Chagua jambo moja na kufanya kitu kimoja kwa ufanisi zaidi

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,353
2,220
CHAGUA JAMBO MOJA ILI USIPOTEZE MUDA NA KUFANYA KITU KIMOJA KWA UFANISI ZAIDI

Kama unataka kujua watu wanaopoteza muda kwenye maisha yao, wakidhani ya kwamba wanaokoa muda, ni watu ambao wanataka kufanya vitu viwili, kwa wakati mmoja na wanavifanyia sehemu moja. Ni rahisi sana ukifikiria juu juu kwamba unaokoa muda. Lakini ukweli ni kwamba unapoteza muda mwingi sana.

Huwezi kuwa mtu mwema na mtu asiye mwema kwa wakati mmoja. Huwezi kuwa na imani mbili zinazopinga na kwa wakati mmoja. Ni lazima kwa wakati fulani utakuwa kwenye hali fulani moja kati ya hizo mbili. Usijidanganye kwamba uko kati kati, maana hapo hakuna chochote unachopata zaidi ya kupoteza muda.

Akili yako ina uwezo mkubwa sana wa kufanya kitu chochote, lakini kama akili hii itapewa uwezo w akuweza kufikiri na kufanya kitu kimoja kwa wakati. Hapa akili hii inapeleka rasilimali zote muhimu katika kushughulikia tatizo lililopo mbele yako na kuhakikisha unapata ufumbuzi.

Hapo ni kufanya kitu kimoja kwa wakati, unatumia muda mchache na unafanya kwa usahihi, tofauti na kama ungefanya zaidi ya kitu kimoja kwa wakati. Pale akili yako inapokazana kuhamisha mawazo kutoka kwenye kitu kimoja kwenda kwenye kingine, unapoteza muda mwingi sana. Ni bora zaidi kufanya kila kimoja kwa wakati wake.
 
Hili la kuwa neutral side ni unafiki haiwezekani mtu akose u pande kuhusu kufanya jambo moja kwa waqt ni sahihi wahenga wanasema mshika mawili moja litamponyoka au karamu mbili zilimshinda fisi.
 
Back
Top Bottom