CHADEMA yavunja uongozi Wilaya ya Mtwara, mmoja ahamia CCM

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,720
55,852
Mkutano Mkuu wa CHADEMA Kanda ya Kusini umetengua Uongozi wa Wilaya ya Mtwara Mjini na wajumbe wote wa bodi kutokana na kutokuelewana.

=======

Chadema yavunja uongozi Wilaya ya Mtwara, mmoja ahamia CCM-VIDEO
By Mary Sanyiwa na Raisa Said, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz
Kwa ufupi

Mwenyekiti wa chama hicho wa Kanda ya Kusini ambaye pia ni Mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe alisema jana kuwa, uamuzi huo umefikiwa baada ya kumalizika kwa kikao cha ushauri na wanachama kilichofanyika mjini humo.
Advertisement

Wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kusini kikivunja uongozi wa Wilaya ya Mtwara na kuweka viongozi wa muda, aliyekuwa Mwenyekiti wa Wilaya ya Muheza mkoani Tanga, Rwebangira Karuwasha ametangaza kuhamia CCM.

Mwambe alisema wamefikia uamuzi huo baada ya kuona kuna mgogoro uliosababisha kutokuwapo maelewano tangu wakati wa Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka 2015.

“Hatuwezi kuacha watu wagombane kwa miaka miwili hadi mitatu katika eneo lao, ni lazima hatua zichukuliwe. Tumeliona hili, tumeamua kuvunja uongozi uliopita na kuweka wa muda kwa ajili ya kukijenga chama na kuangalia namna tutakavyoweza kusonga mbele,” alisema Mwambe.

Mwenyekiti huyo alisema kamati ya ushauri inaendelea na kazi kuhakikisha majina ya watu wanne yanapatikana ambao mmoja kati yao atakuwa mwenyekiti na mwingine katibu. “Watu hawa watakuwa kwenye kikosi maalumu cha mpito kwa sababu Uchaguzi Mkuu wa kikatiba wa chama utafanyika mwezi Machi mwakani na hivi karibuni tumetoka katika mikutano ya Kamati Kuu tumekubaliana uchaguzi utafanyika mwezi huo,” alisema.

Mwanachama wa Chadema katika Manispaa ya Mtwara Mikindani ambaye pia ni Diwani wa Viti Maalumu, Lulu Abdallah alisema wamefurahishwa na uamuzi huo kwa kuwa walikuwa na shida ya uongozi.

Mwenyekiti wa chama hicho katika Halmashauri ya Mtwara, Ismail Liuye alisema uongozi huo ulikaimishwa, hivyo ni sahihi kuvunjwa. Katika hatua nyingine, akizungumzia kuhamia CCM ikiwa ni siku chache baada ya Kamati Kuu ya Chadema kukutana mjini Tanga na kuvunja uongozi wa Wilaya ya Muheza, Karuwasha amesema ameamua kuhamia CCM ili kuendelea na siasa.

Akizungumza jijini Tanga jana, alisema ameamua kukihama chama hicho kwa kuwa uamuzi wa kuvunjwa kwa uongozi wao haukufuata utaratibu.

Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Tanga, Mathew Mganga alisema wamepokea taarifa kuhusu Karuwasha kuhamia katika chama chao na kwamba, wanamkaribisha kwa dhati.

Chanzo: Mwananchi
 
Ok...umeretoa taarifa kama umbea "wavuana vyeo",huenda ni utaratibu wa kawaida tu then wewe ukajua wanavuana kwa sabab u mpita njia
 
Tusisahau utabiri huu:
Uchaguzi wa ndani CHADEMA 2018/19 Utaenda na wengi.

Ndesamburo, kikwazo Uchaguzi wa Kanda ya Kaskazini CHADEMA

Wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kusini kikivunja uongozi wa Wilaya ya Mtwara na kuweka viongozi wa muda, aliyekuwa Mwenyekiti wa Wilaya ya Muheza mkoani Tanga, Rwebangira Karuwasha ametangaza kuhamia CCM.

Mwenyekiti wa chama hicho wa Kanda ya Kusini ambaye pia ni Mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe alisema jana kuwa, uamuzi huo umefikiwa baada ya kumalizika kwa kikao cha ushauri na wanachama kilichofanyika mjini humo.

Mwambe alisema wamefikia uamuzi huo baada ya kuona kuna mgogoro uliosababisha kutokuwapo maelewano tangu wakati wa Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka 2015.

“Hatuwezi kuacha watu wagombane kwa miaka miwili hadi mitatu katika eneo lao, ni lazima hatua zichukuliwe. Tumeliona hili, tumeamua kuvunja uongozi uliopita na kuweka wa muda kwa ajili ya kukijenga chama na kuangalia namna tutakavyoweza kusonga mbele,” alisema Mwambe.

Mwenyekiti huyo alisema kamati ya ushauri inaendelea na kazi kuhakikisha majina ya watu wanne yanapatikana ambao mmoja kati yao atakuwa mwenyekiti na mwingine katibu. “Watu hawa watakuwa kwenye kikosi maalumu cha mpito kwa sababu Uchaguzi Mkuu wa kikatiba wa chama utafanyika mwezi Machi mwakani na hivi karibuni tumetoka katika mikutano ya Kamati Kuu tumekubaliana uchaguzi utafanyika mwezi huo,” alisema.

Mwanachama wa Chadema katika Manispaa ya Mtwara Mikindani ambaye pia ni Diwani wa Viti Maalumu, Lulu Abdallah alisema wamefurahishwa na uamuzi huo kwa kuwa walikuwa na shida ya uongozi.

Mwenyekiti wa chama hicho katika Halmashauri ya Mtwara, Ismail Liuye alisema uongozi huo ulikaimishwa, hivyo ni sahihi kuvunjwa. Katika hatua nyingine, akizungumzia kuhamia CCM ikiwa ni siku chache baada ya Kamati Kuu ya Chadema kukutana mjini Tanga na kuvunja uongozi wa Wilaya ya Muheza, Karuwasha amesema ameamua kuhamia CCM ili kuendelea na siasa.

Akizungumza jijini Tanga jana, alisema ameamua kukihama chama hicho kwa kuwa uamuzi wa kuvunjwa kwa uongozi wao haukufuata utaratibu.

Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Tanga, Mathew Mganga alisema wamepokea taarifa kuhusu Karuwasha kuhamia katika chama chao na kwamba, wanamkaribisha kwa dhati.

http://www.mwananchi.co.tz/habari/C...ahamia-CCM/1597578-3875652-m0q3bbz/index.html
 
Inauma sana Makamanda wanakimbia jamani....

Mbowee anakiua chama....bora Mwenyekiti apewe Kamanda Boniface
 
Chadema ni chama la hovyo kuwahi kutokea duniani.

Na Mbowe hatapenya uchaguzi wa 2018 ,haiwezekani makapi ya ccm yawe chaguo la kwanza la Mbowe
 
Ccm na chadema ,,,wale wale naichukia siasa na wana siasa mmetufikisha hapa tulipo
 
Siku watanzamia watagundua kuwa Mbowe ni Mhuni wa siasa
hawata amini kupoteza muda wao,
Muda utaonge 2018
Lazima moto uwake
Tunajua Mbowe anajipa uenyekiti wa milele ndani ya chadema
lakini Lazima Kiwake
 
Back
Top Bottom