleeni takataka hiyo, irudi kwa mke wake uingereza, mkikosea hatamuona jimboni huyo, shauri yenu, maisha yake yatakuwa Dar na uingereza.
 
Kikwete alifikiri chalinze ni mali yake?atashangaa matokeo

Haa msinambie.... ya kweli hayo? mwana wa mfalme aweza kuangushwa? Itabidi liwe swala la kifamilia zaidi, mkuu mwenyewe atashuka ulingoni kuokoa jahazi!
 
sio kila aliye vaha nguo ya ccm lazima awe muokota makopo,
wengine ni njaa tu inawasumbua,ndiyomaana asilimia kubwa akili zao wamezipiga pini,
hila zao ndiyo zinazowafanya waendelehe kutawala lakini akika tumewachoka sana hao wezi.
 
Back
Top Bottom