Weka muda special kwa ajili ya mamaaaa na muda special kwa ajili ya JF, mfano mzuri ni mimi mwenyewe huwa nipo JF kama sina kipindi (nafundisha chuo kikuu fulani) Pia kama nipo busy huwa naiweka JF pembeni hadi nimalize lakini kabla ya kulala lazima niangalie leo kulikuwa na nini na kuchangia kidogo na kulala kwa ajili ya kesho kuwahi tena kazini. Hayo ndio maisha yangu kwa muda huu.
Okoa ndoa yako mkuu, mpe nafasi yake mkeo, msikilize kwani ana umuhimu pia katika maisha yako usiwasahau na watoto pia kama unao.
Pia mshawishi mkeo nae ajiunge huku JF ili aamini na aone ya kuwa hamna vitu vibaya unavyofanya huku JF.