TAECOLTD
JF-Expert Member
- Mar 2, 2013
- 1,051
- 1,835
Habari za muda ndugu zangu,
Bila shaka mu bukheri wa afya, leo ningependa tugusie kuhusu machaguo tuyafanyayo katika maisha yetu. Watu waliofanikiwa kuzifikia ndoto zao walikaa chini na kufikiri ni jambo gani sahihi wawezalo kufanya na kufikia mafanikio yao maishani, somo lililopita niligusia kuhusu talanta. Baada ya kujiridhisha hiyo ndio talanta yako na kuifanyia kazi ipasavyo ndio barabara sahihi ya kukufikisha mbali.
Watu wengi hufananisha chaguo sahihi kwa kile walichokisomea chuo labda kama alisomea business huisi ndio talanta yake sahihi, la hasha kuna watu walisomea engineering lakini leo ni wanamuziki wakubwa tu. Wengi wetu tumeishia kuteseka na kazi tuzifanyazo lakini hazikuwa talanta zetu au hatukufanya chaguo sahihi na ndio sababu tunateseka mpaka tunaingia kaburini.
Linapokuja swala la chaguo ndio huvuruga maisha ya mtu kabisa, hapa kuna mambo mawili;
1) Chaguo la mtu binafsi
2) Chaguo la wazazi
Wengi tumeishi katika familia ambazo wazazi wetu ndio hutuchagulia nini cha kufanya katika maisha yetu na machaguo hayo ndio yameharibia maisha ya watu kabisa. Kuna watu walichaguliwa na wazazi wao kuwa waalimu lakini mbeleni wakabaini halikuwa chaguo sahihi ndipo wakabaini chaguo sahihi na kulifanyia kazi na hatimaye kufanikiwa. Tunaishi katika ulimwengu wa utandawazi hivyo watu hujiamulia kufanya jambo wakiamini ndio chaguo sahihi kisa wamemuona fulani amefanya nao hufanya na kuishia kwenye mateso.
Kuna kauli watu huitumia sana 'role modal' sababu kamuona Flaviana Matata ameng'aa basi naye hukurupuka kufanya hivyo kwa kumuangalia huyo hatimaye kupotea. Lazima utambue kipawa chako kipo wapi baada ya kukibaini ndipo utafute ambao wamefanya hivyo ndio uwaweke role modal wako.
Rejea kwa Vanessa Mdee alichosomea na anachokifanya ni tofauti, alitambua alichosomea halikuwa chaguo sahihi ndio maana akagundua chaguo lake na sasa yupo mbali. Kuna Nahreel na wengine kazi ni juu yako kwenye kufanya chaguo sahihi ambalo hutajuta maisha yako yote badala yake utafurahia maisha yako yote.
Binafsi chaguo langu na talanta yangu imeangukia kwenye uandishi wa vitabu kitu ambacho hata sikusomea lakini nilibaini ndio chaguo langu na nalifanyia kazi na ninafurahi sana kufanyia kazi kipawa changu, je wewe umeshabaini chaguo lako sahihi na unalifurahia kutoka moyoni?! Jambo lolote ambalo unalifurahia toka moyoni pasi kusukumwa ni lazima likufikishe kwenye mafanikio sababu utalifanya kwa moyo wote.
Sasa endelea kuteseka na kazi za watu na kutimiza chaguo la mtu mwingine, maamuzi yapo mikononi mwako ama uendelee hivyo au ukae chini na kujitafakari upya.
Niwatakie siku njema yenye baraka tele.
Mtenga Gerald
TAECO LTD
TANZANIA