Chagga Restaurant

Ehud

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2008
Posts
2,685
Reaction score
338
Wana JF nina wazo la kuanzisha Restaurant itakayouza vyakula vya Kichaga tu kama mtori,kiumbo,kishimba,machalari na kadhalika. Je hii biashara italipa kwa miji ya Dar es Salaam na Arusha? Pia kama kuna mtu anajua vyakula vingine vya kichaga ani-pm au avitaje hapa ili niviweke kwenye menu. Asanteni
 
wazo zuri lakini kwa nn visiwe vya makabila yote kama unajua mapishi yao au ukaajiri wapishi wanaoujua? bora uite jina lingine lakini sio chagga restaurant kwani dar hawaishi wachaga tu........iite Restaurant ya Kijamii au Traditional Food Restaurant
 
Wazo zuri sana Mkuu, Siku nikiwa Dar Lazima niitafute hii Restaurant. Tuambia iko wapi ili tuwe tunaitembelea.
Mi ni mpenzi sana wa Ngande kwa hiyo nadhani itakuwepo.
 

Nataka iwe ya ki-traditional zaidi lengo langu ni kutengeneza identity ya vyakula vya kichaga kama vile ambavyo Ethiopia au Chinese au India restaurant zilivyo. Vyakula vingine vinaweza kuwepo lakini nataka itambulike ni specialist wa chagga foods.
 
Wazo zuri sana Mkuu, Siku nikiwa Dar Lazima niitafute hii Restaurant. Tuambia iko wapi ili tuwe tunaitembelea.
Mi ni mpenzi sana wa Ngande kwa hiyo nadhani itakuwepo.


Usipate tabu mkuu itakuwepo ngande ya maharage na nyama wala usiwe na hofu.
 

Kiburu (ndizi na maharage inakuwa kama mtori hivi), Ngande (ndizi na soe...magimbi flani meupeeee ndani yanaotaga mndenyi huko)... uwe serious basi sio umeandika kuongeza thread ulizoanzisha tu! wateja 'regular' tupo.
 
Wakuu nashukuru kwa maoni yenu nayafanyia kazi..
 
Mkuu we fungua tuu wateja tupo nyomi,mbona tunakulaga ng'ande hapo soccer city sinza?Ila usisaha VISHA/RLEMBWE(kunde zinapikwa halafu zinasongwa) pia NGARARIMO na KITAWA kwa asubuhi sio mbaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…