Chagonja na sinema ya mwaka!

Inshu Ya Magaidi Ya Amboni, Imeishia Wapi? Ulitangazwa Unaenzwa Na Mmbu Wa Mchana Na Kuwa Tishio Kwa Taifa Umeisha Wapi? Chenji Za Rada Zimeishia Wapi? Wale Wahindi Wa Kaliakoo Waliokamatwa Kwa Ajili Ya Epa Wako Wapi? Zile Siku Tisini Za Kuvua Magamba, Bado Hazijaisha? Likizo Ya Jobu Ndugai Ni Ya Mda Gani? Najiuliza Sipati Jibu.
 
Nami sipati jibu kulikoni Lowassa aliyechafuka kuhusiana na Richmond,mpaka wakataka kumvua gamba ikiashindikana leo akageuka Lulu kwa Viongozi baadhi wa dini na wanafunzi kwa kile kinachodaiwa ana maamuzi magumu
 
Tanzania ni nchi yenye maajabu ya kipekee.Mojawapo ni hili la serikali yake kukosa uongozi thabiti na nchi inajisogeza na kujiongoza yenyewe,mithili ya ndege isiyo na rubani!
 

Badala ya kukaa na kudhani, isaidie serikali kupambana na maovu yanayopangwa na wahuni wachache wasioitakia mema nchi hii.
Hizo assumptions hazisaidii kwa sababu siku utakapokuja kugundua kuwa serikali haijihusishi na upuuzi kama huo, unaweza kuwa umechelewa wakati pengine mchango wako ungesaidia endapo ungeutoa mapema.
Jenga nchi yako, achana na negative thinking.
 
Kama kuamka kwa Watanzania itakuwa ni kuwachagua wahuni wa CHADEMA, basi ni vyema nchi iendelee kulala milele
 

uso wa nyoka;
Nisamehe bure tu kwa kusema; Sijui kama umeusoma uzi vizuri. Hizo assumptions ulizoona nimeziandika ni zipi?? Hivi kweli unataka kuniambia Watz tumekuwa wazembe kiasi hicho kwamba Askari wa JWTZ auawe kwenye mapambano kule amboni azikwe ka nyoka tu hivi hivi?? Basi Tz haiwathamini walinzi wake. Kama tulionyeshwa magari ya kivita yakikimbizwa kama hayana dereva kuelekea humo amboni, ilishindikana nini kutuonesha tu mazishi ya askari aliyefia kwenye mapambano??
Kama uliyafuatilia mambo haya, wakumbuka kuwa tulioneshwa gaidi mmoja aliyekamatwa na wachimba kokoto ambao walionekana wameva nadhiiiifu na hawana chochote mkononi?? Huyu gaidi alikuwa ameleweshwa yale mabomu au?? Fikiri kwanza kabla ya kunijibu.
Hata kama ni propaganda, aliyezitunga asilipwe chochote. Zikafa hivi hivi kama ule mchezo wa kuigiza kuwa kuna ndege imeanguka uwanjani watu wakafadhaika sana kumbe ni kipimo kuona kama tuna uwezo wa kukabiliana na janga likitokea tu. Huu ka ni mchezo watuambie, lakini kuwa ni ukweli nakataaaaaa tena aliye ubuni asilipwe chochote.
 

Nimekuelewa Mkuu, lakini hebu jaribu kufikiria, serikali ifanye maigizo ili iweje wakati zama hizi karibu kila kitu kiko hadharani?Hata mtoto wa shule ya msingi leo hii ukijaribu kumdanganya darasani atahoji, sembuse watu wazima? Kinachosumbua ni sisi baadhi ya raia kuwa na ile imani kuwa kila kinachotendwa na serikali yetu kina makusudio ya kisiasa kiasi kwamba hiyo hali imetufunika mpaka tunashindwa kuutambua mchango wa serikali katika kudumisha vitu kama amani, usalama na utulivu uliopo.
Swala la mhalifu kuvaa yeboyebo au kuwa pekupeku ni jambo la kawaida sana kwa sababu kuna uwezekano mtaji alionao ni mdogo na kama akifanikiwa atavaa suti tu na hata kama waliomkamata hawakuvaa kulingana na kazi walizotaja, huwezi kujua kuwa siju hiyo walikuwa katika shughuli gani, na pia uzingatie kuwa kutokana na vurugu zile, kwa vyovyote shughuli kama za uchimbaji wa kokoto zilisimama kwa muda kutokana na watu kuhofia usalama wao.
Mwanajeshi kuzikwa kimyakimya sidhani kama ni jambo la ajabu, labda nikuulize, umeshuhudia mara ngapi wanajeshi wakizikwa kupitia Luninga? Unaifahamu idadi ya wanaokufa katika mapambano?
Kingine ni kuwa kama unaona kuna walakini, kuna njia za kupitia uende ukahoji kilichotokea mradi uwe raia. Jeshi sio kampuni au chama cha siasa liwe linajipa promo kwa kila kinachoendelea katika shughuli zake, lazima wanazo sababu tu.
 

uso wa nyoka;
Nimekusoma vyema na najitahidi kukuweka sura niijengee maswali yangu ya moyoni. Naomba hivi; Ukizoea kudanganya danganya hata siku unasema ukweli huaminiki tena. Serekali yangu hii sikivu imezidi kuwafanya watu ndondocha.
Ahadi hewa wanazozitoa hazihesabiki. Wanaweza kukuahidi hata kukununulia ndege na usiione. Sasa watu hawawaamini tena, miye nikiwa mmoja wapo. Nisamehe bure.
Kuhusu shughuli kusimama, nakataa kwani ka shughuli zingeli simama huyo Gaidi hakujipeleka kwao kukamatwa, watu walikuwa kazini tena wawili walikuwa na zana zao za kazi.
Tatu, kuhusu askari kuzikwa kimya kimya, mbona walituonesha wale walio uawa kule DRC? Ni yupi ungelikuwa ni weye unge mfanyia media coverage? Aliyefia Congo au Ambini japo waote walikuwa kazini???
Nasema, nimejaribu kukupiga picha, sikuelewi elewi. Are yu realy piganiaring and tetearing this Government?? Siichukii ila nachukia watendaji hao magumashi
 
Kuna kitu kinaitwa false flag Ni mbinu za kuziingiza nchi ktk mambo flani kwa kisingizio flani lakini tatizo linakuwa false flag zetu zinatugawa ndani Na madhara take Ni makubwa wenzetu false flag zao Ni kumshetanisha adui wa nje huku kwetu tunawashetanisha kwa mfano siku za karibuni waislam mpaka itafikia watu wa dini nyingine wawaonie Ni maadui hata waone kuwaua Ni sawa Na mkianza kuwaua nao watajibu Na hapo ndipo kina la ugaidi litakapotimia,tatizo Ni waislam Ni nusu ya watanzania Na vita yoyote dhidi Yao haitaliacha taifa salama,huu Ni mchezo hatari zaidi kuwahi kucheza!
 

Nakuelewa unachozungumza ila wakati mwingine usichukulie kama vile serikali ni maroboti yasiyo na hisia za kibinadamu kiasi cha kutenda mambo bila kujali uhalisia wa mambo au hisia za watu.
Kama serikali ingeamua kufanya mambo ili kupotosha watu, naamini ina uwezo mkubwa sana wa kufanya hivyo na si kama mnavyochukulia kuwa wanafanya kirobotiroboti, kwa sasa huwezi kuelewa ila ukitulia ukajiuliza na kutafakari utanielewa.
Umetolea mfano wa wanajeshi waliokufa Congo, je Comoro, Sudan, na je hao wa Congo ni wote uliowaona wakizikwa?
 

Huo unabisha ndo ukweli utambanaje na majambazi wakati yako serikalini na yanatumia jeshi la polisi kukuua wewe, utapambanaje na magaidi wakati yanadhaminiwa na serikali, utapambanaje na majangiri yanayowinda watu/wanyama wakati yametumwa na ccm
 
Huo unabisha ndo ukweli utambanaje na majambazi wakati yako serikalini na yanatumia jeshi la polisi kukuua wewe, utapambanaje na magaidi wakati yanadhaminiwa na serikali, utapambanaje na majangiri yanayowinda watu/wanyama wakati yametumwa na ccm

Kwa jinsi unavyozungumza utakuwa unao ushahidi, hebu tuletee na sisi tuuone ili tujiridhishe kuwa hayo unayozungumza siyo maneno ya kutunga au kudhani.
 

uso wa nyoka;
ngoja tu niweze ku declare my interests;
Mimi simo kwenye system, ila naona kuwa weye umo kwenye system. Yaani waweza sema kitu kikaeleweka huko kwenye hii serekali.
Elewa hivi, nataka nikufahamishe kuwa sijakosea niliposema; Aliyeibuni propaganda hii asilipwe mshahara au posho yake. Hakujua tyming.
mara nyingi, hao wadau wa serekali huwa aidha nusu siku nyuma ya kila propaganda yao. Unaposema mfano wa maaskari waliokufa huko na huko kuwa je ni wote tulioneshwa, nasema sio wote ila usilinganishe 50 wakaoneshwa 5 tu ili kukidhi mioyo/ kuisuuza mioyo ya watz waliofiwa kuwa huenda yule wa kwangu ataoneshwa siku moja. Nadhani umenielewa halafu ulinganishe na askari mmoja tu aliyeuawa na magaidi akiwa kazini yaani kwenye field ya vita. Huyu usipo mwonyesha alivyo fanyiwa heshima, nasema penda usipende, huku ni kuua ari ya jeshi letu.
Huwezi onesha vifaru na mizinga uache kuonesha mmoja wa hao vinara alipoanguka na kuzikwa. Amini utakavyo ila that is not good
 
Uso wa nyoka
Unapoona nchi ina utulivu wakati majirani zake hawalali, usidhani ni bahati au imetokea tu, ujue kuna watu wanaoitunza hiyo amani hata kama huelezwi kila kinachotokea iwe mipakani au katika maeneo mengine ambako wabaya wanajaribu kuyatumia kama mwanya wa kutekeleza mabaya dhidi ya wananchi.
Vifaru na magari ya Deraya unayoyaona, ni sehemu ndogo sana ya kile kinachofanyika katika kulinda amani na mengi yanayofanyika sidhani kama utayaona kwenye TV. Na hilo si kwa nchi yetu tu, hata Mmarekani pamoja na maonyesho ya zana anayofanya kila siku, sidhani kama anaonyesha kila kitu kinachomfanya aendelee kuwa na nguvu kuliko mataifa yote Duniani. Huyo askari aliekufa, aliapa kulitumikia taifa na naamini hata alipokuwa akipambana, hilo ndilo lililokuwa moyoni mwake na sio kutafuta sifa au kung'aa kwenye TV.
 

mi mwenyewe nachukia hii tabia ya kila mtu kuilalamikia serikali kwa kila kitu aisee... kula like yangu mkuu
 
mi mwenyewe nachukia hii tabia ya kila mtu kuilalamikia serikali kwa kila kitu aisee... kula like yangu mkuu

Tuko pamoja Mkuu. Wakati mwingine tunapaswa kushukuru kwa yale serikali inayofanya na si tukubaliane na kila kitu ila kama kuna jema tulitambue.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…