Chadema yazindua kampeni kwa ‘chopa’

Chadema yazindua kampeni kwa ‘chopa’

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,578
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimezindua kampeni za udiwani kwa mbwembwe, ambapo wametumia helikopta kudondosha vipeperushi vyenye maelezo ya wagombea wao.

Madiwani hao wa kata za Kimandolu, Elerai, Kaloleni na Themi, walifukuzwa uanachama baada ya kudaiwa kukiuka maagizo ya vikao vya juu vya chama chao.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo, Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Arusha, Ephata Nanyaro alisema helikopta hiyo itaendelea kutumika muda wote wa kampeni za udiwani.

Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini, Godbless Lemay alisema hatahudhuria vikao vya Bunge kwa kipindi chote cha kampeni, kuhakikisha chama hicho kinarejesha viti hivyo.

Alisema lengo la Chadema ni kuweza kuongoza halmashauri ya jiji baada ya kukinyang’anya CCM kiti cha udiwani Kata ya Daraja Mbili, kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika mwaka jana.

CCM na Chadema zimeweka wagombea kwenye kata zote nne, lakini CUF inayoshiriki uchaguzi huo kimesimamisha wagombea katika kata tatu za Kaloleni, Elerai na Themi.

Kampeni za uchaguzi huo zinatarajiwa kugubikwa na vituko vilivyojaa ushindani kati ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) na chama hicho kikuu cha upinzani nchini. Chadema na CCM vimekuwa na mvutano wa kisiasa mara kwa mara mkoani humo.
 
Kumbe wanaamini CCM bado ni tishio arusha tofauti na ambavyo wamekuwa wakijinadi kuwa hata wakisimamisha jiwe litashinda tu
 
Lakini cdm kwa mtizamo wangu. Kama cdm wakifanikiwa kupata viti vyote vinne katika jiji la Arusha basi mayor wa ccm lazima ang,olewe tu!
 
Kumbe wanaamini CCM bado ni tishio arusha tofauti na ambavyo wamekuwa wakijinadi kuwa hata wakisimamisha jiwe litashinda tu

Arusha ccm haina chake,ccm imebaki na viongozi tu hata wanachama haina
 
Gharama ya kutumia helkopta ni shilingi ngapi?
Huu unaweza ukawa ni matumizi mabaya ya fedha
 
Matumizi mabaya ya fedha za ruzuku ambayo ni kodi yetu msajili kula nao sahani moja hawa
 
Gharama ya kutumia helkopta ni shilingi ngapi?
Huu unaweza ukawa ni matumizi mabaya ya fedha

Siyo pesa nyingi ni milioni 90 mpaka kampeni ziishe wakati wameshindwa kulipia ofisi huko Mbeya laki 3.
 
Kama Chadema imenunua mafuta ya chopa ili iwavutie wana AR, ni yupi anatumia fedha zake vibaya. Aliyenunua shehena ya mabomu ya machozi kuwatiisha wana AR huyo mnamuona alitumia vizuri pesa za kodi yangu??
Mbona jamani mna nongwa hivi?? Mnyonge mnyongeni lakin haki apewe. B/up cdm. Mungu asiye lala usingizi azidi kuwapa hekima mshinde kata zote 26 na hicho kiporo kilichofichwa hapo AR pia. Mungu ibariki TZ, Mungu ibariki cdm.
 
Kumbe wanaamini CCM bado ni tishio arusha tofauti na ambavyo wamekuwa wakijinadi kuwa hata wakisimamisha jiwe litashinda tu

ccm ni lazima wawe tishio kwa wananchi sababu ni WAUAJI,WEZI na MAFISADI.
 
ccm wahuni wanajisumbua bure archuga
 
Ni matumizi mazuri ya fedha hayo

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Jana tulikuwa na mikutano 8,kwenye kata nne za Jiji la Arusha,pamoja na kugawa vipeperushi kwa watu wa Arusha,sababu ya msingi ni kufikia lengo hilo la kufanya mikutano ya uzinduzi kwenye kata hizo,lakini pia kufikia watu wengi ambao kwa sababu kadhaa wamehama kwenye kata zenye uchaguzi,na lengo hilo limefikiwa
Hapa hakuna uoga wala matumizi mabaya ya rasilimali,
 
Mkuu Liverpool njoo uwaelimishe hawa gambaz bei ya jet A 1. Yanafikiri ni millioni kwa lita.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom