kailakarama
Member
- Aug 30, 2014
- 73
- 30
Ziara ya mwenyekiti wa taifa wa Chadema Mh. Mbowe mkoani Kigoma yawavuruga wanachama na viongozi wa Chadema Kigoma.
Baada ya Mbowe kufanya ziara mkoani Kigoma na kuzomewa katika mikutano mbalimbali ya hadhara aliyofanya mkoani Kigoma tofauti na alivyotarajia ilimlazimu kukutana na viongozi mbalimbali wa CDM katika kikao maalum kilichofanyika katika hotel ya Coast View mjini Kigoma.
Hali haikuwa shwari hata kidogo katika kikao hicho baada ya viongozi hao kutoleana matusi na kashfa mbele ya Mbowe.
Hali hiyo ilimpelekea atoke kwenye kikao na kwenda kujifungia katika chumba alichofikia na kuwaacha viongozi hao wakilumbana.
Baada ya Mbowe kuondoka Kigoma vurugu hizo zinaendelea na sasa hali imekuwa si shwari baada ya baadhi ya viongozi kuaanza mikakati ya kuuondoa uongozi uliopo madarakani kwa Kumuondoa Mwenyekiti Ally Kisala na kumuweka Yared naye katibu wa mkoa Lucas Madede kutoka na nafasi yake kuchukuliwa na Idan Ndowa.
Mapinduzi haya yanayoratibiwa na Yared Fabilaus ambaye ni mjumbe wa kamati kuu ya CDM taifa aliyedhubutu kumtukana matusi ya nguoni Meya wa manisipaa ya Kigoma Ujiji Bakari Beji mbele ya Mbowe na hakukemewa hata kidogo na Mbowe kwa matusi hayo.
Yared alikuwa anampa Mbowe taarifa za kiutendaji/ kisiasa za manisipaa ya Kigoma Ujiji inayoendeshwa na Chadema.
Chadema imeshindwa kupata wagombea katika mitaa,vijiji na vitongoji vingi mkoani Kigoma pamoja na ahadi ya Mbowe ya Tsh 300,000 kwa yoyote atakayejitokeza kugombea uenyekiti.