Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,068
- 151,315
Utawala wa Magufuli,tofauti na ule wa Kikwete,unagusa moja kwa moja maisha ya mtanzania wa kawaida kijamii na hasa kiuchumi.Miezi 8 ya Magufuli kuwa madarakani imeathiri sana uchumi wa mtu mmoja mmoja ukiachilia mbali madhara ya kijamii ya zoezi la bomoabomoa,kufukuza wanafunzi wa UDOM na mambo mengine mengi kama kuzuia Bunge live n.k.
Ni kweli kabisa vitendo viovu vya ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka vilishamiri sana katika utawala wa awamu iliyopita ila ni kweli pia vitendo hivyo havikumgusa mwananchi wa kawaida moja kwa moja japo vilikuwa na madhara kitaifa hivyo havikuweza ku-influence maanuzi ya wapiga kura wengi kutokana na wengi wao kuwa na uelewa mdogo na zaidi wengi walimudu walau kupata mkate wa siku na maisha yakaenda japo yalikuwa magumu ila awamu hii ugumu huo unaweza kuongezeka kiasi cha kumzindua mwananchi hata ajue thamani ya kura yake katika kuchagua kiongozi/viongozi.
Awamu hii hali ni tofauti na kila kukicha ni afadhali ya jana. Wafanyabiashara wanalia, wakulima wanalia na wafanyakazi wa umma ndio kabisa hali yao ni "mahamumu".
Hivyo basi,hasira na machungu waliyonayo wananchi hawa yatajidhihirisha katika chaguzi ndogo zijazo(kama zitakuwepo) na katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
Dhana ya utumbuaji majibu haiwezi kuibeba CCM kwani ina mapungufu mengi kiasi kwamba wapinzania wakijipanga na kuichambua vizuri majukwaani,karata hii kwa CCM haitolipa bali inaweza kuwamaliza.
Hata Bajeti ya serikali ya 2016/2017, inaweza kabisa kuchangia anguko la CCM katika chaguzi zijazo.
Tusubiri.