Chagueni watu sio vyama.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chagueni watu sio vyama....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Njowepo, Aug 27, 2010.

 1. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #1
  Aug 27, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  na Grace Macha, Moshi

  UMOJA ya Makanisa ya Kikristo mkoani Kilimanjaro, umetoa waraka unaowataka wananchi kuchagua viongozi bora, huku wakisisitiza umuhimu wa kuchagua watu badala ya vyama vilivyowasimamisha.

  Waraka huo ni mwongozo wa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu na umesainiwa na Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Moshi, Isaack Amani, Dk. Martin Shao wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini (KKKT) na Glorius Shoo wa Kanisa la Tanzania Assembies Of God (TAG) .

  Waraka huo ambao Tanzania Daima ina nakala yake, ulianza kusambazwa juzi kwenye makanisa yote huku ukiwahimiza waumini wao kuona umuhimu wa kudumisha amani na upendo hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
  "Mtu yeyote mwenye sifa ya uongozi achaguliwe bila kuangalia yeye anatoka dini gani au kabila fulani ama sehemu anayotokea ama chama chake," unasomeka sehemu ya waraka huo.

  Maaskofu hao wamewataka wananchi kuepuka vitendo vya rushwa kwa kile walichosema kuwa mbali na kuwa hufunika ukweli na kuwakosesha haki wengine lakini pia ni dhambi kwa Mwenyezi Mungu.

  Aidha viongozi hao wa dini walihimiza jamii kuona umuhimu wa kujitokeza na kuwa waangalifu katika kuweka mawakala waaminifu watakaosimamia zoezi la upigaji na kuhesabu kura ili haki itendeke.

  Waraka huo pia unaeleza umuhimu wa wananchi kushiriki mikutano ya kampeni ya wagombea mbalimbali, jambo litakalowawezesha kuwapima na kujua uwezo wao na uchungu walionao katika kuwakomboa kutoka katika umaskini unaowakabili.

  MY TAKE
  Ni muda mwafaka kwa watazania kuchagua watu with proven records za utendaji wao waweze endeleza mazuri ya nchi yetu.This should be at all levels ie uraisi,ubunge na udiwani to mention but a few Mwakyembe,Magufuri,Dr Slaa etc
   
 2. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #2
  Aug 27, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,939
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  CCM wana bango linasema 'chagua CCM, chagua Kikwete', baadhi ya viongozi wa dini wanasema "chagua mtu na sio chama". Sasa hapa nani yuko sahihi? Kwanza chama halafu mtu au mtu halafu chama?
   
 3. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #3
  Aug 27, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama wewe ni independent kama mimi basi ni chagua mtu na sio chama!

  YES WE CAN
   
 4. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #4
  Aug 27, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  chagua mtu hata kama si wa chama chako ikiwa huyo mtu anafaa kuongoza. Kuwa memba wa chama fulani kusikulazimishe umchague mtu wa chama chako hata kama hafai.
   
 5. M

  Msharika JF-Expert Member

  #5
  Aug 27, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  ninaunga mkono kabisa kuchagua mtu na siyo chama, Mfano ni ushindi wa OBAMA , kura zilitoka vyama vyote na alizipata kwasababu alionyesha kuwa chachu ya maendeleo.
   
 6. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #6
  Aug 27, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  huyo mtu mnaetaka kumchagua anaenda kutekeleza sera zipi? Does not make sense. Sijui mawazo ya kijima hayo! agh tutaona kila aina ya utumbo humu
   
 7. Xuma

  Xuma JF-Expert Member

  #7
  Aug 27, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 631
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  MY TAKE
  Ni muda mwafaka kwa watazania kuchagua watu with proven records za utendaji wao waweze endeleza mazuri ya nchi yetu.This should be at all levels ie uraisi,ubunge na udiwani to mention but a few Mwakyembe,Magufuri,Dr Slaa etc

  sawa lakini magufuri inabidi tumuangalia pia sura yake ya pili. kwani ni mambo mengi aliyosimamia yalienda mrama, uuzwaji nyumba za seikari, utoaji tenda kwa wachina ambao walikuwa hawana uwezo wa kuhimili ukubwa wa tenda husika upindishwaji wa barabara ya Geita Bihaharamulo kuwa Geita Chato to mention but a few
   
 8. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #8
  Aug 27, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Sera zipo nzuri ajabu LAKINI hazitekelezeki.
   
 9. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #9
  Aug 27, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Mwone huyu naye! Sijui anaongea nini huyu! Kitu gani usichokielewa juu ya kuchagua mtu na si chama. Acha pumba hizo wewe!
   
Loading...