Chaguzi ndogo na uchaguzi wa serikali za mitaa CCM itapata anguko la kihistoria

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,888
143,985
Utawala wa Magufuli,tofauti na ule wa Kikwete,unagusa moja kwa moja maisha ya mtanzania wa kawaida kijamii na hasa kiuchumi.Miezi 8 ya Magufuli kuwa madarakani imeathiri sana uchumi wa mtu mmoja mmoja ukiachilia mbali madhara ya kijamii ya zoezi la bomoabomoa,kufukuza wanafunzi wa UDOM na mambo mengine mengi kama kuzuia Bunge live n.k.

Ni kweli kabisa vitendo viovu vya ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka vilishamiri sana katika utawala wa awamu iliyopita ila ni kweli pia vitendo hivyo havikumgusa mwananchi wa kawaida moja kwa moja japo vilikuwa na madhara kitaifa hivyo havikuweza ku-influence maanuzi ya wapiga kura wengi kutokana na wengi wao kuwa na uelewa mdogo na zaidi wengi walimudu walau kupata mkate wa siku na maisha yakaenda japo yalikuwa magumu ila awamu hii ugumu huo unaweza kuongezeka kiasi cha kumzindua mwananchi hata ajue thamani ya kura yake katika kuchagua kiongozi/viongozi.

Awamu hii hali ni tofauti na kila kukicha ni afadhali ya jana. Wafanyabiashara wanalia, wakulima wanalia na wafanyakazi wa umma ndio kabisa hali yao ni "mahamumu".

Hivyo basi,hasira na machungu waliyonayo wananchi hawa yatajidhihirisha katika chaguzi ndogo zijazo(kama zitakuwepo) na katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Dhana ya utumbuaji majibu haiwezi kuibeba CCM kwani ina mapungufu mengi kiasi kwamba wapinzania wakijipanga na kuichambua vizuri majukwaani,karata hii kwa CCM haitolipa bali inaweza kuwamaliza.

Hata Bajeti ya serikali ya 2016/2017, inaweza kabisa kuchangia anguko la CCM katika chaguzi zijazo.

Tusubiri.
 
Uko sahihi, utawala huu unaujuzi mkubwa wa kubomoa, kujenga mwisho uteuzi na maelekezo kuwa mkachape kazi, wakienda kwenye viwanja vya kazi ni kufukuzana tu hakuna cha maana,
Kwa mfano:-
Badala ya kuwafanya wahandisi kusimamia wakandarasi wafanye kazi zenye viwango vilivyokubaliwa kwenye BOQ wanaanza kutimua wakandarasi waliopo kisheria.

Wamekuwa washtuaji kama joti, sukari imewaumbua!!!!
Tulia amewafedhehesha
Itafika wakati watumishi maofisini watasubiri mwongozo kutoka magogoni uwafikie ndio wabebe mafaili, kijijini ndio wakulima wakalime, kwenye maduka ndio wafungue viduka vyao.

Hali ni mbaya mungu atunusuru.
 
kweli BAVICHA, hamna kiongozi, KUB inaogopa hadi kivuli cha Dr Tulia, sasa eti wanampinga mdada tu kawashinda, hoja ya bunge live, kugoma ndo iwatoe CCM, bado sanaaaaa
 
Kipimo cha kwanza kuhusu kuanguka kwa chama cha baba Je.sca ni uchaguzi mdogo wa mbunge wa Longido. MaCCM lazima yakae.
Mungu ni mwema , hatimaye amefungua njia ya kuichamba na kuichambua serikali hii kupitia chaguzi ndogo ikiwami jimbo LA longdo. Hapo sasa
 
kweli BAVICHA, hamna kiongozi, KUB inaogopa hadi kivuli cha Dr Tulia, sasa eti wanampinga mdada tu kawashinda, hoja ya bunge live, kugoma ndo iwatoe CCM, bado sanaaaaa
Aliyeshindwa ni Tulia au nani unavyojua wewe? MTU kama anakiuka kanuni kichwan mwako anafanya sahihi au sio?
 
kweli BAVICHA, hamna kiongozi, KUB inaogopa hadi kivuli cha Dr Tulia, sasa eti wanampinga mdada tu kawashinda, hoja ya bunge live, kugoma ndo iwatoe CCM, bado sanaaaaa

Vijana wa lumumba kwanini mnakimbilia matusi jibu hoja,,,mtoa mada huko sahihi kabisa utawala wa awamu hii hali ya mtaani ni ngumu kwa kila mtu vitu vimepanda bei sukari juu,mafuta ya kula juu,chumvi juu,sabuni ya unga kipande juu,vinywaji ndo hivyo vinakuja mwezi ujao mihamala ya simu nayo uwiiii makato,,,kila kitu juuu uchaguzi wowote ukija watapokea za uso hawataamini macho yao!!!
 
Nyıe watu nadhanı mna akili kidogo sana, jishughulishe vingnevyo mtakufa masikini.Mbowe wala Lisu hawana umasikini km wenu!
 
Utawala wa Magufuli,tofauti na ule wa Kikwete,unagusa moja kwa moja maisha ya mtanzania wa kawaida kijamii na hasa kiuchumi.Miezi 8 ya Magufuli kuwa madarakani imeathiri sana uchumi wa mtu mmoja mmoja ukiachilia mbali madhara ya kijamii ya zoezi la bomoabomoa,kufukuza wanafunzi wa UDOM na mambo mengine mengi kama kuzuia Bunge live n.k.

Ni kweli kabisa vitendo viovu vya ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka vilishamiri sana katika utawala wa awamu iliyopita ila ni kweli pia vitendo hivyo havikumgusa mwananchi wa kawaida moja kwa moja japo vilikuwa na madhara kitaifa hivyo havikuweza ku-influence maanuzi ya wapiga kura wengi kutokana na wengi wao kuwa na uelewa mdogo na zaidi wengi walimudu walau kupata mkate wa siku na maisha yakaenda japo yalikuwa magumu ila awamu hii ugumu huo unaweza kuongezeka kiasi cha kumzindua mwananchi hata ajue thamani ya kura yake katika kuchagua kiongozi/viongozi.

Awamu hii hali ni tofauti na kila kukicha ni afadhali ya jana. Wafanyabiashara wanalia, wakulima wanalia na wafanyakazi wa umma ndio kabisa hali yao ni "mahamumu".

Hivyo basi,hasira na machungu waliyonayo wananchi hawa yatajidhihirisha katika chaguzi ndogo zijazo(kama zitakuwepo) na katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Dhana ya utumbuaji majibu haiwezi kuibeba CCM kwani ina mapungufu mengi kiasi kwamba wapinzania wakijipanga na kuichambua vizuri majukwaani,karata hii kwa CCM haitolipa bali inaweza kuwamaliza.

Hata Bajeti ya serikali ya 2016/2017, inaweza kabisa kuchangia anguko la CCM katika chaguzi zijazo.

Tusubiri.
CC: Molemo
 
Iwapo tu makaratasi "kura" za wananchi zitaheshimiwa. Kinyume chake,Jecha hajastaafu bado...
 
kweli BAVICHA, hamna kiongozi, KUB inaogopa hadi kivuli cha Dr Tulia, sasa eti wanampinga mdada tu kawashinda, hoja ya bunge live, kugoma ndo iwatoe CCM, bado sanaaaaa
Nliwahi kusikia ila sijathibitisha ni kua vijana wa lumumba wengi wao ma bwabwa ndo maana hawaogopi kutukana
 
Watapigwa sana awamu hii. Wananchi wameshachoshwa na hiki chama cha dikteta uchwara. Maisha yamekuwa magumu hata wana Geita wameanza kumkataa ndugu yao (baba Jes.ca a.k.a dikteta uchwara) na chama chake.
 
mitumba itakapokoma kuingia na mbadala hamna, hee mafundi cherehani watapata kazi ya nyongeza kuweka viraka, mafundi viatu nao watafaidi kiana. tujipange tu!
 
MPIGA wa kawaida kama hana maisha mazuri tu ya kumpatia mlo wa uhakika hawezi kukipigia kura.Wananchi wanahitaji uchumi wao binafsi kwanza uwe mzuri.Ajira nyingi,washibe kwanza ndiyo watoe kura.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom